Makonda, Mpina ni chambo tu, sukuma gang inakuja taratibu

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,503
2,980
Tarehe 7 mwezi Aprili 2022, kwa mara nyingine tena Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina LM kupitia Chaneli ya Mtandao wa YouTube ya Dar24 alijitokeza hadharani kuishambulia Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Rais, Samia Suluhu Hassan (SSH) kwa kivuli cha kumshambulia Waziri wa Nishati January Makamba (JM) kwa kile alichokieleza kuwa JM ni mhujumu uchumi ambaye amekuwa akienda kinyume na maagizo ya Rais Samia. Je hii ni bahati mbaya? Unadhani LM amekurupuka?

Kabla hatujasonga mbele sana nikumbushe tu kuwa LM aliwahi kuhudumu kama Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wakati huo Waziri akiwa ni JM na Makamu wa Rais akiwa ni SSH na mambo hayakwenda sawasawa baina yao sababu LM alihisi kuwa hapewi nafasi ya kusikilizwa sana na SSH na hii ni kutokana na mchango wako kuwa mdogo katika mambo ya Muungano na Mazingira.

Lakini kwa kuwa LM alikuwa anatoka ukanda mmoja na Hayati JPM yeye alikuwa akienda kushtaki kwa "Baba" na alihakikishiwa kuwa kila kitu kitakuwa sawa na hatimaye akapewa Uwaziri wa Mifugo na Uvuvi na JM akavuliwa Uwaziri jambo lililopelekea dharau kushamiri kati yake na JM lakini pia kati yake na SSH akiamini kuwa hana nguvu yoyote bali mwenye nguvu ni JPM pekee.

Muda ukasonga tukapata msiba na leo hii tuko hapa LM ni Mbunge wa kawaida tu, JM ni Waziri wa Nishati, SSH ndiye Rais na Amiri Jeshi Mkuu, na ile iliyokuwa ikiitwa SG karibu yote haina Mamlaka ya kutisha tena.

Sasa SG wameona jiko lina majivu kwa juu hivyo wanatikisa ili kujua chini kuna moto kiasi gani, ili wajue kama utawachoma au wanaweza kuuzima. SG bado wana ndoto za kumuweka Rais wako katika uchaguzi ujao wa 2025, bado hawajaamini kuwa wamepoteza nguvu kabisa na mipango yao ya kidikteta imezimika kama mshumaa uliomwagiwa maji, bado wanachokonoa waone nguvu ya Rais.

KWANINI INASEMWA MPINA AMEMSHAMBULIA RAIS NA SIO WAZIRI
Mpina anagusia agizo la kuondolewa kwa tozo ya Shilingi 100 akisema Waziri alimdanganya Mheshimiwa Rais. Ukirudi katika taarifa toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu iliyosainiwa Jafar Haniu ya tarehe 05 Oktoba 2021 ilieleza kuwa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameelekeza kupunguzwa kwa tozo kwenye mafuta zenye thamani ya Shilingi Bilioni 102 kwa mwaka. Rais aliagiza ufanyike haraka mchakato wa kupeleka marekebisho ya Sheria bungeni endapo zipo sheria zinazohitaji mabadiliko ili kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta (BOFYA HAPA KUSOMA BARUA HIZO).

KAMA MHESHIMIWA RAIS NDIYE ALITOA AGIZO NA LEO HII MPINA ANATOKA HADHARANI KUMKOSOA WAZIRI KWA MAAGIZO ALIYOTOA RAIS NI WAZI KUWA WAZIRI HAPO NI KIVULI TU, ANAYESHAMBULIWA NI RAIS NA MPINA AMETANGULIZWA TU KAMA CHAMBO ILI KUONA RAIS ATACHUKUA HATUA GANI

Baada ya kelele za Mpina Jana (11 April 2022) ameibuka aliyekuwa RC wa Dar es Salaam Paul C. Makonda akieleza kuwa kuna wanaotaka kumtoa uhai kwa mambo aliyoyafanya akiwa madarakani.

Sote tunafahamu aliyoyafanya Makonda, hakuna haja ya kuyarudia, sote tunafahamu furaha alizoleta kwa wananchi lakini tunafahamu machungu machozi na maumivu aliyosababishia Watanzania na pia tunafahamu yeye pia (Makonda) ni mhanga wa SG, hivyo baada ya karata ya kwanza ya Mpina kutoka sasa wamekuja na karata ya pili ambayo ni Makonda. Bado wanapima kuona Rais na Serikali vitachukua hatua gani.

Na hii ni mbinu ya kuirudisha nyuma Serikali kuwachukulia hatua za kisheria wanaostahili, mimi ninamini Rais Samia ni Imara na atasimama kidete kwa maslahi ya nchi, hatoyumbishwa na SG au yeyote na kama kuna anayepaswa kuelekea Segerea kwa makosa aliyoyafanya huko nyuma basi sheria ifuate mkondo wake. SG watulie dawa iwaingie, ule wakati wa kuongoza nchi kwa mkono wa chuma umekwisha, kulialia na kutafuta huruma ya wananchi hakutowarejesha madarakani au kuwapeusha na mkono wa sheria, kwa Serikali hii ya Mama hakuna jiwe litabaki juu ya jiwe lingine, wote tutarudi kwenye mstari

Sg.jpg

1.jpeg

2.jpeg
 
Tarehe 7 mwezi Aprili 2022, kwa mara nyingine tena Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina LM kupitia Chaneli ya Mtandao wa YouTube ya Dar24 alijitokeza hadharani kuishambulia Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Rais, Samia Suluhu Hassan (SSH) kwa kivuli cha kumshambulia Waziri wa Nishati January Makamba (JM) kwa kile alichokieleza kuwa JM ni mhujumu uchumi ambaye amekuwa akienda kinyume na maagizo ya Rais Samia. Je hii ni bahati mbaya? Unadhani LM amekurupuka?

Kabla hatujasonga mbele sana nikumbushe tu kuwa LM aliwahi kuhudumu kama Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wakati huo Waziri akiwa ni JM na Makamu wa Rais akiwa ni SSH na mambo hayakwenda sawasawa baina yao sababu LM alihisi kuwa hapewi nafasi ya kusikilizwa sana na SSH na hii ni kutokana na mchango wako kuwa mdogo katika mambo ya Muungano na Mazingira. Lakini kwa kuwa LM alikuwa anatoka ukanda mmoja na Hayati JPM yeye alikuwa akienda kushtaki kwa "Baba" na alihakikishiwa kuwa kila kitu kitakuwa sawa na hatimaye akapewa Uwaziri wa Mifugo na Uvuvi na JM akavuliwa Uwaziri jambo lililopelekea dharau kushamiri kati yake na JM lakini pia kati yake na SSH akiamini kuwa hana nguvu yoyote bali mwenye nguvu ni JPM pekee. Muda ukasonga tukapata msiba na leo hii tuko hapa LM ni Mbunge wa kawaida tu, JM ni Waziri wa Nishati, SSH ndiye Rais na Amiri Jeshi Mkuu, na ile iliyokuwa ikiitwa Sukuma Gang karibu yote haina Mamlaka ya kutisha tena.

Sasa Sukuma Ganga wameona jiko lina majivu kwa juu hivyo wanatikisa ili kujua chini kuna moto kiasi gani, ili wajue kama utawachoma au wanaweza kuuzima. Sukuma Gang bado wana ndoto za kumuweka Rais wako katika uchaguzi ujao wa 2025, bado hawajaamini kuwa wamepoteza nguvu kabisa na mipango yao ya kidikteta imezimika kama mshumaa uliomwagiwa maji, bado wanachokonoa waone nguvu ya Rais.

KWANINI INASEMWA MPINA AMEMSHAMBULIA RAIS NA SIO WAZIRI
Mpina anagusia agizo la kuondolewa kwa tozo ya Shilingi 100 akisema Waziri alimdanganya Mheshimiwa Rais. Ukirudi katika taarifa toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu iliyosainiwa Jafar Haniu ya tarehe 05 Oktoba 2021 ilieleza kuwa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameelekeza kupunguzwa kwa tozo kwenye mafuta zenye thamani ya Shilingi Bilioni 102 kwa mwaka. Rais aliagiza ufanyike haraka mchakato wa kupeleka marekebisho ya Sheria bungeni endapo zipo sheria zinazohitaji mabadiliko ili kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta (BOFYA HAPA KUSOMA BARUA HIZO).

KAMA MHESHIMIWA RAIS NDIYE ALITOA AGIZO NA LEO HII MPINA ANATOKA HADHARANI KUMKOSOA WAZIRI KWA MAAGIZO ALIYOTOA RAIS NI WAZI KUWA WAZIRI HAPO NI KIVULI TU, ANAYESHAMBULIWA NI RAIS NA MPINA AMETANGULIZWA TU KAMA CHAMBO ILI KUONA RAIS ATACHUKUA HATUA GANI

Baada ya kelele za Mpina Jana (11 April 2022) ameibuka aliyekuwa RC wa Dar es Salaam Paul C. Makonda akieleza kuwa kuna wanaotaka kumtoa uhai kwa mambo aliyoyafanya akiwa madarakani.
Sote tunafahamu aliyoyafanya Makonda, hakuna haja ya kuyarudia, sote tunafahamu furaha alizoleta kwa wananchi lakini tunafahamu machungu machozi na maumivu aliyosababishia Watanzania na pia tunafahamu yeye pia (Makonda) ni mhanga wa Sukuma Gang, hivyo baada ya karata ya kwanza ya Mpina kutoka sasa wamekuja na karata ya pili ambayo ni Makonda. Bado wanapima kuona Rais na Serikali vitachukua hatua gani. Na hii ni mbinu ya kuirudisha nyuma Serikali kuwachukulia hatua za kisheria wanaostahili, mimi ninamini Rais Samia ni Imara na atasimama kidete kwa maslahi ya nchi, hatoyumbishwa na Sukuma Gang au yeyote na kama kuna anayepaswa kuelekea Segerea kwa makosa aliyoyafanya huko nyuma basi sheria ifuate mkondo wake. Sukuma Gang watulie dawa iwaingie, ule wakati wa kuongoza nchi kwa mkono wa chuma umekwisha, kulialia na kutafuta huruma ya wananchi hakutowarejesha madarakani au kuwapeusha na mkono wa sheria, kwa Serikali hii ya Mama hakuna jiwe litabaki juu ya jiwe lingine, wote tutarudi kwenye mstari

View attachment 2184762

View attachment 2184763

View attachment 2184764
Naona umetumwa kuja kuchonganisha..tambueni kanda ya ziwa ndio wenye kura ya turufu..mtakuja mnalialia tu kuwaomba wawaunge mkono..kuweni makini sana na hizi siasa ya utengano mnazozianzisha.

Endelea kupumzika kwa amani JPM rais uliyekua na maono makubwa kwa nchi hii.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kura ya turufu kufanya nini, kila mmoja ana kura sawa nchi hii na wala hazitahesabiwa wala kupigwa kwa Ukanda na ndio maana tunapinga ukanda
 
Kura turufu ya nyoko. Huu ndiyo ujinga mnaotumia kujitambua kama wasukuma huku Geita vijijini Mpina alituchomea nyavu zetu si wavuvi kama mtoto aliyelelewa ziwani hawezi kufanya hivi Mpina aliua uchumi wa ziwa Victoria Na kuleta umaskini kaya za usukumani kwa asilimia 90.
 
Kura ya turufu kufanya nini, kila mmoja ana kura sawa nchi hii na wala hazitahesabiwa wala kupigwa kwa Ukanda na ndio maana tunapinga ukanda
Naona unatangaza amani huku umeficha mapanga..nani asiyejua nguvu ya kanda ya ziwa katika chaguzi za nchi hii..yawezekana wewe ni mtoto wa juzi huwezi elewa.

All in all acheni hizo siasa maji taka za utengeno zitawaghalimu sana...absurd.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kura turufu ya nyoko. Huu ndiyo ujinga mnaotumia kujitambua kama wasukuma huku Geita vijijini Mpina alituchomea nyavu zetu si wavuvi kama mtoto aliyelelewa ziwani hawezi kufanya hivi Mpina aliua uchumi wa ziwa Victoria Na kuleta umaskini kaya za usukumani kwa asilimia 90.
Umepaniki wewe..ila ni kutaarifu tu siasa za utengeno mnazozifanya hazitawasaidia kitu..zitawangamiza mana kundi mnalolishambulia nikubwa sana na linaelewa nini kinachoendelea...swindlers wakubwa ninyi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wasukuma jihadharini sana na kilindi hicho Cha warundi Cha SUKUMA GANG kwani so watu waziri ona wanavyopamdikiza ukabila na inajulikana wametapakaa Tabora ,Kigoma,Geita,Shinyanga, Mwanza na msipijiangalia Ile chuki ya Watz kwa mateso waliyopata awamu ya Tano msije rithishwa. Kwa kuwadanganya kuwa hatima ya nchi hii imo kwenye kurà zenu.
 
Hilo jina silipendi sana..kwanini msitumia magufuli gang..kuliko kuliingiza kabila zima kwenye huo upumbafu..lengo lenu nini hasa.?

#MaendeleoHayanaChama
 
Naona unatangaza amani huku umeficha mapanga..nani asiyejua nguvu ya kanda ya ziwa katika chaguzi za nchi hii..yawezekana wewe ni mtoto wa juzi huwezi elewa.

All in all acheni hizo siasa maji taka za utengeno zitawaghalimu sana...absurd.

#MaendeleoHayanaChama
Wewe nawe una ujinga mwingi wa mambo ya UKABILA....kila siku unaongelea ukabila ukabila ukabila....una matatizo gani wewe jamaa?!!!😲😲😲

Taifa hili ni bora zaidi ya huo ujinga unaouhubiri kila siku.......

Nimewaita Mods waufute huu uzi kwa kuwa hauna faida kwetu WANANCHI tusio katika MIRENGO yenu ya CHUKI ZA KIBAGUZI.....

PATHETIC
 
Back
Top Bottom