Makonda akabidhi ofisi kwa RC Kunenge, adai ofisi hiyo ina majungu mengi

Duduvwili

JF-Expert Member
Jan 31, 2015
3,872
3,792
Wakuu Shalom naona mubashara hapa RC Matata Bwana Makonda akidai kua anafurahia sana kwenda kumtunza Mwanae na kwamba hajapoteza lolote na amedai70% ya wananchi wa Dar ni wambea uzi tayari ntazidi kuwajuza.

=======

Capture.PNG

NISAMEHENI NILIPOENDA KINYUME NA MAPENZI YENU. MAADAMU YESU NINAYE, MUSIWE NA SHAKA NA MIMI
Ninaamini, wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, ninaamini nimetumia uwezo wangu wote; nimetumia akili zangu zote, na nimetumia kipaji changu chote, na hatimaye ninaamini mwendo nimeumaliza vizuri.

Kama binadamu naweza kuwa na mapungufu yangu, na mapungufu mengi niliyokuwa nayo, inawezekana kutokana na wewe kutokuwa na taarifa sahihi juu ya kile tunachokiamua, lakini munisamehe pale nilipoenda kinyume na mapenzi yenu. Lakini, mukielewa kuwa nilifanya kwa mapenzi mema ya kuwatumikia wananchi wangu wa Dar es Salaam.

Niwahikishie ninayo furaha ya kutosha na nina amani ya kutosha, na wala msisite na maneno ya watu ya kwamba “Ataishije?” “Ataenda wapi?”. Mungeumia Zaidi na munapaswa kuumia zaidi siku mukisikia Makonda amemuacha Yesu. Lakini maadamu Yesu ninaye, musiwe na shaka na mimi, maisha yangu yapo kwenye mikono salama.

70 % YA MKOA HUU [DAR] NI WAMBEA, WANAPIGA MAJUNGU SANA
Nikupongeze RAS mpya. Nami nina matumaini makubwa kuwa utamsaidia kaka yangu kwa utumishi uliotukuka ili jiji hili liweze kwenda vizuri. Asilimia 70 ya huu mkoa ni wambea. Seventy percent ni wambea, na wanapenda umbea kuliko chochote kile. Usikubali wakakuchonganisha na RC wako. Watakutafuta wewe wakupe taarifa mbaya za RC, watamtafuta RC wampee habari mbaya za kwako wewe RAS – msikubali! Lazima mubaki focused kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Wanapiga majungu sana hawa msiwaone hivi. Wanamjua mtu kuliko hata anavyojijua yeye, lakini wewe endelea kuwa focused na utumishi. Rais amewaamini, anaamini mutamsaidia kwenye utumishi wake, na hasa katika kuwatumikia wanyonge wa Mkoa huu wa Dar es Salaam.

NITASHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU, 2020
Ukishakuwa mstaafu unarudi kwa wanakijiji wenzako…, tutakaa na wananchi wenzetu tutakuwa tunashauriana namna ya kufanya mambo ya pale

Nafahamu kwamba upo mchakato unaoendelea katika ngazi ya Wilaya, mkoa na ngazi ya taifa. Lakini kazi yetu kama wanaCCM, ambalo hili haliwezi kufichika, na hili RC ulitegemee sana. Nitapiga debe mtaa kwa mtaa, kata kwa kata, tarafa kwa tarafa, wilaya mpaka mkoa kuhakikisha kwamaba Dkt. John Pombe Magufuli anaibuka kidedea kwenye mkoa huu wa Dar es Salaam, wabunge wanashinda wa Chama cha Mapinduzi.

Sasa hivi mimi ni raia lakini lakini kadi yangu ya CCM haijapotea. Nasubiria wakati tu. Kama ni kuniona tegemeeni kipindi cha kampeni nikiungana na Mwenyekiti wangu wa Mkoa na Mwenyekiti wangu wa Wilalya ya Kigamboni tukisaka kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020 wa Rais, Wabunge na Madiwani.

NIKIJA [OFISI YA MKUU WA MKOA] BASI NI MWANANCHI WA KAWAIDA KUPANGA FOLENI
Mheshimiwa RC nasema kwasababu ndio naaga na sitegemei tena kurudi katika nafasi hii katika ofisi hii, Nikija basi ni mwananchi wa kawaida kupanga foleni pale na kuweza kusikiliza lakini naamini haya yote tunafanya kwasababu mwenyezi Mungu alitupa nafasi ya Uhai.

UPIMAJI WA TEZI DUME NI ZOEZI NINALOSIKITIKA KUONDOKA MADARAKANI BILA KULITEKELEZA
Eneo moja ambalo bado ambalo nalikumbuka na sijalifanya kwakweli, na moyo wangu unaweza kuwa unajuta na kujisikia vibaya, ni suala la tezi dume kaya kwa kaya. Nilitamani sana kulifanya, lakini kwasababu ya ratiba na muingiliano wa mambo mengi, tumekwama.

Kansa ya tezi dume inatesa sana watu. Ukipita kwenye idara ya afya utaona takwimu watu wengi wanavyopata shida. Shida kubwa sana. Ndoto yangu ilikuwa ni kuanzisha utaratibu wa kupita kaya kwa kaya kupima, kwasababu watu wanaaminii wakienda hospitali au sehemu Fulani itakuwa ni aibu. Lakini nilitamani niwafuate wananchi kwenye makazi yao.

Laiti ningelipata nafasi, ningefurahi sana kwamba kila kaya tungepima tezi dume. Na watu wanafikiri tezi dume ni kwa wanaume tu, la hasha! Hata wanawake wanapata tezi dume. Si ugonjwa wa aibu, si ugonjwa wa jinsia moja, lakini ni ugonjwa hatari unaoua Watanzania wengi.
 
Tukio liko mubashara Clouds tv karibu.

Up dates;

Makonda anasema alikuwa hafanyi kazi kwa kukurupuka maamuzi yake mengi aliwashirikisha RAS Kunenge na RPC Mambosasa

Makonda anasema baada ya kustaafu ataendelea na maisha yake ya kawaida huko nyumbani kwake kigamboni na milango iko wazi kwa yoyote yule atakayehitaji ushauri wake.

Kadhalika amemtaka RC Kunenge na RAS mpya kuwa makini sana na watumishi kwani ofisi hiyo imejaa wapiga majungu.

Makonda amemkabidhi Kunenge Ilani ya uchaguzi na amemtaka asimwangushe katika kuitekeleza.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hii ndo inadhihirisha Dar ni Jiji linaloshikiria roho ya Nchi ofisi imekbidhiwa utadhani Laizer anatoa madini kwa serikali tukio live kabisa.

1. Mh Rais Magufuli
2. Mh Samia Suluhu
3. Mh Kassim Majaliwa
4. RC wa Dar
 
Tukio liko mubashara Clouds tv karibu.

Up dates;

Makonda anasema alikuwa hafanyi kazi kwa kukurupuka maamuzi yake mengi aliwashirikisha RAS Kunenge na RPC Mambosasa
Kuna rafu imechezwa?
Mbona online chanel inayoonyesha ni ya wasafi tuu?
Millard na clouds online hawaonyeshi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom