Makonda ameipigia Saluti maiti ya Hayati Magufuli bila sare kama nani?

Benson Mramba

JF-Expert Member
Oct 29, 2013
644
1,482
makonda.jpg

SALUTI
(a) Je, ni nini maana ya kitendo cha kupiga saluti kinachofanywa na askari?
(b) Je, ni askari wa ngazi gani hupigiwa saluti?
(c) Je, ni maafisa/viongozi wa ngazi gani uraiani katika mihimili ya Serikali, Mahakama na Bunge ambao wanastahili kupigiwa saluti?

MAJIBU
(a) Saluti ni salamu ya kijeshi ambayo hutolewa na askari kwa mujibu wa sheria na kanuni za Kudumu za Utendaji wa Jeshi la Polisi (Police General Orders No. 102).

(b) Askari wote kuanzia cheo cha mkaguzi msaidizi na kuendelea hustahili kupigiwa saluti.

(c) PGO namba 200 imeainisha taratibu za saluti kwa viongozi wa Serikali na taasisi zingine kama ifuatavyo:
Askari wa vyeo vyote wanatakiwa kupiga saluti kwa Mheshimiwa Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naJaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mawaziri wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wanapokuwa katika maeneo ya Bunge au Majimboni mwao. (Makofi)

Viongozi wengine wanaostahili kupigiwa saluti ni pamoja na Wakuu wa Mikoa na Majaji wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi. Aidha, kuanzia askari mwenye cheo cha Konstebo hadi Mkaguzi wanapaswa kuwapigia saluti Wakuu wa Wilaya na Waheshimiwa Mahakimu wote wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi. Askari akiwa ndani ya sare anaruhusiwa kuipigia saluti maiti ya kiraia, kijeshi, hata ya mtoto mchanga. KUHUSU KUIPIGIA SALUTI MAITI ni kwamba; Askari wa aina yeyote akiwa ndani ya sare anaruhusiwa kuipigia saluti maiti ya kiraia, kijeshi, hata ya mtoto mchanga ila HARUHUSIWI Askari asiyekuwa ndani ya sare wala Raia wa kawaida kufanya hivyo.
 
Mramba hujui chochote kuhusu Saluti za kijeshi ama kiraia.

Nikusihi tu kaa chini jifunze upya hata wewe utaanza kuzitumia ikikupendeza.

Pole sana kwa maumivu ya moyo
 
Back
Top Bottom