Mnyanyembe wa Mboka
JF-Expert Member
- Feb 10, 2017
- 2,348
- 3,036
Leo nimeamini ukitaka kujua tabia ya mtu mpe mamlaka, Mh Mkuu wa Mkoa DSM amejikuta anatumbukia kwenye wimbi la shutuma za kejeli na dharau huku akibezwa kwa vitendo vyake vya kibabe na majigambo yenye jeuri na vijembe dhidi ya walio mtangulia kiumri na kimadaraka mbele ya wananchi anaowaongoza.
Kwa ufahamu wangu mdogo sikumbuki kama kuna RC wa DSM alie wahi kutumbukizwa kwenye zengwe kama hili linaloendelea kwa makonda tangu enzi za kina Songambele hata mpaka wakati wa Kina Chipungahelo "Mama Chips" na hatimae kina Makamba mpaka Sadiki na wengineo waliopita huko nyuma.
Leo hii tumeshuhudia mkuu wa mkoa akikaidi wito wa Mahakama Kuu na kuitikia wito wa Radio ili kwenda kujibu shutuma zinazomkabili hii ni dharau ilioje kwa muhimili wa serikali? kweli jamani tumefika huko sasa.
Makonda anatuonyesha mfano gani wananchi wake? au ndio makuzi?
Niliwahi kusikia msemo mmoja kua "Masikini Akipata Matako hulia Mbwata". Nilisoma gazeti moja lilielezea wasifu wa Makonda na Maisha aliyopitia, kwa busara zangu fupi nilipojaribu kuunganisha wasifu wake na matendo anayoyafanya ni kama vinaendana
1. Anapenda sana kuonyesha status ya maisha aliyonayo kwa sasa kupitia mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kuonyesha staili za mavazi aliyovaa katika mitindo mbalimbali, maeneo anayokwenda kwa nyakati tofauti, uwezo wa kujicjanganya katika makundi tofauti n.k
Kulingana na wasifu wake nagundua pengine huyu Mh. Makonda labda ni ulimbukeni kwa sababu katika maisha aliyopitia hakuwahi kutegemea kupata nafasi ya kufanya hayo anayoyafanya kwa sasa na kuishi maisha Mazuri kama aliyonayo sasa kwa umasikini aliokua nao.
2. Kila issue anayokurupuka nayo haikamiliki kwa sababu anaikuripukia bila ya mipango, tathmini wala mitazamo ya faida, hasara, athari na uwezo wa kulivamia au kulisemea jambo analo anzisha au kulikurupukia
kulingana na wasifu wa maisha yake shule imekua ya ubabaishaji mara elimu ya watu wazima, mara chuo cha uvuvi mbegani, mara chuo cha ushirika moshi, mara kagushi vyeti, hivyo shule yake haipo consistance kwa anachokisomea na kwa lengo la masomo yake na kujikuta atakachookota ndio hichohicho bora qualification tu isiyo na dira
3. Anapeda kuonyesha watu kua JPM kwake ni wa karibu sana pengine kuliko kiongozi mwingine yeyote na hata anaweza kuongea nae mbele yenu kwa simu na akaiweka loud na nyie mkasikia anaongea na mkuu wa nchi kwa muda alio utaka yeye, du! ha ha ha haaa hii kali sana
Labada kulingana na wasifu wake alikua na infiriority complex iliyo mnyima nafasi ya kuji expose kwa wanene na bigheads fulani, ndio maana leo tunashudia akilishwa keki na kina Mo, kwa kua amepata nafasi na sababu ya kua nao karibu, anahalalisha dhamana za kina GSM kwa mambo mbalimbali kama BAKWATA na kwingineko hali yankua chimbuko la GSM hakuna asie lijua nchi hii, na ndio maana uadilifu wake wa kumtaja na kumshirikisha sana Mungu na ufalme wake wa mbinguni unaonekana kama sanaa na maigizo kuwazuga wajinga walio wengi nchi hii
4. Anapenda kujiona kua anachokifanya ni cha uhakika na hakuna yeyote atakae weza kufikia utendaji wake na atakae jaribu kumnyoosha atamjibu chochote na hakuna wakumuhukumu
Hili pia linaoana kabisa na wasifu wa maisha yake aliyopitia, kwa sababu maranyingi katika maisha ukiwa mtu wa chini ni mara chache kupewa nafasi ya kusikilizwa na pengine hata watu kufuatilia hoja zako, hivyo pale unapo ipata nafasi unataka kutanua mbavu kuwadhihirishia kua walikupuuza bure wewe ndie kichwa kuliko wao
5. Amekua anatabia ya kupiga vijembe viongozi wenzie na hata kudharau vyombo vyenye mamlaka makubwa katika serikari na kujiona yeye ndie super star wanchi hii.
Kutokana na wasifu wake wa maisha ya kimasikini aliyopitia na ghaflankuibukia katika nafasi ya uongozi wenye mamlaka na kujikuta katika nafasi ya kua juu ya watu na mahitaji yao basi ni lazima atakua anajiona kama mungu mtu
6. Amekua anakurupuka kwa ku create attention juu ya vitu au issue zenye public interest ili tu kupata support ya ubunifu wake katika kudeal na vitu vilivyowashinda watu
Kutoka na wasifu wa maisha aliyopitia amekua yuko chini ya daraja la maisha hivyo watu hawakujua kua somwhere kuna mtu anaitwa Makonda na ndio maana badala yake kulingana na hadhi na uwezo alio nao kwa sasa inabidi atafute vitu vitakavyo mjengea attention na watu kujua kua kuna mtu anaitwa Makonda
7. Anapenda sana kuongea kibabe kwa kutumia neno "Tutamshughulikia" hii ikiwemo kutoa kauli za kuogofya au kutia hofu na kufoka pasipo takiwa hata kukemea.
Pengine kutokana na wasifu wake alisha pigwa sana na makoleo ya mchanga huko mashimoni kwa mdomo wake manake kule watu hawatakagi ujinga, sasa labada hapa anataka kulithibisha hilo kua yeye ni mbabe zaidi ya mnavyofikiri
Mheshimiwa shoo anazoonyesha Instagram haziendani na hadhi yake, akumbuke anatuongoza watu masikini sana ambao si vyema kutuonyesha na kututambia mbele yetu kua unajua kuvaa nguo nzuri za thamani sana unasafiri kwenda ng'ambo kupimzika katika maeneo ya ndoto zetu.
Mwisho ni kua sisi wananchi tunao kupenda tunakusihi uache dharau ... Mahakama imekuita umedharau leo hii umeitwa na Redio ghafla umeitikia wito na kutoa appointment ya muda, siku na wakati utakao hudhuria wito huo... Mwe!!!
Wako
Mnyamwela
Wa Mbokamanyema