Makonda na Musiba, Magufuli hayupo. Je, mmejiandaa kisaikolojia?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,720
Kifo cha rais John Pombe Maguli ni pigo kubwa kwa taifa na Afrika kwa ujumla. Ni rais ambaye amejijengea sifa, maadui hata marafiki. Tanzania, bila unafiki wala kificho itamkumbuka baada ya mwanzilishi wake Mwl Julius Nyerere.

Alikuwa mkweli na muwazi ingawa maradhi yake yalizungukwa na kificho bila sababu ya msingi kana kwamba hakuwa binadamu wa kawaida. Hata hivyo, wakati tukiomboleza, kuna watu saa hizi hawamuombolezi kwa vile wanampenda bali maisha yao yatakuwa hatarini tokana na kujipendekeza kwao wakidhani wangefanikiwa kumtumia.

Ndoto ya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi pia imo mashakani. Si vizuri kuongelea urithi wakati hata marehemu hajazikwa. Hata hivyo, urais si mali binafsi, lazima tuanze kufikiri mbele.

Wakati tukifanya hivyo, kuna watu watajuta kuzaliwa na wengine hasa mafisadi waliofichwa mahabusu wanasherehekea na wale waliosaidiwa wanasaga meno. Kati ya hao Daudi Bashite aka Makonda na Msiba Musiba watakuwa na hali ngumu.

Haya ni mawazo yangu kama baba yenu.

RIP JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI. YOU INDEED WERE OPEN AND TRUSTWORTHY FOR YOUR NATION AND PEOPLE.
 
Mi nashauri Mh. Samia amtafute makamu wake ambaye ni mchumi mmbobezi ambaye amtamsaidia kuurudisha uchumi kwenye mstari, lakini mtu mwenye ufahamu wa diplomasia vizuri itamsaidia pia kuurudisha mahusiano na nchi marafiki na mwisho mtu walau mwenye uzoefu wa shughuli za serikali.

Possible candidates include former CAG, former Katibu mkuu kiiongozi Sefue,

Proffesor Mkenda, Mizengo Linda.

Mheshimiwa aepuke kutea makada ambao wanaweka chama mbele na sio taifa
 
Back
Top Bottom