Makongoro ampigia magoti Mpendazone mahakamani afute kesi ya uchaguzi

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Dk. Makongoro aliibuka mahakamani hapo jana ghafla ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa ambapo alisalimiama na Mpendazoe, kisha baadaye wakati akiondoka, akamuomba Mpendazoe afute kesi hiyo ili mwaka 2015 amwachie jimbo hilo.

Kesi namba 98 ya mwaka 2011 inayosikilizwa na Jaji Profesa Ibrahim Juma, ilifunguliwa na Mpendazoe aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akipinga ushindi wa Dk Mahanga.

SAHIHISHO:
Wasomaji Jamii Forums, habari hii sijaiandika mimi mwenyewe, ni nukuru ya moja kwa moja kwa kudonoa kipande katika mada ndefu iliyokuwa kwenye gazeti. Aliyefanya kosa la uchapaji ni gazeti na wala sio mie. Ila ieleweka ni 2015 badala ya 2005. Nadhani ni makosa ya miss spell toka kwa wahariri na mhariri msanifu wa kurasa mara nyingi hashughuliki na mambo madogo kama haya, labda mhariri mkuu hakufanya uhakiki huu.
 
Dk. Makongoro aliibuka mahakamani hapo jana ghafla ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa ambapo alisalimiama na Mpendazoe, kisha baadaye wakati akiondoka, akamuomba Mpendazoe afute kesi hiyo ili mwaka 2005 amwachie jimbo hilo.

Kesi namba 98 ya mwaka 2011 inayosikilizwa na Jaji Profesa Ibrahim Juma, ilifunguliwa na Mpendazoe aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akipinga ushindi wa Dk Mahanga.
Mkuu edit kidogo!! Hata hivyo nimekupata, Mpendazoe aendelee kukaza uzi hakuna kufuta kesi, akumbuke tulimchagua na kura zilizoibiwa ni zetu wananchi! Pia fedha tulichanga za kusaidia mpiganaji wetu, kwa hiyo mwendo huo huo hadi mwisho!!
 
Ameshaona hali inazidi kua ngumu kwake huyu gamba,Mungu aendelee kuwasimamia hawa wasimamizi wa kesi katika misingi ya haki ili haki isipindishwe
 
Halafu 2015 ikifika atamwambia wananchi wamemwomba aendelee! Yaani siasa huwa zinafanya watu wawe kama watoto!
 
Ni mbunge wangu huyo Makongoro na kiukweli aliiba kura na hakuna maendeleo yoyote aliyoyafanya mpaka leo.Natamani aondoke hata kesho,
 
Duh, Mpendazoe kadanganywa kitoto kweli, yaani aachiwe jimbo mwaka 2005??? Na yeye kakubali kweli? Itakua maajabu ya Abunuasi ya sufuria kuzaa
 
Mwizi anaomba nini tena? Makongoro ndo aachiwe Jimbo 2015,kwasasa apishe mshindi aongoze!!!
 
Aibu zake zitamtokea puani...alipe gharama zote za kesi na yeye ajiudhulu aachie jimbo!
 
Duh, Mpendazoe kadanganywa kitoto kweli, yaani aachiwe jimbo mwaka 2005??? Na yeye kakubali kweli? Itakua maajabu ya Abunuasi ya sufuria kuzaa

Mmesoma vizuri hiyo post au mnakurupuka? Mbona sioni hiyo 2005???!!!?
 
Maji yanakaribia kumwagika hapa ngoja tusubiri mwaya tuone mwizi akinaswa mchana. Naomba msiandae vitofali au matairi na petroli bali aibu inamtosha.
 
Dk. Makongoro aliibuka mahakamani hapo jana ghafla ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa ambapo alisalimiama na Mpendazoe, kisha baadaye wakati akiondoka, akamuomba Mpendazoe afute kesi hiyo ili mwaka 2015 amwachie jimbo hilo.

Kesi namba 98 ya mwaka 2011 inayosikilizwa na Jaji Profesa Ibrahim Juma, ilifunguliwa na Mpendazoe aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akipinga ushindi wa Dk Mahanga.

Ulevi wa madaraka! Amwachie Jimbo kwani yeye ana haki milki ya Jimbo hilo? Amewashoirikisha akina John Jambele? Dr. Makongoro kweli amenusa harufu ya kubwagwa. Asidanganye hana mpango wa kugopmbea mwaka 2015 kwa kuwa ameishaona nini kitampata ndio maana hana habari tena na jimbo anajifanyia mambo yake tu.
 
Dk. Makongoro aliibuka mahakamani hapo jana ghafla ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa ambapo alisalimiama na Mpendazoe, kisha baadaye wakati akiondoka, akamuomba Mpendazoe afute kesi hiyo ili mwaka 2015 amwachie jimbo hilo.

Kesi namba 98 ya mwaka 2011 inayosikilizwa na Jaji Profesa Ibrahim Juma, ilifunguliwa na Mpendazoe aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akipinga ushindi wa Dk Mahanga.

Haki ya Mungu nilikwenda nyumbani kwake siku 4 kabla ya Uchaguzi na nilikuwa na Gari yenye bendera ya Chadema na kila akasema nguruwe kaingia msikitini.Nilikwenda kumwonya mwenyekiti wa serikali ya mtaa asipokee pesa ya huyu jamaa kwani ni mtu ninayemfahamu na rafiki yangu sana.alinielewa ila bado walinizunguka.Kura yangu waliiba nilipigia Segerea New Ambassador Skuli.Please Makongoro, La kuvunda halina Ubani na Huba huna na hisani Hukumbuki...Is a time to now...We need to enjoy new Changes. you among the spoiled needs to be hanged like Sadam...Step down for your sake
 
Back
Top Bottom