MAKONDA ANAHUJUMIWA NA VIONGOZI WA SERIKALI YA MTAA WA TUANGOMA - KIGAMBONI
Katika hali ya kuhuzunisha na kushangaza juhudi za Mh. Paul Makonda katika kutunza mazingira ili kuliweka jiji letu katika hali ya usafi kama mkuu wa mkoa wa Dar es salaam zinatiwa doa, tena kwa makusudi na viongozi wa serikali za mitaa wakishirikiana na wananchi wasio na elimu ya mazingira au kwa kukusudia.
Hii inatokana na maeneo ambayo yaliachwa wazi kwa matumizi tofauti na serikali baada ya kupima na kuuza viwanja kwa wananchi kuvamiwa na watu wanaojiita wenyeji na kujenga kiholela katika maeneo hayo mtaa wa Tuangoma. Maeneo ambayo yameathirika na uvamizi huu ni yale yaliyoachwa kama mabonde (valleys), water ponds na cemetaries (makaburi).
Eneo lililoathirika sana na uvamizi huu ni Block 9 nyuma ya Viwanja namba 169 mpaka 195 ambayo yanatambulika kama bonde na makaburi. Tayari wavamizi hao wameshajenga nyumba zaidi ya 5 na wamehamia na familia zao.
Watu hao wanajiita wao ni wenyeji na inaonekana wana baraka za mwenyekiti wa mtaa, kwani mwenyekiti huyo ameonekana akiwa anawaonesha mipaka na kuwagaia maeneo bila kuingilia maeneo ya makazi ya watu ambayo yana beacons.
Wakazi wa maeneo hayo wanapojaribu kupanda miti katika maeneo hayo hung'olewa na mara watu hao huanza kujenga.
MADHARA YA UVAMIZI HUU HATUA ZISIPOCHUKULIWA MAPEMA
Uvamizi huu utapelekea ujenzi holela katika njia za maji na sehemu za maji kutuama yaani ponds na makaburi. Matokeo yake ni serikali na jamii kuingia hasara kama ambavyo inatokea mara kwa mara maeneo ya bonde la msimbazi na maeneo kama hayo na zaidi watu wanye makazi halali kukosa sehemu za kuhifadhi wapendwa wao pale wanapofariki.
Vilevile hali hii ikiachwa kuendelea inaweza kusababisha uvunjifu wa amani siku za usoni, kwani watu hawa wanajenga bila kufuata utaratibu.
Magonjwa ya milipuko inaweza kuibuka wakati wowote kwani nimeshuhudia familia mbili zinaishi katika nyumba walizojenga ambazo hazina choo.