Makonda, Gambo na wengine wa aina zao wakishindwa kuwa Wabunge wanapowania itakuwa aibu kubwa kwao na kituko cha karne!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,196
25,516
Kuna aina mbili za viongozi wa mikoa na wilaya wanaowania Ubunge. Wapo wale wanaowania kwenye majimbo ambayo hayako kwenye mikoa au wilaya walizokuwa wakizioongoza. Na wapo wale ambao wanagombea kwenye majimbo ambayo yapo kwenye mikoa na wilaya walizokuwa wakiongoza.

Nawazungumzia waliokuwa wakuu wa mikoa na wilaya. Paul Makonda na Mrisho Gambo ni kati ya wakuu wa mikoa na wilaya wa naowania Ubunge kwenye majimbo yaliyopo kwenye mikoa waliyokuwa wakiiongoza. Makonda anawania Kigamboni ya Dar es Salaam na Gambo anawania Arusha Mjini kule Arusha.

Kwa jinsi walivyokuwa wakijipambanua, kujitangaza na kuonekana kama wachapakazi na watatuzi wa changamoto za wananchi wao huku wakijisifu kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM, ni rahisi kuamini kuwa wana nguvu kubwa ya kuwaunga mkono ndani na nje ya chama chao cha Mapinduzi.

Leo, zoezi la kuchukua, kujaza na kurejesha fomu za kuwania Ubunge ndani ya CCM limekamilika. Sasa unasubiriwa mchakato wa ndani ya chama kuwapata wagombea wa Ubunge katika majimbo husika. Makonda, Gambo na wanaofanana nao kwa jinsi walivyojichora hawapaswi kushindwa.

Kushindwa kwenye majimbo yao, ndani ya chama au kwenye uchaguzi mkuu, itakuwa ni aibu na kituko cha karne. Itawezekanaje 'wachapakazi na watekeleza ilani' kama Makonda na Gambo kushindwa? Kama ni kweli walikuwa wakiwatumikia vyema wananchi, wanapaswa kutunzwa kichama na wananchi wao.

Karibu ukweli utajianika!
 
Nawazungumzia waliokuwa wakuu wa mikoa na wilaya. Paul Makonda na Mrisho Gambo ni kati ya wakuu wa mikoa na wilaya wa naowania Ubunge kwenye majimbo yaliyopo kwenye mikoa waliyokuwa wakiiongoza. Makonda anawania Kigamboni ya Dar es Salaam na Gambo anawania Arusha Mjini kule Arusha.

Kwa jinsi walivyokuwa wakijipambanua, kujitangaza na kuonekana kama wachapakazi na watatuzi wa changamoto za wananchi wao huku wakijisifu kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM, ni rahisi kuamini kuwa wana nguvu kubwa ya kuwaunga mkono ndani na nje ya chama chao cha Mapinduzi.
Ngoja nikuambie siri moja ya uchaguzi. CCM huamua ishinde wapi na ishindwe wapi, au mgombe yupi wa CCM ashinde au kushindwa. Ukiweka hilo akilini basi huna haja ya kuwazia yajayo juu ya Makonda na Gambo, Tulia, Kabudi, nk. Mengineyo ni maigizo tu.
 
Bashite katumiwa na Magu kufanya matukio mazito sana ya kikatili.

Kinachoendelea, yeye kamtuma apate ubunge halafu afanywe spika ili awe na kinga post-2025 ( sheria washapitisha )

So Tusichoshane :)

Mtu muongo miaka 5 mfululizo, halafu aje aaminike kwa kikauli kimoja tu
 
Dah... umeweza mbali sana mkuu... yaani hayo yameanza kukliki kichwani kwangu
 
Bashite katumiwa na Magu kufanya matukio mazito sana ya kikatili.

Kinachoendelea, yeye kamtuma apate ubunge halafu afanywe spika ili awe na kinga post-2025 ( sheria washapitisha )

So Tusichoshane :)

Mtu muongo miaka 5 mfululizo, halafu aje aaminike kwa kikauli kimoja tu
Ngoja tuone bwana graduate Kama utabiri wako utatimia
 
Bashite katumiwa na Magu kufanya matukio mazito sana ya kikatili.

Kinachoendelea, yeye kamtuma apate ubunge halafu afanywe spika ili awe na kinga post-2025 ( sheria washapitisha )

So Tusichoshane :)

Mtu muongo miaka 5 mfululizo, halafu aje aaminike kwa kikauli kimoja tu
Mkuu unaweza kututajia huyo mtu muongo?

Ukiminywa kende mi simo
 
Ngoja nikuambie siri moja ya uchaguzi. CCM huamua ishinde wapi na ishindwe wapi, au mgombe yupi wa CCM ashinde au kushindwa. Ukiweka hilo akilini basi huna haja ya kuwazia yajayo juu ya Makonda na Gambo, Tulia, Kabudi, nk. Mengineyo ni maigizo tu.
Kwamba CCM huamua ishindwe wapi!!!
Ndugu, hakuna kitu kama hicho.
 
Bashite atapitishwa. Usicheze na nguvu ya Chairman. Kama Gambo alitumbuliwa kweli (na sio kuondolewa baada ya kuomba na kupata baraka za mfalme..) huyu yupo shakani kupitishwa.

Kumbuka: kushinda kura za mchujo kwa wanachama kwenye jimbo husika sio ticket ya jina lako kuwa endorsed na vikao vya juu vya Chama
 
huwa najiuliza huwa anajisikiaje huyu bwana Bashite mbingunikwetu pale anaposhuhudia vile watu hawampendi!

Mkuu mbingunikwetu ingekuwa nimimi ninge-keep low profile niachane hata na siasa kabisa, maana sio fisiem, upinzani wala wasio na chama wanaokukubali! Ww kweli ni failure!
 
Umekuja kufanya nini hapa Duniani kama unaona kushindwa kwa mtu aliyejaribu ni aibu? Isitoshe aibu ni kwa yule aliyejaribu na kushindwa au wewe ambaye hakuna kitu umefanya maisha yako yote hapa Duniani zaidi ya kukaa kusubiri Binadamu xyz anayejaribu akishindwa umcheke? Wakishindwa maisha yataendelea ndiyo Uanaume huo, lkn angalau watakuwa wamejua limitations zao, kurekebisha kama wakiweza na kusonga mbele na maisha, kuna mengi zaidi ya kufanya, ...
 
Am sure 100% makonda atashinda kigamboni na atakuwa mbunge napia atakuwa waziri wa mambo ya ndani ,mark my words
 
Back
Top Bottom