Makonda apewa gari ya milioni 55 na kampuni ya GWM

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
KAMPUNI ya Kifaru Motors wakishirikiana na Great Wall Motors (GWM) wametoa msaada wa gari aina ya Wingles yenye thamani ya Sh milioni 55 kwa ofi si ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kusaidia shughuli za maendeleo.Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda amezishukuru kampuni hizo na kusema kuwa gari hiyo itawasaidia kukabiliana na changamoto ya uhaba wa magari uliopo katika ofisi hiyo.

Aliongeza kuwa gari hiyo itakabidhiwa kwa Idara ambayo inafanya kazi nzuri. Alisema: “Nataka wananchi wa Mkoa huu ndio waamue gari hii iende katika idara gani ambayo wanaona inafanya kazi nzuri, nitatoa namba ya kupiga kura katika vyombo mbalimbali vya habari na baada ya siku 10 mshindi atapatikana na atakabidhiwa gari na huu utakuwa ni utaratibu wetu kila mwaka.”

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Kampuni hizo Meneja wa GWM, Jianguo Liu alisema kampuni hizo zilifikia uamuzi wa kutoa msaada huo baada ya kuvutiwa na utendaji kazi wa Makonda pamoja na serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.

Chanzo: Habari leo
 
Hehehe GWM awapendi ujinga. Halafu madereva kasema itakua utaratibu wa kila mwaka? Hii inamaanisha atakuepo kwenye hicho kiti cha enzi milele au mi sjaelewa
 
Inawezekana idara ambayo inafanya kazi vizuri ina vifaa vya kutosha ikiwa ni pamoja na magari na ndio maana ikaonekanan comparatively ina- perform. Mara nyingi opinion za public haziwi fair au hazina technical component. Mkuu wa Mkoa ana timu ya wataalam ambayo inaweza kufanya performance review ambayo ni technical na taarifa hiyo ikatumika kama kigezo cha kutoa gari hizo
 
Hii nayo ni Habari? Hiyo Kampuni isaidie Mitaji kwa Masikini na sio kuosha sura.... Million Hamsini tunasubiri huku vijijini
 
utaratibu wa kila mwaka kwa maana gwc kila mwaka watavutiwa na utendaji wa bashite na kutoa gari.
 
Hehehe GWM awapendi ujinga. Halafu madereva kasema itakua utaratibu wa kila mwaka? Hii inamaanisha atakuepo kwenye hicho kiti cha enzi milele au mi sjaelewa
Huyu jamaa zero kabisa eti kila mwaka maana yake ana uhakika wa kupewa gari mwaka? Au ana jipa mwenyewe???...huyu bashite
 
RC amkabidhi RAS hiyo gari aipangie matumizi maana yeye ndiyo mtendaji Mkuu wa Mkoa. Yeye ndo anajua wapi kuna upungufu na wapi pataleta tija endapo watakuwa na aina hiyo ya gari. Zaidi ya hapo ni siasa na kutafuta KK
 
Ingawa wengi mnamuona Magufuli anamkumbatia Makonda lakini atakapolala mbele na GSM ndio mtapata jibu kamili.
 
Bashite for really..yaani ameona akitumia kauli ya....nataka wananchi wa dar waamue gar ipelekwe wapi..

Hiyo kauli imejaa misifa tu...
 
Back
Top Bottom