Makonda atoa onyo kali kwa viongozi wa Dini

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
upload_2016-3-28_11-6-58.png

  • Asema atawasweka ndani viongozi wa dini wote watakaokimbilia polisi kutatua migogoro yao ya ndani ya makanisa.
  • Asema serikali na polisi ndio wanatakiwa kwenda kanisani kutatua migogoro yao, sio makanisa kukimbilia polisi.
  • Asema kuna watu wanatoa mafunzo(ya kijeshi) kwa watoto kwenye bonde la mto ulio mpakani mwa Dar es Salaam na mkona wa Pwani.
  • Asita kuelezea mengine "mazito" ya kiusalama maana Rais hajamruhusu kuyasema
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema mkoa wake hauko salama kama watu wanavyodhani kwa sababu silaha nyingi zinamilikiwa kiholela na mafunzo ya matumizi ya silaha hizo hutolewa hata kwa watoto.Makonda alisema hayo jana wakati wa ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano na kuwataka wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kuhakiki silaha zao na kusalimisha zile zinazomilikiwa kinyume cha sheria.

Alisisitiza kwamba ifikapo Julai Mosi, operesheni maalumu ya kukamata silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria itaanza na yeye mwenyewe ndiye atakayeiongoza.“Tumegundua kwamba kwenye bonde la mto unaotenganisha Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, kuna mafunzo yanatolewa kwa watoto. Wazazi wanadhani watoto wao wamekwenda shule kumbe wamechukuliwa huko. Hatuwezi kukubali hali hiyo iendelee,” alisema.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka waumini waendelee kumwombea ili aifanye kazi yake vizuri kwa kutenda haki na aliwataka pia kumwombea pia Rais John Magufuli kwa sababu kazi anayoifanya ni kubwa.Alisema Rais anapotumbua jipu moja, ndani yake kuna kundi la watu wanaoathirika na hatua aliyoichukua hivyo, alisema watu wa aina hiyo hawawezi kumpenda kwa sababu amevunja mtandao wa masilahi yao.

“Ninaomba kanisa pamoja na viongozi wote wa dini mnisaidie katika kuhimiza suala la ulinzi na usalama ili amani yetu iendelee kudumu. Ninaomba tushirikiane katika hilo, Dar es Salaam haiko salama kama mnavyodhani, mengine siwezi kusema kwa sababu sijaruhusiwa na Rais,” alisema.

Migogoro kanisani

Akizungumzia migogoro makanisani, Makonda alisema hataki kusikia kiongozi yeyote wa dini anakimbilia polisi au mahakamani kutaka suluhisho la matatizo yao ya ndani na kuwa atamweka ndani atakayejaribu kufanya hivyo.

Alisema ni aibu kubwa kwa kanisa kukimbilia kwenye vyombo vya dola badala ya polisi na Serikali kukimbilia kanisani kuomba ushauri. Alisema kanisa ndicho chombo cha usuluhishi wa matatizo mbalimbali ya jamii.

“Serikali inahitaji msaada wa kanisa na viongozi wa dini ili iweze kufanya kazi vizuri. Sitaki kusikia polisi wanakwenda kanisani (kukamata watu) katika mkoa wangu na wale wanaotoa taarifa kutaka polisi nitawaweka ndani,” alisema Makonda ambaye kabla ya kuwa mkuu wa mkoa, alikuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Askofu Mokiwa

Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentino Mokiwa alibainisha mambo mbalimbali aliyoyaita majipu ambayo yanafanya kanisa hilo lisiendelee katika kufundisha waumini wake yaliyo mema.

Mokiwa alitaja mambo hayo kuwa ni pamoja na mashindano ya kimadhehebu. Alisema madhehebu mbalimbali yanashindanishwa kupima kanisa lipi ni kubwa, lina waumini wangapi, linamilikiwa na nani na nguvu yake ni ipi.

Jambo jingine alisema ni maaskofu wenyewe kupigana vita. Alisema sasa ni kawaida kwa askofu mmoja kumchimba mwingine, askofu mmoja kupanga mapinduzi dhidi ya mwingine na baadhi ya maaskofu kutukanana waziwazi.

“Maaskofu wanasemana na kusingiziana mambo ya uongo, injili haiwezi kwenda mbele. Wengine wanatumia fedha na vyombo vya habari ili kutukana wengine. Kanisani pia kuna walaghai na wezi ambao wanavaa kanzu,” alisema Askofu Mokiwa.

Alisisitiza kwamba waumini wanapaswa kuogopana wao kwa wao kwa sababu ndiyo vikwazo vya wao kwenda mbinguni.


Chanzo :Mwananchi
 
Yeye anao uwezo wa kisheria wa kuwazui Polisi kutekeleza wajibu wao wa kisheria chini ya sheria zilizotungwa na Bunge kwa mujibu wa Katiba yetu? Yaani mtu anaona kafanyiwa jinai kanisani kwao, Kwa akili ya Makonda mtu kama huyo yeye "atamweka ndani" kama akilipeleka jambo hilo Polisi. Naona jamii ya wana Dar es salaam inazidi kumdekeza Makonda!!?
 
Kwa hili la Kuwa Sweka Ndani wale wote watakaopeleka kesi za kikanisa polisi, Hili namuunga Mkono Ndugu Yangu Makonda Tena Asiwaonee huruma kabisa Maana hawa wamesha Kengeuka kutoka kuwa Kondoo Adi kuwa Mbuzi.

Juzi, Juzi nilishuhudia Waumini wa kanisa la Anglikana wakimgomea Askofu wao Nilishangaa sana Yani waumini wamekuwa na Nguvu kuliko Mchungaji? Hata shetani anatushangaa maana siku hizi waumini hawataki kuchungwa wamekuwa Mbuzi. Maana sote tunajua Mungu ametuasa kuheshimu mafuta yaliyo juu ya Mtumishi wake.

Tena nakuomba Ndugu Makonda na Watandikwe viboko kabisa. Wanatia haibu Kanisa la Mungu.
 
Napata shida sana matamko ya kiserikali yanapotolewa kwenye nyumba za ibada. Hili jambo naliona sana kwa wenzetu Wakenya na linawakera sana watu wengi pale viongozi wa kisiasa wanapotumia majukwaa ya kidini kutoa matamko kwa hili wamelalamikiwa saana. Wakati wa uchaguzi lilianza kujitokeza na watu walilikemea sana, naona linaanza kushamiri na tunaweza kuanza kulaumiana pale watu wengine wakitumia hayo hayo majukwaa kujibu mashambulizi.
Wanasiasa wana majukwaa mengi sana na wakati mwingine ndani ya nyumba ya ibada kuna wengine wanakarahika na wengi hujuliza wamekwenda kusali na kupata neno la Mungu au kusikiliza porojo za wanasiasa? Hili suala la kutumia makanisa au misikiti kuhubiri siasa ni vyema lisiendekezwe!
 
Kw
Kwa hili la Kuwa Sweka Ndani wale wote watakaopeleka kesi za kikanisa polisi, Hili namuunga Mkono Ndugu Yangu Makonda Tena Asiwaonee huruma kabisa Maana hawa wamesha Kengeuka kutoka kuwa Kondoo Adi kuwa Mbuzi.

Juzi, Juzi nilishuhudia Waumini wa kanisa la Anglikana wakimgomea Askofu wao Nilishangaa sana Yani waumini wamekuwa na Nguvu kuliko Mchungaji? Hata shetani anatushangaa maana siku hizi waumini hawataki kuchungwa wamekuwa Mbuzi. Maana sote tunajua Mungu ametuasa kuheshimu mafuta yaliyo juu ya Mtumishi wake.

Tena nakuomba Ndugu Makonda na Watandikwe viboko kabisa. Wanatia haibu Kanisa la Mungu.
Kwani Mchungaji no Mungu! Km akienda ndvy cvyo je hdi kupindukia
 
Hapa sasa patamu, sasa Gwajima yuko huru maana atayemshtaki polisi atawekwa ndani yeye. Haya viongozi wa Makanisa uchwara endeleeni kuchukuwa wake wa waumini wenu hamtapelekwa polisi kama alivyafanya Flora na Gwajima.
 
Back
Top Bottom