Makonda ukipiga marufuku na haya Hakika Itapendeza

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Makonda popote ulipo yamulike haya; miundo mbinu inajengwa Kwa gharama kubwa lakini huharibiwa Kwa uzembe;
Ufugaji Wa mifugo mingi maeneo ya mjini hususani jijini dar es salaam huchangia Kwa kiasi kikubwa uharibifu Wa miundo mbinu hususani barabara.
Kwato za Ng'ombe huchimbua barabara na kupomoa kingo za mitaro, pamoja na hayo pia mifugo imekuwa chanzo cha kuvunja alama za barabarani kutokana na ng'ombe kuegemea/kujikuna kwenye Nguzo za alama barabarani.
Pamoja na kero Kwa watumiaji wengine Wa barabara mifugo huleta uchafuzi Wa mazingira Kwa maeneo ya mijini ikiwemo vumbi na vinyesi!
Ni wakati wako mkuu Wa mkoa piga marufuku ufugaji maeneo ya mijini!
IMG_20171119_161623.jpg
IMG_20171119_161612.jpg
IMG_20171119_161606.jpg
 
nani kakuambia huko unapokaa ni mjini?sijawahi kuona ng'ombe mjini, mazingira yenyewe yanaonyesha siyo mjini, mtu unaishi huko pugu ma kibamba ndani nani unadhani ni mji
Mkuu inaelekea ww ni mgeni, mbezi tank bovu mifugo kibao, haya nenda temeke mifugo ipo, vingunguti, buza, kigambon, hadi magomeni kote ni vijijini mkuu?
 
Sitasahau siku nilipokutana kundi la kondoo nilipowapigia honi, kondoo mmoja akapiga kichwa taa ya gari yangu ikavunjika.
Usiwapigie honi wanyama. Ni balaa.
Hata ukipita kwenye hifadhi za taifa hutavuka salama. Tembo, faru na nyati watakufanyizia.
 
Back
Top Bottom