Makondakta wa Dar huibia wananchi kwa njia hii

Kajolijo

JF-Expert Member
May 30, 2016
3,364
4,606
Leo nikiwa nasafiri kwenye daladala kutoka Temeke nimegundua namna makonda wa magari wanavowaibia wananchi kupitia nauli zao.

Kwanza ukipanda mfano kutoka Temeke kwenda Tuangoma nauli kwenye tiketi n tsh 450 lakini wao haijalishi unashukia wapi nauli iko palepale ukibisha wanakuambia angalia tiketi imeandkwaje. Pia nmepanda toka Tuangoma hadi Kibada lakini nmetozwa nauli ya Feri yaani tsh 600 badala ya mia nne au mia tano, nilipobisha wakanimbia kuwa tazama tiket imeandikwa bei gani.

My take:
Je huu ndio mfumo mpya wa awamu hii? Maana kipindi cha nyuma ilkuwa ukushukia njiani unatoa mia nne. SUMATRA mnalijua hili? Na kama mnalijua kwanini hamjatuambia kuwa bei au utaratibu umebadilika?
 
Du ni zaidi ya ugumu 600-150=450 hapo unachokilalamikia ni 150 tu hata mtoto wako pipi hapati
 
Du ni zaidi ya ugumu 600-150=450 hapo unachokilalamikia ni 150 tu hata mtoto wako pipi hapati
Hapo ndiyo kuna tatizo kubwa. Si hela ndogo hiyo. Anafanya kwa wangapi siku nzima?
Fikiria mwenye gari anaruka vituo vingi kufuata sehemu yenye unafuu wa Shs 40 kwa lita moja. Ni Shs 400 kwa lita kumi! Shs 2100 kwa week na Shs 8400 kwa mwezi!
 
dawa yao ni unakua na pesa ya chenji chenji...unampa mia nne keshi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom