Makonda ataka TAKUKURU kuwachunguza watendaji wa mkoa wa Dar-es-Salaam kwa tuhuma za ubadharifu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,994
144,329
Wakati yeye akituhumiwa kwa mambo mengi na akiwa hajajibu tuhuma zinazomkabili,Mkuu wa Mkoa wa Dar-ez-Salaama,Paul Makonda,ameitaka TAKUKURU kuwachunguza watendaji wa mkoa huo kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ys shilingi bilioni 7 za miradi ya maendeleo.

Makonda amedai yeye na timu yake ndio wamegundua udanganyifu katika vitabu vya mahesabu vya miradi viliyowasilishwa kwake na hivyo katoa wiki mbili kwa TAKUKURU kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua wahusika.

Chanzo:TBC 1

Hii ndio Tanzania bwana!

Ni bora tukayajua haya ili kama ni nyongo kupanda basi iendelee kutupanda tu ili 2020 tusifanye makosa.

Maumivu na maudhi haya ndio yatatupa akili maana sisi ni wepesi wa kusahau.
 
Aisee si ilishatangazwa kuwa huyu jamaa asipewe promo yoyote mbona wewe unamjengea shavu?
Vitu vingine kwakweli havivumikiki na ni bora watu wakavijua ili tuona jinsi wenye mamlaka wanavyotuchukulia.

Hii nchi inasikitisha sana
 
Wakati yeye akituhumiwa kwa mambo mengi na akiwa hajajibu tuhuma zinazomkabili,Mkuu wa Mkoa wa Dar-ez-Salaama,Paul Makonda,ameitaka TAKUKURU kuwachunguza watendaji wa mkoa huo kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ys shilingi bilioni 7 za miradi ya maendeleo.

Makonda amedai yeye na timu yake ndio wamegundua udanganyifu katika vitabu vya mahesabu vya miradi viliyowasilishwa kwake na hivyo katoa wiki mbili kwa TAKUKURU kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua wahusika.

Chanzo:TBC 1

Hii ndio Tanzania bwana!
Hakuna tatizo kwa kuwa yeye bado ni RC wa DSM, na hivyo pamoja na tuhuma dhidi yake bado anawajibika kufuatilia hatua za maendeleo za mkoa wake.
 
Back
Top Bottom