Makonda: Wasio na Kitambulisho cha Taifa wala Namba Mkoani Dar, waliendekeza umbea

"Watu wanajua nyumba za wageni bila kuelekezwa kuliko wanavyojua vitambulisho vya NIDA Watu mnapenda umbea kuliko maisha yenu" By Bashite
Hiv mfano ukasajiliwa laini kwa jina la mtu mwingine kisheria ikoje? au hakuna chochote kitachotokea
 
Fatilia habari kuanzia mwanzo!!
"Ili uweze kusajili laini ya simu kwa alama za vidole ni lazima uwe na kitambulisho cha Taifa au namba. Kesho Jumapili Januari 20, 2020 laini za simu ambazo hazijasailiwa kwa alama za vidole zitazimwa." C&P
Narudia tena leo ni tarehe 20/01 /20 siku ya Jumatatu.
 
Juzi umesikika ukisema kule Temeke kuwa Watu wa Dar wanapenda sana umbea kuliko hata habari za NIDA.
Hapo ndio nikakumbuka mapenzi yako na mzee juu ya kipindi cha SHILAWADU cha Clouds TV.

Kipindi hiki ambacho maana yake ni Shirika LA Wambea Duniani (tafsiri ni yao)/ mzee alitamka wazi hadharani kuwa anapekipenda sana kukitazama.

Na wewe sababu kubwa ya kugombana na Clouds hadi kuingia studio na bunduki ni kuhusu mada uliyopeleka kwenye kipindi hicho (umbea) na haikurushwa. Umbea huohuo wa kule Clouds ulisababisha Waziri Nape apoteze uwaziri wake.
Hayo ndio mapenzi yako kwenye kipindi cha umbea yalivyo dhihirika wazi.

Je, mwishimiwa Makonda huoni mapenzi ya watu wa Dar juu ya kupenda Umbea ni kufuata nyayo zako na za mzee? Hudhani kuwa hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi?
 
Huyo jamaa anawashwa washwa. Yaani waache.kuongoea TCRA anaongea yeye. Afunge hilo bakuli lake.
 
"Watu wanajua nyumba za wageni bila kuelekezwa kuliko wanavyojua vitambulisho vya NIDA"

Nyumba za wageni zipo kila mtaa tofauti na NIDA mpaka uifungie safari kwenda Wilayani.
 
Back
Top Bottom