Wenzako waliusoma mchezo mapema wakajua huwezi kufika popote, wakasusa ukabaki peke yako, hakuna cha waziri wa mambo ya ndani wala naibu wake, sikumuona waziri wa Afya angalau kuwapokea kina Chidi Benzi, hadi wabunge wa chama chako wamekususa, kama yangekuwa matakwa yake kamanda Sirro usingemuona.
Alipoteuliwa Rogers Sianga haraka haraka wenye akili tukajua mchezo umekwisha.
Next time unapoambiwa kutekeleza jambo jaribu kujiongeza, angalia ukubwa wake, ukiona linakuzidi kimo kuwa muwazi kama unavyojinasibu sema siwezi, wenzako wameshakusoma wanakufanya mbuzi wa kafara, mzigo mzito mpe mnyamwezi.
Ona sasa umejijengea maadui wengi tena wa hatari, watu uliowachafua hata kama tayari walikuwa wachafu watakapoanza kuyakung'uta matope lazima yatakurukia, ingawa ulisikika ukisema huogopi hata ikibidi kufa, lakini jiulize mwenzako nani alikuwa tayari kufa nawe, ndugu yangu angalia utakuja kufa peke yako, usione watu wakikupongeza wakisema wewe ni shujaa ukajaa kichwa ukafikiri wote ni wema wengine wanataka ushindwe.
Ni hayo tu kwa leo, Alamsiki.