Makonda, kwanini kila ukimtaja Rais Magufuli lazima ukosee na kumtaja Kikwete?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,791
71,195
Namsikiliza Makonda hapa Clouds alipokwenda kujikosha kuhusu shisha na rushwa ya Polisi akikosea tena badala ya Rais Magufuli na kuanza kutaja Rais Kikwete.

Hii sii Mara ya kwanza, hilo kosa analifanya sana na Magufuli ana zaidi ya mwaka ndani ya cheo hicho.

Wataalamu wa saikolojia wanaamini kuwa yule aliyejaa kichwani mwako ndiye mwepesi kumtamka mdomoni.

Jee Makonda akili yake bado imejaa kwa Rais Kikwete kuliko Magufuli au hilo linatokea kwa vile anaripoti mambo kwa Kikwete kinyemela?

JPM Ajichunge kwani wapo wateule wake ambao akili zao hazipo kwake Bali kwa mtangulizi wake.
 
Naona kaenda "kusafisha hali ya hewa" aliyochafua.

Wenzake wanaenda moja kwa moja ofisini,yeye anaamshana asubuhi na Pj,Masoud Kipanya.

Naona anaibia muda wa kutumikia umma.

Sijawahi ona magufuli,au majaliwa anaamkia tbc.
 
Namsikiliza Makonda hapa Clouds alipokwenda kujikosha kuhusu shisha na rushwa ya Polisi akikosea tena badala ya Rais Magufuli na kuanza kutaja Rais Kikwete.
Hii sii Mara ya kwanza, hilo kosa analifanya sana na Magufuli ana zaidi ya mwaka ndani ya cheo hicho.
Wataalamu wa saikolojia wanaamini kuwa yule aliyejaa kichwani mwako ndiye mwepesi kumtamka mdomoni.
Jee Makonda akili yake bado imejaa kwa Rais Kikwete kuliko Magufuli au hilo linatokea kwa vile anaripoti mambo kwa Kikwete kinyemela?
JPM Ajichunge kwani wapo wateule wake ambao akili zao hazipo kwake Bali kwa mtangulizi wake.

Kikwete atakumbukwa sana, ni vigumu kumsahau Kikwete haraka haraka.

Hilo si kwa Makonda tu, wengi wanamkumbuka sana tu, mpaka tumewasikia upinzani wakimkumbuka wazi wazi mara kadhaa na kwa makusudi kabisa si kwa kukosea kama Makonda.

Ukweli ubaki kuwa ukweli.
 
Kikwete kakaa mioyoni na akilini kwa miaka kumi

Magufuli ana mwaka tu

its natural kukosea kutaja kikwete badala ya magufuli

unless wewe sio binadamu
 
Namsikiliza Makonda anavyojiuma kuhsu umbea aliomhusisha nao Sirro......jamaa Mkoa mgumu kwake.
 
Yani Huyu Jamaa Jinsi Anavyobwabwaja Lawama Nyingi Anazishusha Kwa Kamanda Sirro yani Huyu Jamaa mmhh Hizi Siasa Hizi.
 
This is stupidity of highest order

kikwete kakaa mioyoni na akilini kwa miaka kumi

magufuli ana mwaka tu

its natural kukosea kutaja kikwete badala ya magufuli

unless wewe sio binadamu
Basi akili yako ina walakini, hata ukae na mtu miaka 20 tena hukuwa mtendaji wa karibu, halafu unakaa mwaka mzima na mtu ambaye utendaji wako wa day to day uko naye kisha unakosea jina lake?
 
Back
Top Bottom