Makonda awaponza Star Tv na Sahara Media mbele ya TEF | Page 19 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makonda awaponza Star Tv na Sahara Media mbele ya TEF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurzweil, May 19, 2017.

 1. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2017
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 5,252
  Likes Received: 5,237
  Trophy Points: 280
  UAMUZI WA STAR TV NI USALITI KWA TAALUMA YA HABARI
  Kwa muda wa wiki moja sasa kampuni ya Sahara Communications Limited, wamiliki wa Star TV na vyombo vingine vya habari kupitia mitandao ya kijamii wanasambaza taarifa kuwa watafanya mahojiano maalum na Mkuu wa Mkoa wa Dar ea Salaam, Paul Makonda, Jumatatu Mei 22, 2017.

  Kusudio hilo la Star TV limekuja wakati kiongozi huyo akiwa amefungiwa na vyombo vya habari kwa uamuzi ulioitikiwa kwa pamoja baina ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na kuungwa mkono na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) na taasisi nyingine za kihabari nchini. Uamuzi wa kumfungia Makonda uliotangazwa Machi 2017, ilitokana na kiongozi huyo kuvamia Kituo cha Utangazaji cha Clouds Madia, March 17, 2017 akiwa na askari wenye bunduki.

  Uvamizi wa Clouds ulikuwa mwendelezo wa matukio ya RC Makonda kudhalilisha wanahabari, kutukana na kutoiheshimu taaluma ya habari. Katika tamko hilo, Makonda tulimpa masharti mepesi kurejesha uhusiano na tasnia ya habari, ambayo ni kuomba radhi waandishi wa habari kwa tukio la Clouds na matukio mengine kwa ujumla wake kama sehemu ya uungwana wa Kitanzania.

  Tulisema katika tamko kwa yeyote atakayeshirikiana na Makonda naye tutamhesabu kama adui wa tasnia ya habari nchini. Kwa mantiki hiyo tunasema ikiwa Star TV wameamua kushirikiana na Makonda, basi ni wazi wameamua kwa hiyari yao wenye kujitangaza kama adui wa tasnia ya habari nchini.

  Kila Mtanzania anajua jinsi ya kupambana na adui kwa namnaya kujilinda, na tasnia haitasita ku fanya hivyo. Kadhalika hivi sasa TEF tunafuatatilia kwa karibu uhusiano wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na vyombo vya habari kutokana na matukio ya mara kwa mara ya kudhalilisha wanahabari wanapokuwa kazini kwa amri yake. Matukio haya yakiendelea, tutalazimika kupitia uhusiano wa RC Gambo na vyombo vya habari nchini.

  Mwisho, tunavipongeza vyombo vya habari, kwa maana ya magazeti, radio, televisheni na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi kwa kutekeleza uamuzi wa kumfungia RC Paul Makonda kwa uaminifu uadilifu wa hali juu, licha ya vishawishi vya hapa na pale vinavyotolewa na wapambe wake.

  Nguvu yetu ipo katika umoja wetu kama wanahabari. Tusiipoteze Mungu ibariki Tanzania.

  Deodatusi Balile
  Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania.
  Mei 19, 2017

  4db4c219-d817-4d7e-9f11-02c7e4a692e4.jpg
   
 2. c

  comte JF-Expert Member

  #361
  May 20, 2017
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 1,129
  Likes Received: 483
  Trophy Points: 180
  Mnaminya uhuru wa habari
   
 3. mtembea kwa miguu

  mtembea kwa miguu JF-Expert Member

  #362
  May 20, 2017
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 914
  Likes Received: 1,078
  Trophy Points: 180
   
 4. Mdf

  Mdf Senior Member

  #363
  May 20, 2017
  Joined: May 16, 2017
  Messages: 116
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Haya yooooote ni jeuri isiyokuwa na sababu,mtu yeyote anayetetea mambo aliyofanya mpaka vyombo vya habari kumsusia sidhani kama yupo sahihi.wanaompenda na walio karibu yake wamshauri aombe msamaha hata kama ni wakinafiki ili maisha yaendelee vinginevyo hata siasa zake bila wanahabari atakwama tu hata kama siyo leo basi huko mbele ya safari.siasa gani atakayofanya kwa ushirikiano wa Star tv tuuu?ni jambo la muda tuu labda kama anafikiria kutoka kwenye siasa.
   
 5. mwengeso

  mwengeso JF-Expert Member

  #364
  May 20, 2017
  Joined: Nov 27, 2014
  Messages: 5,029
  Likes Received: 2,723
  Trophy Points: 280
  Deodatusi Balile: popote ulipo, kama taarifa hiyo umeiandaa wewe mwenyewe, tambua kwamba wewe si mwana habari aliyekamilika. Rejea sifa na wajibu wa mwanahabari ambayo ni kuwahabirisha watu katika mazingira yoyote yale, hata ya hatari.

  Kama hiyo taarifa inawakilisha tasnia ya habari, ni hakika kwamba Tanzania haina wanahabari bali wachumia tumbo. Mnainajisi tasnia ya habari.

  Kipi kinachohatarisha mwanahabari hadi aache kutafuta na kutoa habari, iwapo hata vitani, wanahabari wanakuwepo!

  Iwapo, mna ushahidi tosha kuhusu RC Makonda kuvamia CloudsTV (nukuu ya maandishi katika rangi nyekundu), njia sahihi si kususia kuaandika maswala ya RC Makonda, hata yanayohusu ofisi yake (Mkuu wa Mkoa), ila kumfikisha kwenye vyombo vya sheria. Naamini wanahabari wanao uwezo wa kuchunguza na kukusanya ushahidi wa kutosha, na ndiyo maana wengi hutegemea vyombo vya habari kupata taarifa ya kila tukio na masuala mbalimbali.

  Deodatusi Balile: TOA BORITI JICHONI KWAKO KWANZA
   
 6. mangia22

  mangia22 JF-Expert Member

  #365
  May 20, 2017
  Joined: Mar 10, 2017
  Messages: 455
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  nilishaachaga kuitazama star tv siku nyiiiingi..kwa hio warushe tu wala sina khabari....naskia mapato yao yameshuka sana tofauti na ilivyokua kabla ya uchaguz. sasa hivi wateja wao wengi tumehamia channel ten na azam tv.
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #366
  May 20, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,500
  Likes Received: 22,990
  Trophy Points: 280
  Mkuu Chige, kwanza asante kwa objectivity yako katika hili, ingawa umesema wewe sii mwandishi wa habari, ila kiukweli kwa maswali haya wewe ni zaidi ya mwandishi!. You have the Intellect ya kuhoji kuliko hata mwandishi, kiukweli if you're not a lawyer, then you should have been one, kwenye cross examinations ungewabananisha kwenye kona hadi hakuna pa kutokea. Maswali yako ni mengi na yote ni ya msingi, hivyo kukutendea haki, nitayajibu yote, I'll leave no stone unturned, ila naomba tuu uwe mvumilivu. Nitakujibu taratibu. Naomba usiulize mengine ili nikimaliza ndipo tuendelee na maswali mengine.
  Bashite ni binadamu tuu kama wanadamu wengine. Hii ya kutengeneza movie ya Gwajima, japo sio sahihi ila angetumia msanii wa kweli, lakini kitendo cha kutumia msanii wa kuchonga
  Kiukweli huu ni uendawazimu. Huyu ni mwendawazimu, nimesema mwendawazimu sio mtu wa kuadhibiwa bali anapaswa kusaidiwa.
  Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa Wengi Kuliko Tunavyojidhania?!.
  Insane Anahitaji Huruma, Kusaidiwa. Sio Kulaumiwa, Kulaaniwa na Kususwa! He Needs Help, Tumsaidieje?
  Kama kutengeneza ile movie ni ukichaa, then kitendo cha Bashite kulazimisha kurusha pia ni ukichaa. Japo aligharimia zoezi zima kwa kutoa mtonyo, aliamini kwa mtonyo ule wangerusha, kumbe wenzake wamevuta huku na kule, hivyo alikwenda kwa hasira ambayo sasa ni hasara.
  Hatua haikuwa halali. Kama tangu mwanzo ni ubatili, then ubatili huu unabatilisha zoezi lote kwa ujumla wake.
  Kwa mujibu wa tathmini yangu, Bashite hakuwa na kosa kisheria ila ana kosa kijamii. Kisheria ili kutenda jinai lazima kwanza vitu viwili vifanyike, actus reus (kitendo cha jinai) na mens rea (nia ya kutenda jinai), japo kitendo kimetendeka, jee Bashite alivamia Clouds kwa nia ya kutenda jinai?. Jibu ni no!. Ukiisha mhesabu mtu ni insane, sheria inamsamehe kwa kumuhesabu alikuwa hajui atendalo. Ile kulia kanisani madhabahuni ni uthibitisho tosha this man is insane ila hayuko peke yake!, hata yule mwenzake pia ni insane!. Naomba usiniulize mwenzake yupi!.
  SMG ni sehemu ya MOAT, TEF na UTPC by preference only and not obligation. Maelekezo ya TEF sio compulsory kuyafuata kwa sababu sio binding. Unaweza kuyatekeleza na unaweza kuyapuuza na nothing will happen.
  SMG wanaonewa kwa sababu kuna mambo makubwa na mabaya zaidi tasnia hii imetendewa na wahusika hawakuchukuliwa hatua kali hivi. SMG licha ya kuwa ni chombo cha habari it has to survive, MOAT, UTPC na TEF, hakuna hata mmoja anayetoa sentano yake kuisupport SMG, kwa vile Bashite ndiye mwanaye kipenzi anayependezwa naye, he who pays the piper may call the tune ili maisha yaendelee!. SMG wako right kumualika Bashite.
  Double Standards ya TEF sio kwenye hii issue ya Bashite, kwa sababu hicho kinachoitwa uvamizi is not kuwa ni uvamizi kweli bali imekuwa just blown out of proportion na kufanywa a very big deal. Mambo mangapi makubwa mabaya media tumefanyiwa na sijaona TEF wakifanya kitu.
  Sio lazima kila uamuzi usiokubaliana nao useme, mambo mengine ni actions tuu speak louder than words.
  Kutoka ndani kabisa ya moyo wangu Star TV katika hili wqnaonewa na TEF wamekengeuka!. Journalism ni noble professionals kama udakitari, waandishi hatutakiwi kugoma. Hata wakati wa ule mgomo wa madaktari wengi humu mkawa support, mimi ni miongoni mwa tuliopinga, no matter how bad the situation is, it's un ethical kwa daktari kugoma!, sambamba na mtu wa fire, tanesco, postal na simu etc. Kwenye media ethics nilizosoma mimi, sikumbuki wapi media tuliruhusiwa kugoma, hivyo mgomo wa TEF ni batili! . Acha SMG wapige pesa yao na umma upate habari za uhakika kuhusu Daudi Albert Bashite, mwana Kolomije.
  Nadhani nimeisha izungumza hii huko nyuma. Alichokifanya Bashite kwenye Clouds media ni nothing compared na Jeshi la Polisi lilichokifanya kwa Daudi Mwangosi. Where were TEF wakati wa kifo cha Mwangosi! . Mara ngapi waandishi tunanyanyaswa, tunadhalilishwa, tunapigwa hadi kuuwawa mbona TEF hawatangazi mgomo?. Bashite ni kichaa fulani amefanya ukichaa wake kwa vichaa wenzie wa Clouds media, tusiingeuze ni national agenda.
  Kama nilivyosema mwanzo, japo wewe sio mwanahabari but you're far better kuliko wengi wa wanahabari, kama sio mara yako ya kwanza kusikia viongozi wakisusiwa, then you're far better than me, mimi niko kwenye tasnia hii for 27 years, kwa Tangazo la TEF, ndio mara yangu ya kwanza kuona kususa kunatolewa kwa statement na kufuatiwa na statement ya kukazia hukumu!. Huko nyuma media tumekuwa tunasusa kwa kauli tuu na baada ya muda kususa huko kunayeyuka tuu naturally bila kauli zozote za kulaani au kukazia hukumu.
  To me this is too much attention and emphasis on a non issue!. Media zetu zenyewe zipo zipo tuu kama hazipo, kwa issue kama ya Bashite na mazagazaga yake, tungekuwa na serious media saa hizi tungekuwa tumeisha mtundika msalabani zamani na anayempa kichwa angeisha adabishwa kwa kitu kinachoitwa non volenti mahakamani!, lakini sisi media yetu kazi yetu ni maneno mingi vitendo sifuri!.
  Sijasema alichofanya Bashite ni sahihi, nimesema ule ni ukichaa fulani, hauwezi kuzuiliwa kwa ukichaa mwingine wa TEF
  Standards ni rules and procedures za ku deal na situation fulani ambazo zinakuwa applicable whenever such situation arises. Inapotokea jambo kama hilo na kuwa treated differently!, mangapi mabaya yamefanywa kwa media na kubwa kuliko ni kuuwawa kwa Mwangosi, lakini hao TEF wamefanya nini?!.
  Asante hiyo Jumatatu tuangalie kisha tukutane humu jukwaani ili tupeana feedback.

  Asante

  Paskali
   
 8. k

  kkarumekenge JF-Expert Member

  #367
  May 20, 2017
  Joined: Aug 14, 2013
  Messages: 1,714
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Haya, senema imeanza.Tusubiri!!!
   
 9. Alfred Kikara

  Alfred Kikara Member

  #368
  May 20, 2017
  Joined: May 7, 2017
  Messages: 45
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 25
  Hadithi ya kibiblia juu ya usaliti wa Yuda Iskariote bado roho inatenda kazi,lakini kana ketendo kilchofanywa huyo bwana cha kuvamia tena akitumia askari wenye ailaha na kufumbiwa macho,kama kweli wewe ni mcha Mungu hakikuwa kitendo cha kibinadamu wala cha kuchekelewa.
   
 10. N

  Ndungulila JF-Expert Member

  #369
  May 20, 2017
  Joined: Nov 26, 2016
  Messages: 317
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Je sahara media haikuwepo kwenye makubaliano ya kutompa ushurikiano bashite kama walikuwe na je sahara media sio wanachama kama ni wanachama nisawa na mwanaccm kuto kubaliana na maamuzi ya mabadiliko madogo ya katiba ya sasa
   
 11. Alfred Kikara

  Alfred Kikara Member

  #370
  May 20, 2017
  Joined: May 7, 2017
  Messages: 45
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 25

   
 12. m

  mkaruka ataja rinu JF-Expert Member

  #371
  May 20, 2017
  Joined: Aug 27, 2016
  Messages: 647
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 80
  Hivi Tanzania kuna waandishi wa habari au kuna makanjanja wa habari?
   
 13. Alfred Kikara

  Alfred Kikara Member

  #372
  May 20, 2017
  Joined: May 7, 2017
  Messages: 45
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 25
   
 14. nangalebushesha

  nangalebushesha Member

  #373
  May 20, 2017
  Joined: Apr 15, 2017
  Messages: 39
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 25
  kawaida ya watu wenye akili za ccm bashite kwani hawana jipya ngoja tuone maana mi nasubiri kuona bashite Wa arusha naye tunamfungia hatutaki ujinga
   
 15. lyakurwaD

  lyakurwaD Member

  #374
  May 20, 2017
  Joined: Jan 10, 2017
  Messages: 49
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 15
  Uhuru wa uongo
   
 16. N

  Ndungulila JF-Expert Member

  #375
  May 20, 2017
  Joined: Nov 26, 2016
  Messages: 317
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Mbona nape mnamuita msaliti anapoenda kinyume na matakwa yenu
   
 17. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #376
  May 20, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,240
  Likes Received: 3,602
  Trophy Points: 280
  Mkuu Paskali, yote hayo nayafahamu sana. Lakini kama wamejiwekea utaratibu huo na wanaendesha mambo yao, sioni kama kuna tatizo. Isitoshe issue iliyopo mbele, kwa sasa, sio uhalali wa TEF au MOAT. Issue ni kusalitiana. Labda uniambie kama wahariri wa Startv sio members wa TEF na Startv sio member wa MOAT, lakini kama ni members na vitrip vya mishiko vya TEF huwa wanapokea, na walikubaliana na uamuzi wa kujitenga na Daud Bashite, Startv wanapaswa watekeleze maamuzi ya TEF, na wasipotekeleza TEF hiyo hiyo ya Brela na MOAT hiyo hiyo isiyokuwa na mandate wawashughulikiea wahariri wa Startv na wamiliki wao kwa utaratibu waliojiwekea. Uelewe, kama wahariri wa Startv na Startv wenyewe walijiunga kwenye vyombo hivyo walifanya hivyo baada ya kuona umuhimu wake!

  Na jambo la muhimu kulifahamu ni kwamba, hata hiyo TAJA ni kundi la watu tofauti yake na TEF pamoja na MOAT ni muundo wake tu kisheria. Suala lililoko katika mjadala sio suala la kisheria, ni suala la uaminifu. Ni jambo linaloonekana dogo lakini lenye athari kubwa kijamii. Unapokuwa na wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na wahariri wao "wasaliti" unatarajia nini?

  Naomba unielewe mkuu Paskali. Maoni yangu yanazingatia iwapo tu wahariri wa Startv ni wanachama wa TEF, na Diallo amejiandikisha MOAT na amekuwa akinufaika kama membar wa MOAT.
   
 18. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #377
  May 20, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,240
  Likes Received: 3,602
  Trophy Points: 280
  Nadhani kinachogomba hapa ni uelewa tu. TEF wamejitenga na Daud Bashite ambaye ndiye RC wa Dar es Salaam. TEF hawajajitenga na ofisi ya RC wa Dar es Salaam wala hawana tatizo na utoaji wa habari zinazohusu mkoa wa Dar es Salaam. Si kazi ya TEF kumpeleka mahakamani Daud Bashite. Vyombo vinavyopaswa kufanya hivyo vipo nenda kawaulize hao. Waache TEF na mambo yao kwa kuwa inaonekana hata uelewa wako wa mambo uko low mno!
   
 19. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #378
  May 20, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,240
  Likes Received: 3,602
  Trophy Points: 280
  Kila sekta kuna makanjanja kama unavyothibitisha hapa!
   
 20. mwengeso

  mwengeso JF-Expert Member

  #379
  May 20, 2017
  Joined: Nov 27, 2014
  Messages: 5,029
  Likes Received: 2,723
  Trophy Points: 280
  Una ushahidi na ulichokiandika (maandishi mekundu) au ndio huo ushabiki wa habari za uzushi wa mitandaoni!

  Au utakuja na jibu lako ati Si kazi ya TEF kumpeleka mahakamani Daud Bashite!

  Kama kuna ushahidi usio na mashaka uwekeni wazi, kila raia auone na kushinikiza vyombo husika kuchukua hatua.

  Kumbuka RC Makonda ni Kiongozi wa juu Kitaifa, hivyo hapaswi kutiliwa mashaka ya aina yoyote, maana CHEO NI DHAMANA.
   
 21. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #380
  May 20, 2017
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,055
  Likes Received: 4,438
  Trophy Points: 280
  we shoga mimi sio ccm!!

  usiwe na mawazo ila anayesupport cdm ni cdm au anayeipinga ccm ni mpinzani!! ebu kua na heshimu kuwa ili ni jukwaa!

  haimaanishi kwa sababu mimi ni mwanaume tu, basi naweza kuwa baba yako
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...