Makongoro aibuka na kudai mafisadi wako 4 ndani ya CCM

Lunyungu,

Huyu jamaa ni mjinga kupindukia yaani siamini haya aliyoyasema!

Wana tapatapa sasa hivi hamna hata mmoja mwenye usafi sasa kila mtu sasa hivi anaangalia wapi atashika ili iwe njia yake ya kuwarubini wananchi,hawajui kwamba sasa hivi tumestuki hata wenye PhD ambao tunadhani wapo makini na maslahi ya taifa kumbe wameoza woteeee
 
mahanga.jpg

Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga.

Na Na Leon Bahati

NAIBU Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga amesema makada wa CCM wanaodai kupambana na ufisadi wanapaswa kudhibitiwa ili wasikivuruge chama kwa kuwa mafisadi ndani ya chama hicho hawazidi wanne.

Akizungumza na gazeti hili jana Mahanga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alisema makada hao wasipodhibitiwa watakivuruga chama na kukifanya kipoteze viti vingi vya ubunge kwa wapinzani katika uchaguzi mkuu mwakani, kwa kudhaniwa kimejaa mafisadi.

“Hawa wanaoitwa mafisadi wako wangapi? Mbona hawatajwi?” alihoji Dk Mahanga akibainisha kuwa tathmini yake inaonyesha kuwa kelele zote za ufisadi zinawalenga watu ambao hawazidi wanne ndani ya chama hicho, na kwamba miongoni mwao, tayari wameanza kushughulikiwa.

Alipotakiwa kuwataja hao mafisadi wanne, Mahanga alisema hiyo ni tathmini yake na hakuna haja ya kutaja majina yao kwa vile wanafahamika.

Kwa kauli hiyo, Dk Mahanga anakuwa mtu wa pili ndani ya CCM kupingana na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, John Malecela ambaye Ijumaa iliyopita alitoa kauli kutaka mafisadi wadhibitiwe kwa nguvu zote, ili wasikiweke chama katika wakati mgumu kwenye uchaguzi huo. Tayari kauli hiyo imepingwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.

Lakini jana Dk Mahanga alisema ajenda ya ufisadi imekuwa ikitumiwa vibaya na watu ambao wanafikiri wanajijengea mazingira mazuri kisiasa ili washinde ubunge mwakani, lakini hawafikirii kwamba njia wanayoitumia inalenga kuiharibia CCM.

“Kuna watu ndani ya chama wamedhamiria kuiangusha CCM huku wakijifanya wanapambana na mafisadi ndani ya chama,” alisema Dk Mahanga jana katika mahojiano na Mwananchi Jumapili na kuongeza:

“Kama wapinzani wangesimama majukwaani wakisema ndani ya CCM kuna mafisadi, hakuna mtu ambaye angeshangaa kwa sababu malengo yao ya kisiasa ni kukichafua chama tawala ili kianguke na wao wachukue nafasi hiyo,” alisema Dk Mahanga ambaye pia ni Mbunge wa Ukonga.

“Suala hilo linapozungumzwa hadharani na wanachama wa CCM ni hatari. Hapa wanakichafua chama na ndio wanaosaidia vyama (vya siasa) vya upinzani,” alisema.

Naibu waziri alishauri: “Kama kuna tatizo, lipelekwe kwenye vikao na siyo kwenda kupiga kelele kwenye majukwaa na kukichafua chama machoni pa wananchi.”

Alipoulizwa kama haoni kulizungumzia suala hilo hadharani kutasaidia kuzuia ufisadi nchini, alisema: “Namna suala hilo linavyozungumzwa sasa, inaonyesha kana kwamba kuna kundi kubwa la wanaCCM wanaojihusisha na ufisadi, lakini ukweli ni kwamba watuhumiwa wa ufisadi, hawazidi wanne.”

Kuhusu kuwepo kwa mtandao wa watu ndani ya CCM waliopanga mbinu za makusudi za kuwaangusha wabunge waliopo mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya ufisadi, Mahanga alisema:

“Huo ni woga tu. Hakuna kitu kama hicho. Naunga mkono maelezo yaliyotolewa na Katibu wangu Mkuu (Yusuf Makamba) kupitia gezeti lenu (Mwananchi) toleo la leo jana akisema hayo ni mambo ya kufikirika,” alisema Dk Mahanga.

Alisema kuwa woga huo unatokana na baadhi ya wabunge kuwa na wasiwasi kwamba, wanachama wengine ndani ya CCM wanaweza kuchukua nafasi zao, hivyo kutumia suala la ufisadi kama njia ya kupambana nao.

Alitoa mfano kuwa katika jimbo lake tayari wamejitokeza wana-CCM saba wanaotaka kumrithi, lakini hapigi kelele kwa sababu anajua ni haki yao ya kikatiba na hana wasiwasi na yupo tayari kupambana nao kupitia michakato ya uteuzi ndani ya CCM.

“Hili liko wazi. Hata wengi wao mwaka 2005 kwenye majimbo yao walikuwepo wabunge ambao waliwaondoa na kuchukua nafasi zao,” alisema Dk Mahanga.

Alisema hata kama watu wachache wanaodaiwa kuwa ni mafisadi wakifukuzwa ndani ya CCM bado suala la wabunge kupata upinzani ndani ya chama litakuwa pale pale.

Aliwataka wana-CCM wenye nyadhifa mbalimbali kufahamu kuwa wapo wanachama wengi waliokuwa wanazitamani na hata sasa wanazitaka nafasi wanazozishikilia na wakati huo huo wapo wapya wanaojitokeza kuziwania.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Zamani, Cleopa Msuya amesema kwamba msimamo wa serikali kuhusu mafisadi unajulikana na tayari vyombo vyake husika vimeanza kuwashughulikia, hivyo akataka visiingiliwe,viachwe vifanye kazi yake.

“Mimi sina cha kusema juu ya hilo tatizo, tunaandika sana, hebu tuviachie vyombo vya utekelezaji vifanye kazi yake,” alisema Msuya ambaye alikuwa waziri mkuu katika utawala wa serikali ya awamu ya kwanza na ya pili.

Ndio wabunge vijana hao ambao tunajipa moyo kuwa watabadili CCM. Mbaya zaidi wapo wengi wengine waja na angalao hawa wamesaliti mafunzo ya Mwalimu, miiko na hata fkira za utanzania. wanaokuja 2010 hawajui Fikira, Miiko wala Dira, kwao wao ni UHESHIMIWA (POWER) MBELE KWA MBELE...

omarilyas
 
ila huwa anajitahidi sana kutetea mafisadi, nasikia alikuwa ktk kikao cha EL pale dodoma kupanga mikakati ya kumsafisha

H O N G E R A S A A N A
 
Kishoka umesahau kuwa Makongoro ana PHD fafa so na huo ni upeo wake ktk huo ufafa wake.
 
Wana jf, mesahau sera za CCM? nikuangalia maslai ya chama kwanza sio maslai ya taifa. wanaendelea kulindana.
 
Humu jamiiforum tuwe wa kwanza kutowapa hawa jamaa title feki. Huyu ni MR. MAKONGORO MAHANGA sio DR!! Au ndio maana wanatumia initials DK sio DR?
Kwanza bidi tuwaweke wote kwenye list halafu admin aifanye sticky pale juu ili tuwe na reference!!!
 
Geoff;

Huyu jamaa ana degree ya kwanza na ya pili nzuri tuu, pia ana CSP (T) ile professional award ya materials management and procurement.

Sasa akajipa u Phd kutoka chuo feki. Akaharibu kila kitu.

Inachotakiwa ni kuitwa kwenye vikao vya chama awataje hao mafisadi. Ila kwa upeo wake ukimuuliza atakutajia wale waliojiuzulu (mawaziri) watatu na Rostam Aziz.

Hao ni rahisi sana kuwataja ukiwa ndani ya CCM.

Hili suala si la chama, kama anajiamini anatetea maslahi ya Taifa awataje publicly. Huko ndani ya chama chao wanajua huo uozo. Kumbuka vile vikao vya Butiama Mkuu, ni upuuzi mtupu.
 
Makongoro Ni mbunge wangu wa jimbo la Ukonga, huyu bwana vikao vyake vya mikakati alikua anavifanyia pale banana, kuna bar moja maarufu inaitwa ANGELS BAR, au Tarime bar almaarufu kwa Chota, hapa ndipo alipokua anaanzishia mashambulizi na alipata msaada mkubwa wa Wakurya na wajaluo wanaoishi kipunguni.....bado mbinu zake tunazifatilia, ila naamini uchaguzi mkuu ujao atadondoka kama wapinzani wake ndani ya chama watajipanga vizuri, au kama mission ya wapinzani kuchukua majimbo yote ya Dar es salaam itaungwa mkono na umma,

Kifupi hupaswi kumshangaa Mahanga ila tushangae sisi wana Ukonga tuliemweka madarakani,

Elimu na madarasa yake aliohudhuria hayakutosha kumfuta ujinga, bado ana kiwi cha macho machoni.
 
Yeye ndo fisadi ndo maana anawatetea. Watu kama hawa hawatakiwi ktk zama hizi. Anajikomba kwa wakubwa zake mnafiki mkubwa huyu. hovyooo!
 
Huyu Makongoro naona anatafuta jina tu katika siasa za Tanzania, yeye anasema hao mafisadi mbona hawatajwi wakati yeye mwenyewe anashindwa hata kutaja hao wanne anaowasema, nafikiri sitakosea nikimuita huyu jamaa mjinga kwani naona anachoongea hapa ni pumba tu, if you get nothing to talk about just shut up and enjoy your bonuses from CCM and Bunge....huyu ni mnafiki na mzandiki mkubwa.
 
Geoff;

Huyu jamaa ana degree ya kwanza na ya pili nzuri tuu, pia ana CSP (T) ile professional award ya materials management and procurement.

Sasa akajipa u Phd kutoka chuo feki. Akaharibu kila kitu.

Inachotakiwa ni kuitwa kwenye vikao vya chama awataje hao mafisadi. Ila kwa upeo wake ukimuuliza atakutajia wale waliojiuzulu (mawaziri) watatu na Rostam Aziz.

Hao ni rahisi sana kuwataja ukiwa ndani ya CCM.

Mkuu FP, saafi sana strong analysis.

Respect.

FMEs!
 
Makongoro Ni mbunge wangu wa jimbo la Ukonga, huyu bwana vikao vyake vya mikakati alikua anavifanyia pale banana, kuna bar moja maarufu inaitwa ANGELS BAR, au Tarime bar almaarufu kwa Chota, hapa ndipo alipokua anaanzishia mashambulizi na alipata msaada mkubwa wa Wakurya na wajaluo wanaoishi kipunguni.....bado mbinu zake tunazifatilia, ila naamini uchaguzi mkuu ujao atadondoka kama wapinzani wake ndani ya chama watajipanga vizuri, au kama mission ya wapinzani kuchukua majimbo yote ya Dar es salaam itaungwa mkono na umma,
Kifupi hupaswi kumshangaa Mahanga ila tushangae sisi wana Ukonga tuliemweka madarakani,
Elimu na madarasa yake aliohudhuria hayakutosha kumfuta ujinga, bado ana kiwi cha macho machoni.

- Duh! Papa Sam babu kubwa kumbe na wewe ni wa home saafi sana tupo pamoja, kumbe na wewe unawashitukia wale watu wakurya wa Kipunguni yaani familia ya Mahende waliofilisi ule mradi wa wananchi wa-Denmark wa vifaranga vya kuku pale kona ya Air Aviation, na kuanzisha mashirika ya malori na mabasi, sasa wanaamua nani awe mbunge na nani asiwe! Unajua hawa jamaa ndio waliompa ubunge Chale Kajege kule Mwibara, sasa tizama yaani kwa hela zetu wenyewe wananchi wa Tanzania, that is incredible!

- Mahanga alimshinda Rupia, another joker aliyeahidi kuleta maji pale jimboni kwetu lakini alipochaguliwa hakurudi tena mpaka uchaguzi ulipofikia ndio akajitokeza tena, halafu Mahanga kumbuka alikuwa na support ya Mkapa baada ya kumkarabatia nyumba yake bure pale Sea View na alikuwa kiungo muhimu sana kwa Mtandao.

Otherwise, strong analysis na keep it up unajua umegusa home kabisaa yaani County ya Segerea, inayoundwa na kata za Kinyerezi, Majumba Sita, na Sitaki shari, Kipunguni, Vidunda, na Airwing.

Respect.

FMEs!
 
yeyote anayemtetea mwizi ni mwizi pia, yeyote anayemtetea kibaka ni kibaka pia, na yeyote anayemtetea fisadi ni fisadi pia... kila mwamba ngoma, ngozi huvutia kwake na samaki mmoja akioza wote wameoza hivyo ccm wote ni mafisadi na wote wameoza maana wamewakumbatia, wanawatetea na kuwalinda mafisadi...

ingekuwa awamu ya mzee kifimbo... ile tu ukikisiwa na shombo ya ufisadi au kutotimiza wajibu ipasanyo ungekaa chonjo na kuwekwa kando... ccm ya leo au ccm ya wana mtandao hii ni ndoto za kimweli na hadithi za alinacha... ccm imekuwa sikio la kufa...
sijui ni lini manjonjo na malimbwata ya kifimbo cheza na kalingu yeye yataiamsha ccm usingizini ili ianze kuweka kando mafisadi badala ya kufungua matawi mpaka maka!
 
ingekuwa awamu ya mzee kifimbo... ile tu ukikisiwa na shombo ya ufisadi au kutotimiza wajibu ipasanyo ungekaa chonjo na kuwekwa kando... ccm ya leo au ccm ya wana mtandao hii ni ndoto za kimweli na hadithi za alinacha... ccm imekuwa sikio la kufa...

- Mkuu haya maneno mngekua mnayaacha jamani, hawa mafisadi hawakuzaliwa after 1985.

Respect.

FMEs!
 
Makongoro Ni mbunge wangu wa jimbo la Ukonga, huyu bwana vikao vyake vya mikakati alikua anavifanyia pale banana, kuna bar moja maarufu inaitwa ANGELS BAR, au Tarime bar almaarufu kwa Chota, hapa ndipo alipokua anaanzishia mashambulizi na alipata msaada mkubwa wa Wakurya na wajaluo wanaoishi kipunguni.....bado mbinu zake tunazifatilia, ila naamini uchaguzi mkuu ujao atadondoka kama wapinzani wake ndani ya chama watajipanga vizuri, au kama mission ya wapinzani kuchukua majimbo yote ya Dar es salaam itaungwa mkono na umma,

Kifupi hupaswi kumshangaa Mahanga ila tushangae sisi wana Ukonga tuliemweka madarakani,

Elimu na madarasa yake aliohudhuria hayakutosha kumfuta ujinga, bado ana kiwi cha macho machoni.

Lawam,a ziende kwa wakurya wa Gongo la Mboto walio ikumbatia CCM .Mambo yafanyike kama Tarime
 
Back
Top Bottom