Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,125
- 8,644
Kwanza kabisa nimetafakari upinzani mkubwa nitakao kumbana nao katika hii post lakini siku zote mwanaume hueleza fikra zake na liwalo na liwe.
UTANGULIZI
Mie ni mwana CCM ila ninayemuunga mkono, muumini na mfuasi sugu wa Mh. Lowassa iwe usiku na mchana bado naamini alistahili kuwa na raisi japo yuko UPINZANI
KWA NINI NAMUUGA MKONO MAKONDA
Kwanza kabisa Mh Makonda baada ya kupewa ukuu wa wilaya na Jakaya mimi niliamini na hadi leo naamini ilikuwa ni moja ya zawadi ya fitina kwa kumshambulia Lowassa na tume ya jaji Warioba na hivyo kumfurahisha raisi mstaafu Jakaya na alipoingia Magufuli bado na yeye aliendeleza shukrani kwa kumpa ukuu wa mkoa lakini kwa uchapa kazi na ubunifu alioufanya katika wilaya ya Kinondoni ikiwemo usafi, kuwapunguzia kero walimu ya usafiri lakini pia uimara wa Makonda kutokuwa na woga kwa wakubwa wanaoharibu kazi na taswira halisi ya uongozi.
Nimetafakari chuki kubwa iliyopo juu ya Mh. Makonda na sababu zake hakika nimekosa kabisa na leo nimeamua kujitosa kumtetea.
Makonda nyota yake imekuwa kwa kasi Sana kiasi kwamba hata viongozi wengine/wateule wa raisi wanapwaya kumfikia na hivyo kujenga chuki kubwa na huku upinzani ukiungana mkono kumponda hata mazuri mengi anayoyafanya ukilinganisha mabaya machache anayoyafanya.
Sakata la madawa ya kulevya ndilo kabisa limemjengea uadui mkubwa huku likimjengea wafuasi wengi ndani na nje ya nchi nikiwemo mimi Ng'wanapagi na hili likanifanya nimsamehe yote aliyoniudhi kipindi cha katiba ya Warioba na wakati wa kumpata mgombea uraisi wa CCM kwani hakuna kiongozi yeyote narudia HAKUNA kiongozi yeyote aliyewahi kudhubutu kufungua mdomo wake kuwataja wahusika,watumiaji na watuhumiwa wa madawa ya kulevya akiwemo raisi wetu mstaafu Jakaya ambaye aliishia kusema tu..... Ninayo majina ya wauza dawa za kulevya huku akikenua meno yake kwa dharau.
Mapungufu ya Makonda; Naamini pamoja na uwezo mkubwa wa maarifa ya uongozi (ubunifu), Mh. Makonda sifa zinamfanya hadi ajisahau mipaka yake ya kazi yake mfano hili la kwenda Cloud TV usiku hakika ni ulevi wa madaraka hata mimi siwezi kulifanya pamoja na O level yangu isiyo na credit
Raisi anatakiwa sasa amuonye atambue mipaka yake lakini ASIFANYE KOSA kumfukuza kazi kwani mahasimu wake aliowatengeneza mwenyewe kwa nia njema ya kulikomboa Taifa lake hususani wauza unga na viongozi wezake aliowafunika kiutendaji, watacheeeeeeeka na kutangaza ushindi katika vita vya madawa na naamini, HAKUNA BINADAMU ALIYEKAMILIKA.
Makonda hakika umedhubutu na kwa hili la madawa naweka upinzani wangu pembeni na kukuunga mkono pamoja na mapungufu yanayowezwa kusahihishwa uliyonayo.