Makonda awaponza Star Tv na Sahara Media mbele ya TEF

Msiteseke bila sababu, hivi hamjui sahara media ni ccm!! Kwani hamumjui mmiliki wake ni nani??? Hii tv ni propoganda ya ccm kwa muda mrefu sasa.
 
Sio sheria kufuata matakwa ya TEF,kila chombo cha habari kina mrengo wake,sio suala la TEF kutishia au kushutumu,waache wenyewe wapime na kuamua.STAR TV ni chombo huru
 
Yaani, natamani hawa star TV washupaze shingo alafu warushe kipindi hicho ili tuone watakavywo nyooshwa na wanainchi na wanahabari wenzao eewe mungu mjibu maombi jibu ombi langu hili.
 
Nyie wasimamizi wa vyombo vya habari na nyie hakuna jipya robo tatu yenu MNA vyeti feki mkikaguliwa hakuna wa kutokea sijawahi kuona wanafiki wakubwa Kama waandishi wa habari wa tanzania
 
UAMUZI WA STAR TV NI USALITI KWA TAALUMA YA HABARI
Kwa muda wa wiki moja sasa kampuni ya Sahara Communications Limited, wamiliki wa Star TV na vyombo vingine vya habari kupitia mitandao ya kijamii wanasambaza taarifa kuwa watafanya mahojiano maalum na Mkuu wa Mkoa wa Dar ea Salaam, Paul Makonda, Jumatatu Mei 22, 2017.

Kusudio hilo la Star TV limekuja wakati kiongozi huyo akiwa amefungiwa na vyombo vya habari kwa uamuzi ulioitikiwa kwa pamoja baina ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na kuungwa mkono na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) na taasisi nyingine za kihabari nchini. Uamuzi wa kumfungia Makonda uliotangazwa Machi 2017, ilitokana na kiongozi huyo kuvamia Kituo cha Utangazaji cha Clouds Madia, March 17, 2017 akiwa na askari wenye bunduki.

Uvamizi wa Clouds ulikuwa mwendelezo wa matukio ya RC Makonda kudhalilisha wanahabari, kutukana na kutoiheshimu taaluma ya habari. Katika tamko hilo, Makonda tulimpa masharti mepesi kurejesha uhusiano na tasnia ya habari, ambayo ni kuomba radhi waandishi wa habari kwa tukio la Clouds na matukio mengine kwa ujumla wake kama sehemu ya uungwana wa Kitanzania.

Tulisema katika tamko kwa yeyote atakayeshirikiana na Makonda naye tutamhesabu kama adui wa tasnia ya habari nchini. Kwa mantiki hiyo tunasema ikiwa Star TV wameamua kushirikiana na Makonda, basi ni wazi wameamua kwa hiyari yao wenye kujitangaza kama adui wa tasnia ya habari nchini.

Kila Mtanzania anajua jinsi ya kupambana na adui kwa namnaya kujilinda, na tasnia haitasita ku fanya hivyo. Kadhalika hivi sasa TEF tunafuatatilia kwa karibu uhusiano wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na vyombo vya habari kutokana na matukio ya mara kwa mara ya kudhalilisha wanahabari wanapokuwa kazini kwa amri yake. Matukio haya yakiendelea, tutalazimika kupitia uhusiano wa RC Gambo na vyombo vya habari nchini.

Mwisho, tunavipongeza vyombo vya habari, kwa maana ya magazeti, radio, televisheni na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi kwa kutekeleza uamuzi wa kumfungia RC Paul Makonda kwa uaminifu uadilifu wa hali juu, licha ya vishawishi vya hapa na pale vinavyotolewa na wapambe wake.

Nguvu yetu ipo katika umoja wetu kama wanahabari. Tusiipoteze Mungu ibariki Tanzania.

Deodatusi Balile
Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania.
Mei 19, 2017
Divide and rule
 
Kumbe jamaa bado bachela?
Mana kama ingekua ameoa asingeweza kutuma picha kama hizi huyu jamaa itaku ana mapungufu siyo bure au hii ni fake I'd yake kama ndiyo mwenyewe basi nimeamini ukubwa wa pua siyo wingi wa......
Basi kesho waandishi uchwara utasikia wameandika habari le mutuz kakinukisha jamiifurums.
 
Sioni mantiki ya kumfungia RC mm nkiwa kama Mtanzania nafaidika nini ? na Mgomo huo Tatizo la Waandishi wa Habari nao Njaa Mbele kuliko kuzingatia Maslahi ya Watanzania Yakiwa kuta ndo mnataka Wananchi nao Tuwaunge Mkono!
 
  • Thanks
Reactions: nao
Sioni mantiki ya kumfungia RC mm nkiwa kama Mtanzania nafaidika nini ? na Mgomo huo Tatizo la Waandishi wa Habari nao Njaa Mbele kuliko kuzingatia Maslahi ya Watanzania Yakiwa kuta ndo mnataka Wananchi nao Tuwaunge Mkono!
Ngoja nikuulize swali: Je, unakubaliana na kitendo ambacho alikifanya Makonda pale Clouds TV?! Unaamini alikuwa sahihi kabisa pale na hakuna kosa lolote alilofanya?!
 
Tef wamekaza nafsi ila kimoyomoyo wanaomba DAB aombe peace ili warudi kupokea bahasha kwake,,, hakuna watu wenye njaa kama waandishi wa habari,,, ofisini kwetu huwa hawakauki kuja kumpiga bosi wetu virungu hata km hakuna taarifa,, yani wapo wapo tu hata kuvaa hawajui
 
Siku hiyo watz wote watafungua startv kutaka kumsikiliza Makonda, sio ccm na cdm tu, hata hawa TEF na ndugu zao hawatobanduka kwny kioo. Achana na watz wanavyopenda habari motomoto bhana...
Watz WOTE wakati mi sitaangalia?
 
Mnapoteza muda wenu tu. Star TV ni chombo cha habari cha mtu binafsi. Yeye ndo ana uamuzi wa namna gani akitumie so long havunji sheria za nchi. Hayo mengine sijui TEF kuitangaza Star TV kuwa adui wa tasnia ya habari ni kujifurahisha tu.
 
Wakati huohuo kuna magazeti kadhaa yalilipoti habari ya Makonda kuhojiwa na bunge, na nyinyi mnaojiita waariri sijui MOAT hamkuwahi kusema lolote,sijui kwa vile moja wapo lilikuwa la mwenyekiti wenu?,all in all naona mnatuboa tu, wala hamna maana, either mnacheza ngoma msioijua au utajiri wenu na mitaji yenu kuanzisha vyombo hivyo ilikuwa ya magumashi tu
 
- Ungekaaa pembeni napigana na samaki mkubwa huyo kwa jina la bandia maana huyu amepata ujumbe atafikishia wenzake kuwa kumbe wanapoteza muda na mgomo hahahahahhaa

le Mutuz
Nikae pembeni kivipi kuna sehemu nimeona kile ulichosema nadhani na Diallo mmemlisha SUMU ngoja tuone nani atapata madhara makubwa j3 issue sio kudeal na huyo member Mimi nakwambia ukweli naojua ili tatizo lakujifanya ukiwa ccm ndo UZALENDO ni upumbavu wa ajabu
 
Usitaje bure au bila sababu jina la Mungu au ili uonekane na wewe unamjua Mungu....
Now DAB next Mrisho Gambo, pascal mayalla, pombe magufuri, etc it's just a matter of time, lets wait!!
 
Tatizo hawa wanahabari hawana muungano mathubuti wa kumdhibiti D.A.B. Si ajabu tena siku zijazo watatokea wengine wa kumpa airtime mr. Zero
 
Back
Top Bottom