Makonda kubadili jeshi la polisi kwenda kisasa katika kukabiliana na uhalifu

cocochanel

Platinum Member
Oct 6, 2007
26,731
73,355
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema jeshi la Polisi katika Mkoa huo linatakiwa kuwa la mfano wa kuigwa katika kukabiliana na kila wimbi la uhalifu, ili wananchi waishi kwa amani kutokana na umuhimu wa biashara.

Makonda ameyasema hayo leo (14/06/2017) wakati wa kupeleka magari 26 ya polisi kwenye ukarabati katika gereji iliyoko maeneo ya Utalii mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya matengenzo pamoja na ufungaji wa Kamera katika magari hayo alipokuwa anazungumza na jeshi la polisi leo Osterbay jijini Dar es Salaam.

Amesema katika kukabiliana na rushwa na jeshi hilo, watafunga kamera katika kila kituo ndani ya jiji la Dar es Salaam, ambapo OCD , kanda maalumu, pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi wataweza kuona kile ambacho kinafanyika.

Makonda amesema jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam linatakiwa kuwa la kisasa zaidi katika kukabiliana na uhalifu wa kila namna ikiwa ni pamoja na kuwa na vifaa vya kisasa.

Amesema katika maboresho hayo wataweka Kompyuta kila kituo ili kuachana na kuandika maelezo katika karatasi na mtu yeyote, baada ya kuwekwa kompyuta hizo asikubali kuandikiwa maelezo katika karatasi.

Aidha amesema kuna baiskeli ziko njiani ambazo zitagawiwa kwa polisi ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na uhalifu katika mazingira ambayo kifaa hicho kinaweza kupita.

Nae Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amesema Jeshi la Polisi kanda maalumu inakabiliwa na changamoto ya magari pamoja na mafuta na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi katika kukabiliana na wahalifu wa kila namna .

Amesema kuwa kutokana maboresho hayo yataweza kubadilisha hata takwimu zilizo katika kipindi hiki zisirudie kutokana na maboresho hayo.

PM 1.JPG

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na watendaji mkoa na polisi katika hafla ya upelekaji wa gari 26 ya jeshi la polisi katika matengenezo mkoani Kilimanjaro leo jijini Dar es Salaam.

pm 2.JPG

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya (wa pili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu magari yaliyoharibika kwa ajili ya kwenda katika matengenezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) na watatu kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Ally Hapi leo katika Kituo cha Polisi Osterbay jijini Dar es Salaam.


pm 3.JPG

Moja ya gari mbovu ya Polisi ikiwa tayari kwa kusafirishwa kwa ajili matengenezo mkoani Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Polisi cha Osterbay jijini Dar es Salaam.


pm 4.JPG

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na Wanajeshi wataopeleka magari kwa ajili ya matengenezo mkoani Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika leo katika kituo cha Osterbay jijini Dar es Salaam.

C&P
Chanzo michuziblog 14/06/2017


n.b. jamani nimewaletea habari nzuri sana hii haswa kwa wakazi wa Dar.
 
With all of his efforts but the Media ban (on Bashite) is still existing on..!

Hii habari haijatoka popote pale, itakuwa labda ni hapa na kwenye page ya Le Mpumbuuuzzz.

Duu kweli kukataliwa kubaya... Pole sana Bashite.
Star tv ndo media pekee inayosaliti azimio la kumfungia bashite hii habari ilipewa coverage kubwa saaaana na star tv hadi wameandaa documentary inayoruka Mara Kwa Mara
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom