Makonda awaponza Star Tv na Sahara Media mbele ya TEF | Page 18 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makonda awaponza Star Tv na Sahara Media mbele ya TEF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurzweil, May 19, 2017.

 1. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2017
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 5,223
  Likes Received: 5,192
  Trophy Points: 280
  UAMUZI WA STAR TV NI USALITI KWA TAALUMA YA HABARI
  Kwa muda wa wiki moja sasa kampuni ya Sahara Communications Limited, wamiliki wa Star TV na vyombo vingine vya habari kupitia mitandao ya kijamii wanasambaza taarifa kuwa watafanya mahojiano maalum na Mkuu wa Mkoa wa Dar ea Salaam, Paul Makonda, Jumatatu Mei 22, 2017.

  Kusudio hilo la Star TV limekuja wakati kiongozi huyo akiwa amefungiwa na vyombo vya habari kwa uamuzi ulioitikiwa kwa pamoja baina ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na kuungwa mkono na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) na taasisi nyingine za kihabari nchini. Uamuzi wa kumfungia Makonda uliotangazwa Machi 2017, ilitokana na kiongozi huyo kuvamia Kituo cha Utangazaji cha Clouds Madia, March 17, 2017 akiwa na askari wenye bunduki.

  Uvamizi wa Clouds ulikuwa mwendelezo wa matukio ya RC Makonda kudhalilisha wanahabari, kutukana na kutoiheshimu taaluma ya habari. Katika tamko hilo, Makonda tulimpa masharti mepesi kurejesha uhusiano na tasnia ya habari, ambayo ni kuomba radhi waandishi wa habari kwa tukio la Clouds na matukio mengine kwa ujumla wake kama sehemu ya uungwana wa Kitanzania.

  Tulisema katika tamko kwa yeyote atakayeshirikiana na Makonda naye tutamhesabu kama adui wa tasnia ya habari nchini. Kwa mantiki hiyo tunasema ikiwa Star TV wameamua kushirikiana na Makonda, basi ni wazi wameamua kwa hiyari yao wenye kujitangaza kama adui wa tasnia ya habari nchini.

  Kila Mtanzania anajua jinsi ya kupambana na adui kwa namnaya kujilinda, na tasnia haitasita ku fanya hivyo. Kadhalika hivi sasa TEF tunafuatatilia kwa karibu uhusiano wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na vyombo vya habari kutokana na matukio ya mara kwa mara ya kudhalilisha wanahabari wanapokuwa kazini kwa amri yake. Matukio haya yakiendelea, tutalazimika kupitia uhusiano wa RC Gambo na vyombo vya habari nchini.

  Mwisho, tunavipongeza vyombo vya habari, kwa maana ya magazeti, radio, televisheni na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi kwa kutekeleza uamuzi wa kumfungia RC Paul Makonda kwa uaminifu uadilifu wa hali juu, licha ya vishawishi vya hapa na pale vinavyotolewa na wapambe wake.

  Nguvu yetu ipo katika umoja wetu kama wanahabari. Tusiipoteze Mungu ibariki Tanzania.

  Deodatusi Balile
  Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania.
  Mei 19, 2017

  4db4c219-d817-4d7e-9f11-02c7e4a692e4.jpg
   
 2. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #341
  May 20, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,213
  Likes Received: 3,580
  Trophy Points: 280
  Hasara gani wanayopata?
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #342
  May 20, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,758
  Trophy Points: 280
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #343
  May 20, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,758
  Trophy Points: 280
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #344
  May 20, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,758
  Trophy Points: 280
  Mkuu Chige, Daudi Albert Bashite pale ni kama nyumbani kwake, anaingia saa yoyote bila kupiga hodi au kutoa taarifa. Wale makirikiri ni walinzi wake kila mahali huenda nao isipokuwa msalani na maliwatoni!. Tukio lilikuwa blown over proportion!.

  Media zetu are too weak and too poor to say no to DAB!. Hili nililisema hapa
  Media Kususia Habari za Fulani: Jee Tanzania Tuna Independent Media Yenye Jeuri Hiyo?.

  Hivyo kuwalaumu Star TV ni kuwaonea bure!.
  It's high time TEW watoe rules of engagement with their rules of ethics kuwa hiki kikifanyika, ndipo media isusie, na sio kwa hii double standards za cherry picking.

  Jumatatu asubuhi macho na masikio yetu yote ni Star TV, tunasubiri kwa hamu kumsikia Daudi Albert Bashite wa Koromije akiwa live mubushara au kukiri au kukanusha tuhuma zote zinazomkabili.

  Mimi nitaangalia na nawashauri na wengine tuangalie na kama kuna fursa za kupiga simu hata mimi nitapiga kuulizia baada ya kubainika rasmi jina lake halisi ni Daudi Bashite, kwa nini mpaka sasa bado anatumia jina la wizi la Paul Christian?.

  Paskali
   
 6. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #345
  May 20, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,213
  Likes Received: 3,580
  Trophy Points: 280
 7. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #346
  May 20, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,213
  Likes Received: 3,580
  Trophy Points: 280
  Mkuu Paskali, kuwalaumu StarTV ni sawa. Makubaliano, hata kama yalikuwa ni ya "kijinga" kwa mtazamo wako, lakini kama Startv waliyaridhia kama wanachama wa TEF/MOAT na clubs wakati ule, wanachokifanya ni usaliti unaostahili kushughulikiwa kwa kiwango cha kutoa fundisho kwa wengine!
   
 8. roboka kafwekamo

  roboka kafwekamo JF-Expert Member

  #347
  May 20, 2017
  Joined: Mar 12, 2017
  Messages: 828
  Likes Received: 447
  Trophy Points: 80
  Hivi wamechacha sana kiasi hata masikio na masikio vimeshsu maelekezo. Telepicha gani.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #348
  May 20, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,758
  Trophy Points: 280
  Mkuu Chabusalu, kwanza sijasema katazo ni la kijinga, its just not practical! .

  Sii wengi wanaojua kuwa TEF na MOAT ni taasisi binafsi kama makampuni binafsi na vimesajiliwa Brela, na hazina mandate kwa sababu vyombo hivi sio statutory media organizations na bonafide, representatives za waandishi, hivyo uamuzi wake sio binding. Chombo statutory kama Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania ni TAJA, Tanzania Journalist Association. Taasisi ya Media inayotambulika rasmi ni Baraza la Habari Tanzania, Media Council, MCT ambalo kwa sheria mpya linakufa na sio TEF sio MOAT!. Hivi ni vikundi tuu vya watu.

  Paskali
   
 10. No Escape

  No Escape JF-Expert Member

  #349
  May 20, 2017
  Joined: Mar 7, 2016
  Messages: 4,965
  Likes Received: 4,684
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wameona wanajila! Mishahara watalipaje sasa....
   
 11. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #350
  May 20, 2017
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,632
  Likes Received: 2,702
  Trophy Points: 280
  Star TV ni kama small house ya TBCCM
   
 12. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #351
  May 20, 2017
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,632
  Likes Received: 2,702
  Trophy Points: 280
  Mamaaa Bashite Lenyewe hilooo
   
 13. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #352
  May 20, 2017
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,634
  Likes Received: 3,495
  Trophy Points: 280
  Wakati mnawafungia watu mnasahau kuelewa kwamba sie ni watu na tuna haki ya kuhabarishwa. Kama hamuwezi kutekeleza hii haki yetu mnabaki kufanya mini sasa, akheri muache kufanya kazi ya habari ili wanaoweza kuifanya watusaidie kutuhabarisha. Nawapongeza sana Star Tv
   
 14. M

  Msukumakizazi JF-Expert Member

  #353
  May 20, 2017
  Joined: Jan 13, 2017
  Messages: 1,040
  Likes Received: 610
  Trophy Points: 280
  kumbe wanatangaza kwa kutumia maspika!!!
   
 15. mjingamimi

  mjingamimi JF-Expert Member

  #354
  May 20, 2017
  Joined: Aug 3, 2015
  Messages: 12,810
  Likes Received: 10,651
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 16. cocochanel

  cocochanel JF-Expert Member

  #355
  May 20, 2017
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 19,713
  Likes Received: 61,169
  Trophy Points: 280
  Tunajua awamu hii hauipendiiiiii, tho unajitahidi kujificha ila tunakusoma unayoandika na kukujua hata pale unapofikiri ujanja wa kuweka zig zag...hatutakugundua tunakugundua

  Hivi RC nae kakukosea nini!? Umetoa hukumu juu yake siku nyingi zimepita naona hapa ni umejionyesha zaidi kuwa upo pamoja na hao hao...vibahasha... mjisikitikie huku hamlali mnamuwaza yeye n.k. eeeeh

  Awamu ya tano hiii

  Makonda oyeeeeeee

  Magufuli oyeeeeeeee
   
 17. a

  abuumwasiti20 JF-Expert Member

  #356
  May 20, 2017
  Joined: Oct 19, 2016
  Messages: 289
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 80
  Haya sasa ngoja tuone chombo chahabar nakenyewe kitazuiwaje kurusha habar nawakat kinamitambo yake nakila siku kinarusha habar
   
 18. c

  chige JF-Expert Member

  #357
  May 20, 2017
  Joined: Jul 11, 2016
  Messages: 7,148
  Likes Received: 12,815
  Trophy Points: 280
  Uliyosema yote kuhusu Bashite na Clouds hapo kabla ni ukweli tupu!!! Hata hivyo, twende hatua kwa hatua na unijibu maswali yangu kama ulivyofanay kwa hilo hapo juu:

  Mosi, kwavile tu alikuwa na ukaribu huo na Clouds, unadhani alikuwa sahihi kutengeneza story ya Gwajima kwa manufaa yake binafsi?! Do you really believe it?

  Pili, unaamini alikuwa sahihi kulazimisha kile kipindi kirushwe tofauti na wenyewe ambao hawakuwa tayari kwavile stori ilikuwa haija-balance!!!

  TIP: Ushahidi wa kimazingira unaonesha ni kweli Bashite alishinikiza hiyo habari na ndio maana, baada ya kushindikana kurushwa, mtu wa mwanzo kuisambaza ile habari mitandaoni alikuwa ni Le Mutuz.

  Swali la tatu: Wewe ukiwa kama Mwanahabari; hivi ni kweli unaamini hatua Bashite kutoka na ile content na kwenda kuisambaza informally ilikuwa ni hatua sahihi inayoweza kuhalalishwa kutokana na ukaribu wake na Clouds?!

  ANGALIZO: Hata katika mazingira ya mahusiano ya kawaida ya kati ya mwanadamu mmoja na mwingine; hutokea wakati mwingine watu mkawa mmeshibana kama ilivyokuwa kwa Clouds na Bashite! Na katika hali hiyo mmoja anaweza kujikuta anafanya jambo moja dhidi ya mwenzake huku akiamini anachofanya ni jambo la kawaida tu!!

  Pamoja na kudhani hilo ni jambo la kawaida, mwenzako anajikuta amekwazika kweli kweli... tena sana! Na bila ya kupepesa macho, anakwambia wazi kwamba this's not right, UMENIKOSEA kwahiyo nitake radhi!!!!

  Hivi kwa muungwana bila kujali ni kama kweli amekosea au hapana, hawezi kuomba radhi kwa sababu tu mwenzake amemkwaza?! Hivi mara zote ambazo huwaga tunawaomba radhi wenzetu tunakuwa tumekosea?


  Now tell me, hivi unaamini kabisa, from deep inside your heart, pamoja na yote hayo, Bashite hakuwa na kosa hata kidogo?! Nini kimemfanya asiombe radhi kama alivyotakiwa? Au kwavile yeye ni Mkuu wa Mkoa ndo anadhani hawezi kuomba radhi taasisi zingine?!

  Turudi kwa hao Star TV unaosema wanaonewa!!

  SWALI: Je, unataka kuniambia Sahara Media sio sehemu ya MOAT, TEF na UTPC?!

  Kama sio sehemu ya hizo taasisi, usiende swali linalofuata lakini kama ni sehemu ya MOAT, TEF na UTPC; ni kwa namna gani unasema kwamba Star TV wanaonewa?! Labda ukumbushwe azimio la Jukwaa la Wahariri na Club ya Waandishi wa Habari:

  Jukwaa.png
  Kama Star TV ni sehemu ya hizo taasisi; do you really believe kwamba Star TV wanaonewa?! Au unaweza kunipa mfano mmoja tu wa media yoyote (achana na TBC) ambayo ilishirikiana na Daudi Albert Bashite lakini pamoja na yote hayoTEF na UTPC hawakutoa tamko?! Mfano wako utasaidia kuonesha double standard ya TEF na UTPC... kwamba, kumbe wapo wengine walioshirikiana na Bashite lakini hakuna tamko lolote lililotolewa dhidi yao?

  Au kama Star TV na Sahara Media kwa ujumla waliona uamuzi wa TEF & UTPC haukuwa sahihi; kwanini hapo hapo hawakuweka wazi kwamba hawakubaliani na uamuzi huo na hivyo; wao kama wao wataendelea kushirikiana na Bashite?!

  Kutoka ndani kabisa ya nafsi yako, hivi ni kweli unaamini kabisa kwamba Star TV katika hili wanaonewa?

  Aidha unasema:
  Naamini you're smart enough kufahamu nini maana ya double standard!!! Hivi unaweza kuniambia ni double standard ipi iliyofanyika ama dhidi ya Bashite au Star TV?!

  Mimi sio mwanahabari lakini hii sio mara yangu ya kwanza kusikia viongozi mbalimbali wakisusiwa hapa nchini!!! Hivi ikiwa wengine walikuwa wanasusiwa huku ukiamini kilichofanyika sasa ni double standard; do I miss something in the real meaning of double standard?!

  Btw, inawezekana aliyofanya Bashite yote kwako ni sahihi lakini in the eyes of TEF aliyofanya sio sahihi!!! Kwahiyo ulitaka TEF wasichukue hatua dhidi ya Bashite hadi watakapotoa hizo rules of engagement ingawaje hapo kabla wameshawahi kuchukua hatua kama hizo kwa wengine?!

  Frankly speaking, please gimme Class 101: The Meaning, Application and Limitations of the phrase Double Standard.

  HITIMISHO: Kwamba wewe utafuatilia kipindi na unawashauri wengine wafanye hivyo wala hauna sababu ya kuhamasisha watu kwa sababu mgogoro ni kati ya Daudi Albert Bashite na vyombo vya habari na key players wao!!! Azimio la TEF na UTPC wala haliwataki wananchi wasishirikiane na Bashite; na isitoshe, wala hawana mamlaka hayo!!! Hata hao members wa TEF na UTPC I bet nao wataangalia kwa sababu, nothing is personal here!!

  Hata mimi huenda nikaangalia... na kama atakuwa anaongea mambo ya msingi huenda nikamfuatilia kwa sababu sina mgogoro na Bashite!!! Muhimu ni kama nilivyosema hapo awali kwamba:
   
 19. c

  chige JF-Expert Member

  #358
  May 20, 2017
  Joined: Jul 11, 2016
  Messages: 7,148
  Likes Received: 12,815
  Trophy Points: 280
  Sasa na wewe ndo unaongea mambo gani hapa!!! Kwani wanaotoa ruhusa au kuzuia media kutoa content ni TEF na UTPC?! Au kwani hilo angalizo limetolewa na TCRA?! Au kuna popote ambapo TEF na UTPC walisema media yoyote ikishirikiana na Bashite basi watazuiwa kurushwa habari?!
   
 20. a

  abuumwasiti20 JF-Expert Member

  #359
  May 20, 2017
  Joined: Oct 19, 2016
  Messages: 289
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 80
  Kwan tv nizakwenu?tv niyaantony dialo anamamaka yakufanya atakavo iliradi asivuje sheria za nchi wala hamjamfungulia tv yake wala kumchangia hata mia acha afanye atakavo kwan hakuna anaempangia
   
 21. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #360
  May 20, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,758
  Trophy Points: 280
  Kwa kiwango cha uchafu kilichopo na kasi ya Magufuli ya safisha safisha anayokwenda nayo sasa, ukiachia ile nguvu ya soda aliyoanza nayo ili tuu kupata kiki, then hata 2025 haitoshi kukamilisha kazi ya kuondoa uozo wote na kukamilisha miradi yote, hivyo tumeshauri tubadili katiba tumuongeze angalau kama Kagame, Museveni au Mugabe.
  Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
  Paskali
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...