Makonda, kabla ya kuunda tume ya watoto wa mitaani twambie matokeo na changamoto ya zoezi la lilopita

Tairi bovu

JF-Expert Member
Sep 28, 2017
3,063
2,983
Wanajamvi.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam haishiwi vijimambo. Huyu ni miongoni mwa wakuu wa mikoa wasiojua hata kazi zake.

Kabla ya kuanza kwa zoezi la kutafta baba waliotelekeza watoto hapo Aprili 6 mwaka huu, niliandika hapa kuwa haitoshi tu kubaini watoto waliotelekezwa na wazazi wao yatosha kubaini changamoto zilizopo kwenye sheria ile ya mtoto ya 2009 au ile ya ndoa ya mwaka 1971.

Wapo waliopinga na wapo wapo waliounga mkono hoja ile. ziliibuka changamoto nyingi mno kwenye zoezi lile lakini ukweli ukabaki tu kwamba zoezi lilibuma. ( mpaka leo hatujambiwa hatima ya case ya mtoto fake wa lowasa). Kabla hatujakaa sawa mkuu huyu wa mkoa anakuja na lingine. Anasema anaunda tume ya kushughulikia jambo lile lile la watoto wa mitaani ( inaongozwa na msando, huyu sio mwana taaluma hajui masuala haya, ni mwanasheria) .

Makonda ulitakiwa kuanza na tume lakini kuwashirisha wana wa taaluma ( ustawi wa jamii) commisioner ni mbobevu kwenye mambo haya. Haya ni ya kitaifa, sheria ni ya kitaifa sio ya mkoa ni kazi bure kama hujawashirikisha wenye taaluma yao pale Kijitonyama wao wanajua zaidi ya msando huyo ni kada.

nikwambie mambo ya ustawi ni mapana na mtambuka yenye kuhitaji utaalamu na ubobevu sio siasa. Tatizo moja ( suala ) moja huleta lingine na hayaanzii juu kwa mkuu wa mkoa tena mmoja yanaanzia kwa mtu ( individual) micro, familila / kikundo ( messo) na jamii ( macro) levels yashughulikie kufuata mpangilio huo vinginevyo ukimaliza moja litaibuka jipya mpaka utakapo zeeka huta maliza. ukiwatumia wataalamu watakisaidia.

Mwisho:
Makonda mtu yeyote wa hadhi yako anapaswa kufanya mambo kwa tathmini kujulisha mafanikio na changamoto.

Kabla hujaunda tume twambie mafanikio na changamoto za zoezi wale waliotelekezwa, mafanikio na way foward. Vinginevyo unachanganya na kurukia rukia mambo usiyoyajua ni uhuni.

UNAKUMBUKA ZOEZI LILE LA KUWAPATIA MIGUU BANDIA WENYE MAHITAJI? BILA KUWATUMIA WATAALAMU? SIO KWELI KWAMBA ILILETWA PALE MIGUU ISIYOFAA KWA MATUMIZI?

JE, NI WALEMAVU WANGAPI WANATUMIA MIGUU YAKO ILE YA HOVYO MPAKA LEO?
Kutafakari.
 
Hili bandiko ni la kitoto sana..Nina mashaka na umri wa mleta mada ni wa kumpuuza tu..
Huyu kaandika kulingana na taaruma yake. Huwezi sema ni bandiko la kitoto. Wewe leta lako la kikubwa tuone. Aliowabambikia kesi watoto wakaja kukana wewe unajifanya unazo?
 
Roboti ni mashine inayotekeleza shughuli peke yake bila kuendeshwa na
binadamu . Kuna tofauti kati ya nchi na nchi kuhusu kiwango na ugumu wa shughuli zinazotekelezwa ili mashine iweze kuitwa "roboti".

Asili ya jina roboti ni lugha ya Kicheki na maana yake ni "mfanyakazi ". Kwa Kicheki, kama lugha za Kislavoni nyingine, "robota" inamaanisha kazi.

Tangu karne nyingi kuna watu waliowaza uundaji wa viumbe ambavyo vitengenezwe na binadamu na kutekeleza kazi zake. Kuna hadithi za
Wayahudi wa Ulaya ya kati ambako uundaji wa kiumbe cha "Golem" unasimuliwa na kazi yake ilikuwa kumsaidia rabi wa mji wa Praha mwenye vipaji vya kutenda miujiza .

Katika karne ya 20 msanii Mcheki Karel Čapek alitumia neno "robot" katika
tamthilia aliyotunga mjini Praha kwa watu bandia waliotengenezwa kuwafanyia binadamu kazi.

My note

"Wengine wamewekwa tu na wanadamu kutekeleza yale ambayo hata wao hawayafahamu, hawa ndio kitaalam wanaitwa Robot "
 
Hili bandiko ni la kitoto sana..Nina mashaka na umri wa mleta mada ni wa kumpuuza tu..
Lina utoto gani kama wewe umeshindwa kuweka la kiutu uzima? Acheni kuketa hangover za disco kwenye mambo ya kitaaluma yanayoongozwa na sheria! Itoshe tu kumuunga mkono mleta hoja ya kuhitaji mrejesho na sio utumbili wa kurukia kila tunda!
 
Mkuu zero in paper zero in brain, mwambie Kwanza alete mrejesho suala la walimu wa dsm kupanda daladala bure ,
Hamna kitu hapo
 
Back
Top Bottom