Wong Fei
JF-Expert Member
- Apr 13, 2016
- 4,816
- 6,459
Hili zoezi la “TOKOMEZA MADAWA YA KULEVYA” nililipenda sana inaonesha ni kwa jinsi gani kiongozi wetu wa mkoa anavyowajali watanzania. Hongera sana Mh. Makonda, na pongezi nyingi ziende kwako.
Zoezi lako la TOKOMEZA MADAWA YA KULEVYA umelifanya kwa njia isiyo nzuri kabisa japo nia yako ilikuwa nzuri. Makosa niliyoyagunduaa kuhusu operation yako umetumia njia za mkato na pia hukujiandaa kulifanya zoezi hili na lilikuwa la kisiasa zaidi.
Njia ya kuwaita watu waje kituo cha polisi na unampangia na siku ya kuripoti ni njia ya mkato. Kama mtu anafanya biashara hiyo si utakuwa umempa fursa ya kuyaficha. kuwahoji na kisha kuwaachia bila kupata kithibitisho chochote halafu sisi huku wananchi tunaamini kuwa hawa ndiyo wanatuharibia vijana wetu tunashindwa kukuelewa kabisa. Mfano kwa Gwajima. Njia uliyoitumia ni ya mkato huku umesahau kuwa hili ni zoezi ni la hatari na gumu ambalo hata Marekani na Mexico ambako kuna magenge ya madawa ya kulevya hawajaitumia njia hii.
Zoezi hili umelifanya bila ya kujiandaa na umelifanya kisiasa kabisa kwa sababu muhalifu hambembelezwi Mheshimiwa. Ungefanya uchunguzi wa kina kwa mtu anayetuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya na baada kupata details zote mnamfanyia surprise tu nyumbani kwake au ofisini kwake anao huo mzigo na kisha mnamchukua na madawa ya kulevya yake, mnampeleka jera moja kwa moja tena kifungo cha maisha na siyo mahakamani sababu kithibisho anacho kama wanavyofanya China.
Mh. Makonda wantazania tunahitaji hiyo list ya wauzaji wa madawa ya kulevya na hukumu zao sababu uliwatangaza kwenye media na sisi tunahitaji tupate mrejesho kupitia media. Hatutegemei umkute muuza madawa ya kulevya kisha umlipishe faini tu halafu umuachie hilo ni kosa kubwa sana na inapaswa uwajibishwe kwa sababu ataendelea na biashara yake. Siku zote wauza madawa ya kulevya hunyongwa au hufungwa kifungo cha maisha sababu wanaharibu nguvu kazi ya taifa. Kama alivyosema Mh. JOHN POMBE MAGUFULI kuwa Mtanzania atakayekamatwa nje ya nchi na madawa ya kulevya anyongwe kwahiyo na sisi hatutegemei mtawaachia kwa kuwalipisha faini.
Mheshimiwa Makonda wala usijichoshe kwa sababu hili zoezi halihitaji nguvu bali akili. Wewe dili na polisi na watumiaji wa madawa ya kulevya (mateja) hao ndiyo wanawajua wahalifu. Ongea nao kiutu uzima watakuambia tu. (Kama file la kesi ya jamii forum limepotea mahakamani, sehemu ya ulinzi) watashindwa kukutajia wahalifu?