Makonda: Meya wa jiji ni bora akawa na shughuli nyingine maana kazi yake sio kazi ya utawala!

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,959
Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda ameelezea mipaka yake ya kazi kati yake na meya wa jiji kwa kuwa watu wengi huwa wanachanganya.

Amesema meya wa jiji ni amechaguliwa na madiwani kuwa mwenyekiti wao, kama ilivyo kwa spika wa bunge alivyochaguliwa na wabunge kuwa mwenyekiti wao na kazi yao ni kuwa mwenyekiti wa kikao.

Ameongezea kuwa kiutaratibu meya anaingia manispaa mara mbili kwa wiki na inapendekezwa akatafuta shughuli nyingine maana kazi yake sio kazi ya utawala.



 
Na yeye huko kwenye halmshauri anafuata nini? Sisi tunajua mkubwa wa halmashauri ni DED, wala siyo mkuu wa mkoa au wilaya. Wakae nao kwenye ofisi zao watuachie halmashauri zetu.

Hawa jamaa kwa ufupi hawana kazi za kufanya kule ofisini kwao ndo maana wamebaki kudandia kazi za halmashauri. Hii ndo huwa shida yangu kubwa na vijana kuaminiwa kwenye nafasi kubwa kubwa kama hizi. Busara ni "zero" (kwa lafudhi ya Magu).

Hizi nafasi wapewe watu wazima ambao wana busara!!
 
Imekuaje haya yanasemwa leo baada ya Meya kutoka upinzani kukalia kiti?

Ni wazi kuwa hicho kitu kinawanyima raha sana,ila ni vyema kuheshimu wana Dar walivyoamua kupiga chini watangulizi.

Hivi inakuaje MTEULE anakuwa na kelele kiasi hiki katika mkoa kuliko viongozi wa kuchaguliwa na wananchi wao kama MEYA?, punguza kidogo.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom