Waziri Mwakyembe amshukia Diamond. Asema umarufu utamgharimu, hawezi bishana na Shonza na atapotea kubishana na Serikali

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
FB_IMG_1521606740815.jpg
WAZIRI MWAKYEMBE AKERWA NA KAULI ZA DIAMOND

Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kukerwa na mwanamuziki Diamond Platnumz kutokana na kumdharirisha naibu wake Juliana Shonza wakati akihojiwa katika kipindi cha The Play List cha Times FM na mitandaoni.

Katika maelezo yake Mwakyembe amesema inaelekea sasa Diamond ameanza kulewa umaarufu sasa. Kuhusu hoja ya vikao anavyodai mwanamuziki huyo Mwakyembe amesema kuwa “kama ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, haijalishi ni maarufu kiasi gani."

"Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake," amesema Mwakyembe.

Aidha Waziri Mwakuembe amemalizia kwa kumshauri mwanamuziki huyo kuwa "Si busara kwake kushindana na Serikali, na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya. Sijafurahishwa hata kidogo."

1526C4D4-AA14-4692-889C-6FBF11584536.jpeg


Rejea hapa:
Diamond Platnumz ndani ya Times FM: Ukinifungia nyimbo haunipunguzii kitu nitafanya show hata nje

Shonza: Siwezi kujibizana na Diamond

Diamond arudisha dongo lingine kwa Naibu waziri wa Sanaa Juliana Shonza
 
Tulisema sifa za kijinga zitamtokea puani, huwezi tunishiana misuli na serikali hata siku moja.

Hawa sio clouds au babymama zake, Shonza ni serikali hata kama watu hawamkubali, vita nae ni vita na serikali, kwenye hii vita dayamondi is doomed to fail. Achukue hatua
 
Kayaongelea wapi hayo Maneno Mwakyembe!

Mwakyembe na Diamond Nani alichangia Rais Magufuli kupata kura nyingi zaid?

Mwakyembe asikurupuke, Zitto aliwahi kusema ukiona Kifaranga kinapata ujasiri wa kuruka ruka mbele ya Kunguru ujue Mama yake yuko around

Mwakyembe ataitwa 'kupatanishwa' na Diamond ndipo atapojua kuwa kuna Wafanyakazi na wenye kazi yeye Ni Mfanyakazi tu!
 
Kayaongelea wapi hayo Maneno Mwakyembe!

Mwakyembe na Diamond Nani alichangia Rais Magufuli kupata kura nyingi zaid?

Mwakyembe asikurupuke, Zitto aliwahi kusema ukiona Kifaranga kinapata ujasiri wa kuruka ruka mbele ya Kunguru ujue Mama yake yuko around

Mwakyembe ataitwa 'kupatanishwa' na Diamond ndipo atapojua kuwa kuna Wafanyakazi na wenye kazi yeye Ni Mfanyakazi tu!
Hahahaa........ Umenikumbusha Ruge!
 
Back
Top Bottom