Makonda: Wanaopora mali za watu wapewe kipigo cha kimataifa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
0e8bbc00b2be3ffd52997ed8d34c033b
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Pual Makonda amewataka wananchi kuwachunga watoto wao kwani kuna wimbi la vijana waporaji pamoja wanaoiba vifaa vya magari ambalo limeuka hivi karibuni.

"Uibe tekino au pochi haina kitu tutakuhesabu kama mwizi wa Dreamliner, kipigo chako ni cha Kimataifa. Wale mnaotaka kuonja nafasi ya ukibaka kama ni nzuri onjeni na tusilaumiane, hakuna mtu yuko tayari kuharibiwa kazi kwenye hiki kipindi cha mwisho tunafunga mahesabu"

Akizungumza na wakazi wa wilaya ya Temeke katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo, RC Makonda amesema matukio ya wizi mdogo mdogo wa vitu kama power windows yameongezeka jijini ambapo amemtaka Kamanda wa Polisi kuhakikisha hali inakuwa sawa.
 
Dawa ya mwizi akikamatwa mnampeleka mbinguni kwa baba muumba.
Ukimpeleka Polisi ndo nyumbani,jela bustani anaenda kupunga upepo.
 
Inamaana wanaelwa kabisa tunavyopata shida na hawa vibaka ila hua hawataki kuchukua hatua wanasubiria finali ifike wasiharibu kazi?
Kazi ya serikali ni kutoa kpigo cha kimataifa? Hizi kauli ukichanganya na ile ya wapigwe tu, unaona kabisa tuhuma nyingi kwamba huko wamebobea kupiga kimataifa na kuna uwezekano wanaenda mbali zaidi ya hapo zina ukweli.
 
Hiki ni kipindi cha mwisho wanafunga hesabu ya "kutesa watu".
Means kuna idadi walipewa haijatimia.
 
Na wale viongozi waliopora mali za wafanyabiashara vipi? Kuna wafanyabiashara waliporwa pesa zao na wakubwa flani kwa kutumia vyeo vyao tena kwa vitisho!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom