Makongamano ya vijana wasio na ajira

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,566
Hello JF,

Niko huku Katavi ndani ndani,so mambo mengine yananipita..lol

Sijui kama yalishawahi kufanyika ila ningependa kupendekeza yafanyike makongamano ya vijana wasio na ajira.

Yahusishe pia vijana wanaomaliza masomo yao wapate kuelewa what to expect baada ya kuhitimu masomo yao.

Kisha Mashirika mbalimbali yatume wawakilishi wao, vijana wanaokua interested kwa mfano kufanya kazi na TTCL wanawaona mwakilishi wa kampuni hio ambae atawaelekeza nini kinahitajika zaidi kwenye kampuni kama hio ama kama kuna vacancies ambazo zipo then wanapewa hao vijana.

Lengo ni kuwakutanisha employers na hao vijana...inaweza ikawa kama hiring event.

Pia currently kuna 'mismatch' kati ya education na demands placed by the job-market.

Hii inaweza kutatuliwa as waajiri wataweza kutoa specific skills,experience na knowledge inayotakikana.

But i also believe in social enterprenuarship.

Kwamba matatizo ya vijana yatatuliwa na vijana wenyewe,,so kwa kila kongamano,kuwe na njia ya ku collect ideas kama vile proposals specific ku address tatizo la ajira nchini.

Wanaoleta proposal nzuri wawezeshwe kifedha na usimamizi kutoka kwa experts.

Kwa mashirika yanaoajiri kwenye hizi events wapewe punguzo la kodi.

Vipi hili wazo?nimepuyanga au?

Becky
 
Kabla ya kusema wakutanishwe eti walio hitimu...labda
Yafanyike makongamano ya wataalam na watunga sera

Waulizane yafuatayo..

Kozi zinasomeshwa kwenye vyuo vingi zinaendana na mahitaji ya Taifa?

Mahitaji ya dunia?

Una maelfu ya vijana Wana degree za social work, sociology, records na takataka zingine..
Je haya ndo mahitaji ya dunia na Taifa?

Halafu hata hao waliosomea Engineering na medicine mfano...tunaweza kweli kuwapeleka kwenye soko la ajira la kimataifa na wakafika huko wakaonekana kweli ni 'graduates'?


Au ndo Yale ya msomi anandika jinalake 'Loda' badala ya Rhoda na Lozi badala ya Rose
Hapo bado hujampa dakika 5 za kujieleza kwa kingereza
 
Kipindi cha nyuma, vyuo vilikuwa vinawakutanisha wanaohitimu na wanaotoa ajira na kufanya mdahalo au kongamano, na baadhi ya vyuo vilikuwa vinapambana vijana wao ata baadhi waweze kuajiriwa; lakini kwa sasa vyuo vimekuwa vingi na vinajiendesha kibiashara na si kumtafutia muhitimu fursa; muhitimu baada ya kupata cheti akapambane na hali yake.
 
Kipindi cha nyuma, vyuo vilikuwa vinawakutanisha wanaohitimu na wanaotoa ajira na kufanya mdahalo au kongamano, na baadhi ya vyuo vilikuwa vinapambana vijana wao ata baadhi waweze kuajiriwa; lakini kwa sasa vyuo vimekuwa vingi na vinajiendesha kibiashara na si kumtafutia muhitimu fursa; muhitimu baada ya kupata cheti akapambane
 
Ninachoweza kusema ni mfumo wa elimu tulio nao. Tunafundishwa kuajiriwa sio kujiajiri hapo ndipo panapokuwa pagumu.
Pia na fani tunazosoma, mfano aliyesoma 'Human Resource', 'Public administration', 'Records management', 'Secretarial',' logistics', 'procurement' , 'land planing', 'accounts' n.k unategemea wajiajiri?
 
Wazo zuri. Pengine vijana wenyewe wangekutana na kufanya makongamano. Wakisema serikali iwafanyie nini ili waweze kujiajiri. Labda wafanye kimikoa au kiwilaya sababu mazingira hutofautiana.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom