Makonda: Ndoa zote ndani ya mkoa wa Dar es Salaam kusajiliwa

Nimejaribu kutafakari analenga ku - achieve mini, nimeshindwa kabisa kupata logic yake.....

Watu siku zote wako on move. Watu wanahama na kuhamia mamia ndani ya jiji la DSM kwa mamia kama siyo maelfu kila siku.....

Na ndoa ziko za aina nyingi. Kuna ndoa rasmi (ambazo obvious zina usajili tayari kupitia mamlaka zilizopo kisheria)...

Zipo pia ndoa zisizo rasmi za watu kukubaliana kuishi na kuzaa watoto hivihivi, sasa sijui hawa watawekwa kundi gani.....

Hii ishu (kama ni muhimu na ina maana nyingine yoyote ya kimantiki kwa mujibu wa Bashite), inapaswa kuwa ya nchi nzima na siyo DSM ndiyo inaweza kuwa na maana, siyo hivi....!!
 
Sina nia ya kuchonganisha bali nina nia ya kuweza kujenga hoja ya kutaka ofisi zetu ambazo serikali ilizenga kwa gharama kubwa zinaheshimiwa hata akiteuliwa au akichaguliwa kichaa na kupewa mamlaka kubwa hapo kweny hizo ofisi.

Niseme wazi sijapendezwa na kitendo cha mkuu wa mkoa wa Dsm kutaka watanzania tuache kutafakali madhara ya ajari ya moto,tuache kujadili mkutano mkubwa wa SADC tujiandae kujadili machozi ya akina WEMA SEPETU wanao kwenda kwake kumlilia kisa wanamegwa na kuachwa.

Narudia tena kusema sijafurahi mtu kutoka ofisi kubwa kama ofisi ya mkuu wa mkoa tena jiji kujitokeza hadharani kutuandaa wananchi tujiandae kujadili machozi ya wanawake wa mkoa wa Dsm ambao wanamegwa na kuachwa.

Swali la msingi kwa nini hao wanawake hawaendi kwenye jengo jeupe kupeleka taarifa za kishenzi kama hizi badala yake wanaenda kwenye jengo la makamba?

Je ngazi mkoa,wakuuu wa mikoa hawana washauri?kwa nn huyu kijana amekuwa akijitutumua hivi? Hiv ni nani ambae hajui kuwa Mh mkuu wa mkoa miaka mitano baada ya kufunga ndoa ndo alinahatika kupata mtoto?

Je jasingekuwa na mtt mpka sasa si angeitisha agenda ya kuwasikiliza wakina baba wasio na watoto tatzo ambalo lazma mwishowe wangeishia kulaumu wakina mama ambao wababa Dsm uwatafuna ila hawazai?

Ombi langu kwa wanasiasa,hata kama tumekuchagua watanzania wote,hata kama umeteuliwa na nani katika nchi kama mnashimdwa majukumu muhimu mnayopewa basi ingieni kweny hzo ofisi na mkae kimnya kuliko kutoa matamko yatakayo fanya ofisi hizo zizalauliwe ili zina historia nzuri na iliyotukuka.

Mungu libariki jumba jeupe la magogoni kila aingiane hatunze heshima ya jengo ill kupitia mdomo n matendo.
 
Mkiambiwa bashite ni darasa ka saba B mnakataa haya sasa mmeona wenyewe.
68347730_463768134478090_1761429636425711616_n.jpg
 
Kazi yako ni kuinua maisha ya wana Dar es salaam, buni mipango endelevu hasa kwa vijana na akina mama. Hili la ndoa zetu wewe halikuhusu; kwa sababu tulipokuwa tunakubaliana wewe haukushiriki makubaliano.

Hiyo ni kazi ya Ustawi wa jamii na dawati la njisia - usiingilie kazi za wenyewe
 
Nikumbusheni yule mwanasiasa alisema kuna viongozi wanatumia makalio kufikiria,ni nani tena?,nimewaza sana hii ya Makonda nadhani inafanana na ule usemi wa kufikiria kwa makalio
 
Dogo wa Dar anaifanya kazi ya kubadili majadiliano ya kijamii kwa umahiri mkubwa sana (trend setting).

Ile habari ya Msamvu ni doa jeusi kwa mamlaka kuu, hivyo haraka haraka dogo amekuja na suala la ndoa za watu. Makali ya Morogoro yamepunguzwa tayari.

Kisiasa ni lazima uwe na watu wa aina hii kwenye uongozi wako, na ili umuhimu wao kisiasa uweze kuwa na mashiko wanakabidhiwa mikoa yenye ushawishi mkubwa kama huu wa DAR.


Siasa ni mchezo ambao unaitwa mchafu, lakini ndani ya huo uchafu ni lazima wawepo watu wenye kuweza kuufanya ukaonekana angalafu una usafi wa aina fulani.
 
Dogo wa Dar anaifanya kazi ya kubadili majadiliano ya kijamii kwa umahiri mkubwa sana (trend setting).

Ile habari ya Msamvu ni doa jeusi kwa mamlaka kuu, hivyo haraka haraka dogo amekuja na suala la ndoa za watu. Makali ya Morogoro yamepunguzwa tayari.

Kisiasa ni lazima uwe na watu wa aina hii kwenye uongozi wako, na ili umuhimu wao kisiasa uweze kuwa na mashiko wanakabidhiwa mikoa yenye ushawishi mkubwa kama huu wa DAR.


Siasa ni mchezo ambao unaitwa mchafu, lakini ndani ya huo uchafu ni lazima wawepo watu wenye kuweza kuufanya ukaonekana angalafu una usafi wa aina fulani.
Umejitahidi kuchambua
 
Hakuna jambo lilialonzishwa na Makonda likafanikiwa na hii inatokana ufinyu wa fikra alionao.
Back to the topic. wanaume waliooa watapigwa muhuri usoni?
Teh tutakuwa tunatembea na Passport au Vitambulisho vya Taifa

Wanaangalia jina then wanaingia kwenye Database yao

Aisee Tanzania kuna maajabu mengi sana
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom