Makonda kamwombe radhi Warioba , vinginevyo vijana tutakutenga

hakuna jambo hatari sana katika kuondoa hamani kama ulevi wa madaraka na uroho wa madaraka katika hali ya sasa hivi uvumilivu wa kisiasa imekwisha imebaki ni dalili ya amani kuondoka katika taifa hili wamezoea kuwapiga wastaaf mwanzo walimpiga rais mwinyi kofi leo wamempiga warioba hivi vitendo haviwezi kukubalika mbele ya macho ya haki na usawa katika taifa
 
Tangu lini ccm wakawajali wazee....! Si ni hawa hawa kila mara wanaiasa jamii isiwasikilize na kupotoshwa na wazee kwani hawana jipya bali wanasubiri kufa tu....!
 
Tabia yoyote mbaya haipaswi
kushangiliwa hata kidogo. Na kama yupo kijana wa kitanzania
anavifurahia vitendo na tabia za makonda nitapata shaka juu ya uelewa
wa kijana huyo.

Vijana wa kitanzania wamefunzwa kuwaheshimu watu walio wazidi umri na
kuwaona kama wazazi wao. kuwaheshimu wakubwa na wadogo.

Makonda kama kiongozi anawakilisha hali halisi ya tabia za vijana wa
kitanzania , kwa mantiki hiyo makonda amekuwa akitudhalilisha vijana
mara kwa mara, na mara ya kwanza ni pale alipotoa maneno ya kejeli kwa
mh. lowasa bila kujali kwamba lowasa ni kiongozi mkubwa tena ni mzazi
wake kwa umri . Leo tena kaja na hii mpya na bado wapo watu wanaomtumia
sms za kumpongeza na kumwita shujaa. Na kadiri siku zinavyokwenda na
ndivyo tabia yake inavyokomaa hivyo sitashangaa kuona huko mbele
akimkata mtama mwenyekiti wake au akimrushia kiatu katibu wake kwani
mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Makonda asipoomba radhi vijana tumtenge na tusimpe ushirikiano kwani
anatuchafulia taswira yetu kitaifa na kimataifa. Kulikuwa na sababu gani
ya yeye kama kamanda mhamasishaji wa uvccm kuhamasisha vijana kwenda
kuvuruga kongamano la watu , wakati chama kina ela za kufanya ziara nchi
nzima na kuhamasisha vijana kuipigia katiba kura ya ndiyo .

kwani jaji warioba alitengwa au alipigwa? mkiitwa mayai mnalalamika.
 
Tabia mbaya ni ile ya kumsingizia Makonda eti kamshambulia Mzee Waryoba, tabia hii ni ya uzushi , uzandiki na unafiki wa hali ya juu kabisa. Wote wanaoshadadia suala hili ukiwaomba ushahidi hawana hata chenbe, Waryoba mwebyewe kakanusha kushambuliwa na Makonda. "cheap popularity", za jinsi hii zinapatikana UKAWA na kwa wafuasi wa CDM pekee.
 
Usikute huyo konda ana miaka miwili hapo dar toka huko vichochoroni alikotolewa
 
Huyu jamaa amepangwa na ccm kumdhalilisha mzee wetu warioba we huoni mpaka leo chama tawala hakijasema kitu wala kutoa tamko jiulize ingekua chama pinzani ingekuaje
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom