Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Katika harakati za kupambana na rushwa katika mkoa wa Dar es Salaam Makonda amekuja na mkakati mpya.
Mkuu wa Mkoaa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda ametangaza ofa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam muda na wakati wowote kujitokeza katika ofisi yake kuchukua kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kulipia endapo Mwananchi ameombwa rushwa na watumishi wa Serikali.
RC Makonda amebainisha kuwa kutokana na suala la watumishi hasa wa kada ya Afya kuwadai wananchi rushwa pamoja na maafisa wengine katika jiji la Dar es Salaam, amekuja na Mkakati huo wa kutoa fedha kwa kiasi chochote kile ambacho Mwananchi atakiitaji endapo ataombwa rushwa na mtumishi wa Serikali ndani ya Mkoa wake.
Fedha za moto ni fedha alama maalumu ambazo hutumika kuwanasa wala rushwa, kwani hutumika kama kidhibiti pindi mshukiwa akikamatwa nazo.
Wanaume wa Darisalama changamkieni hela hizo mkanunue viwanja Chamazi huko
Source: Ukitaka pesa za ‘Moto’ ukiombwa rushwa na mtumishi wa Serikali, Makonda anatoa pesa hizo - DEWJIBLOG