Makonda alikataa kuomba msamaha tukio la kuvamia clouds kwasababu “upande wake haukusikilizwa”, Sasa ni wakati wa kusema!

Rais alifanya kosa kuingilia ile adhabu. DAB alisema upande wake haukusikilizwa, Sasa badala ya kumtumbuwa Nape na kuwashikisha Mikono na Ruge, angetakiwa amwachie upande wake usikike. Kama aliamuwa kumbeba mwanae, basi asingemtumbua Nape.

Sijui ni aina gani ya uongozi hii! DAB anatakiwa aseme upande wake.
Atasemaje wkt nchi nzima iliona CCTV Footage.?
 
Nimesema habari za Makonda kuvamia Clouds ni UPUMBAVU. Niliwahi changia
NAPE NNAUYE ALISTAHILI KUTUMBULIWA?
Habari ndugu zangu,ni jambo lililokuwa limepita lkn kutokana na hili lililotokea limenifikirisha kidogo.

Mtakumbuka mwanzo wa mwezi wa pili makonda alianzisha operation ambayo ilikua VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA. Hii vita ilikua ktk phase tofaut2.ktk phase ya kwanza walitajwa watu wengi wakiwemo na wasanii maarufu. Ktk hii vita ilikuja kuingia shubiri kwa mara ya kwanza baada ya msanii maarufu WEMA SEPETU kutajwa. Hapa tunaona Waziri mwenye dhamana na sanaa na michezo akiingia kati.

Kwa mara ya kwanza anakuja kumpinga kiongoz mwenzie hadharani kuwa ANAHARIBU BRAND ZA WATU kwa kuwataja hadharani,sitaki kuongea conflict of interest kati ya NAPE na wema. Lkn ebu tujiulize nape alikua na uhakika gani kama wanaotajwa hawahusiki na MADAWA YA KULEVYA kiasi cha kudai ANAHARIBU BRAND ZA WATU.

Tufanye nape alikua na uhakika kuwa wanaotajwa sio wenyewe. Nape na makonda ni viongoz wanaofanya kazi ktk serikal moja na nje ya serikal ni chama kimoja.Kulikua na ugumu gani kwa nape kumfuata makonda na kumweleza mkuu au Rafiki yangu kuna 1 2 3 unaonaje ufanye hii ishu kwa mfumo huu na huu?privately!Kuna kitu wanaita collective responsibility.ni mwiko na makosa makubwa sana kwa viongoz wa taasisi au serikal moja kukosoana au kupingana hadharani.

Nape angekua anauelewa wa hii dhana basi madhaifu ya makonda ktk ile operation hata ka alifuatwa na akina wema,bado UWAJIBIKAJI WA PAMOJA ulitakiwa uwe mbele,kuliko naye kuungana kumshambulia kiongoz mwenzie.

Hili jambo linatufundisha hata ktk sehem zetu za kazi mfano shuleni. Academic hawez simama assemble au darasan na kuanza kumkosoa mwalimu wa darasa kwa makosa aliyoyafanya ktk kutimiza wajibu wake. Hata ka wanafunz watatoa malalamiko mbele yako na mwalim wa darasa,wewe kama academic na unajua COLLECTIVE RESPONSIBILITY kuna namna ya kusolve hiyo ishu mbele ya wanafunzi ktk kulinda imani baina ya wanafunzi na mwalim na baada ya hapo wewe na huyo mwalim mnakutana chamber na kupeana makavu. NI MWIKO WAFANYAKAZ KUPEANA MAKAVU MBELE YA WALE MNAOWAONGOZA.

Tufanye hapo nape alitereza. Wakati jpm anaweka jiwe la mcng ubungo,ALISEMA MAKONDA CHAPA KAZI,na before jpm kama mkuu wa serikal tayar alishaonesha kukubaliana na njia na hatua anazotumia makonda ktk KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA. Kwa kauli kama hizi hakukuwa na maana YOYOTE kwa nape kuendelea kupambana na hili swala.

Busara ambayo alitakiwa atumie nape hata ka hakuonesha kukubaliana na msimamo wa mkuu wa serikal na makonda,ilikua ni kuandika barua ya kujiudhuru. HII INGEMPA HESHIMA SANA. Ni Africa tu viongoz hadi watumbuliwe kwakutokuwa na misimamo sawa na wakuu wao kitu ambacho wenzetu wakiona tu kile wanachokipigania hakiwez fanikiwa HUJIUDHURU.

Akiwa bado yuko kwenye conflict na makonda,linaibuka swala la clouds. KWA MAONI YANGU LILE SIO TUKIO LA UVAMIZI. Kuelewa hili lazima urudi nyuma na ujiulize,uhusiano wa clouds na makonda,clouds na ccm na clouds na serikal. Haitaj degree kujua clouds kilikua chombo cha propaganda cha ccm na makonda.Kila propaganda yyt kuhusu makonda ilikua inatangazwa clouds na kupewa uzito mkubwa kuliko stations zozote zile Tanzania na hata mkulu nae utaona favourite station yake ni ipi.Clouds wanajuana vizur na makonda,ilifikia makonda anaingia clouds kuaandaa vipind vyake mwenyewe na hadi clouds wanamwandalia happy birthday. Ni clouds ambako kuna hadi computer ya makonda. Ni clouds ambako makonda anazifaham kolido zote za office. Ni clouds tu ambako makonda alikua akienda muda wwt ule na anawafaham kwa majina wafanyakaz wengi kwa majina.

Kwanini makonda alikua haendi ITV,star tv au channel ten?Nafikiri kuna picha tunapata kuwa makonda na clouds walikua ndugu na si marafiki au mteja na mfanyabiasha wasio na ukaribu wwt ule.Kwa mcng huo ugomvi wa hawa watu wawil inahitaj akili nying sana kuingilia.

Ktk video wanayosema makonda alivamia inaonesha akiingia tu.je cctv zilikuwa mlangoni tu?mbona HATUONI kilichojir huko ndani?Wanadai walipigwa,mmoja wa aliyevamiwa alienda nyumbani kwa makonda kufanya nn baada ya kuvamiwa?Walivamiwa lini na lini walienda kuripoti?

Unavamiwa ijumaa,unaanza kwanza kuangaika na media afu ndo unakimbilia polisi tena baada ya mda mrefu kupita. Hao polisi wanaenda kuchunguza nn?kuna maswal mengi mno.

TUJE KWA NAPE SASA.
Kwa mazingira hayo juu nape kwanini hakutumia hata dk 1 kuona tukio la clouds ni la kipuuz na propaganda?kutokana na kuwa na ugomvi na makonda akaona hapa ndo pakumwangamiza. Lkn je tufanye makonda angekua hana uhusiano wwt na clouds na kweli kavamia na kaaribu vitu.Nape alikua na mamlaka ya kuunda tume ya kumchunguza makonda japo baadae alikuja kukanusha kuwa aliunda tume ya kuchunguza tukio na sio makonda.?tukio lilikuwa likihusiana na maswala ya uharifu. Wazir wa michezo ananafas ya kuunda kamati ya kuchunguza swala la uharifu bila kushirikiana na wizara ya mambo ya ndani ambapo angepata sapoti ya wataalam kutoka jeshi la polisi?

Kamati aliyounda nape ilikua ni sahh?Ukianzia na nape mwenyewe tayar alikosa MORAL AUTHORITY ya kushughulikia ishu ya makonda kama nilivoeleza conflict yao huko nyuma,kamati yenyewe ilikua na baraka za MOAT nafikir chairman wake mnamjua na uhusiano wake na makonda mnaujua. Tuje kwa mwenyekiti wa kamati bwana balile,huyu ni mharr wa gazet la jamhuri ambalo before tukio lilikuja na makala za kumchafua makonda,je Ana MORAL AUTHORITY ya kuongoza kamati?UKITUMIA FE 324 ni simple kuelewa. Mambo ya moral authority na conflict of interest yanahusika sana.

Lkn kamati aliyounda nape je ilikua na wajumbe wenye uzoefu wa kuchunguza tukio lile?I mean wataalam. Utaona kamati ya NAPE ilikua INVALID.

Tuseme huko kote yuko sahh,je nape anauwezo na mamlaka ya kumchunguza au kuunda tume ya kumchunguza makonda?Hawa wote ni wateule wa Rais tena viongoz wakubwa,hata siku moja wazir hawez kuunda kamati ya kumchunguza kiongoz mkubwa tena kwa ngazi ya mkuu wa mkoa.Nape alikua anafanya INSUBORDINATION na dawa yake ni kutumbuliwa tu.Kwa ishu ya makonda mamlaka ya uteuzi ilitakiwa ipewe taarifa na kuna jinsi ya kushughulikia maswala ka haya kwa ngazi kubwa ka za mkuu wa mkoa. Nape alichukulia kama mtu wa kawaida na sio mkuu wa mkoa ndo maana akawatuma akina balile wakamhoji.

Kwa maelezo hayo na upungufu mkubwa aliouonesha nape ktk ishu ya makonda ni halali kutumbuliwa.jpm leo kamaliza kila kitu WAONDOE TOFAUT ZAO WAPIGE KAZI. Sasa tofaut za makonda na ruge wewe unataka kuziundia kamati kweli?HAYA LEO WAMEPATANA ye jpm kala kichwa.

Sijaelezea kwa upande wa siasa kwanini jamaa ilikua ni haki yake atumbuliwe. Nkipata mda ntaelezea hili.

WANANDUGU WAKIGOMBANA CHUKUA JEMBE UKALIME.

SIR TAYLOR

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.

Maneno meengi, lakini hamna cha maana..
Uko full of confidence naona...
 
Atasemaje wkt nchi nzima iliona CCTV Footage.?
Ndo tunataka kusikia, kwasababu alikataa kuomba radhi kwa kiburi kabisa tena baada ya “kupatanishwa” na rais!

Na Ruge aliweka wazi kabisa kuwa ameamuwa kuachana na hiyo issue kwasababu hataki kupingana na rais!

Wengi tulichukulia ile hatua ya rais kama kujaribu kuizima ile issue na kuombea radhi! Lakini kwa maoni yangu, ile move yote ilikuwa ya kinafiki, kwasababu Makoda alibakia na kiburi na vitisho, na rais akamfukuza kazi waziri Nape bila kutumia haki ambayo hata Makonda alisema wazi kuwa hakupewa hiyo nafasi.

Kwa maoni yangu wanachama wa ccm wana haki ya kuhoji hilo bila shaka!
 
Wanajamvi, Hii nchi yetu mambo yake ni kama tamthiliya!

Baada ya kufuatilia kuhusu maisha ya Ruge kutokana na tetesi kuhusiana na kifo chake, pamoja na wale wanaosemekana kuwa “maadui wake”, baada ya Makonda kudai “ana subiri Mungu amwambie cha kusema” kuhusu msiba wa Ruge, niliona nipitie nyuma kuhusu haswa msingi wa ugomvi wao!

Baada ya lile tukio la Makonda kuvamia studios za clouds akiwa na walinzi wa ikulu wakiwa na silaha, jambo lile lilikuwa la kushtusha sana! Kwani nchi zilizopinduliwa, ndiyo huwa vyombo vya habari vinavamiwa na kutangaza “a new order”

Baada ya vutanikivute baina yao, kwakweli Makonda alionyesha kiburi sana. Nilimuelewa Ruge aliposema yeye kama Ruge hana shida na Makonda. Lakini kwasababu yeye ni mkurugenzi wa taasisi hiyo kubwa ya habari nchini, basi alikuwa anawajibika kwa watu wengi na kamwe haikuwa issue ambayo ni personal! Ila Makonda alichukulia personal kwa kila hali!

Kwanza alikataa mapendekezo ya kuomba radhi! Ambapo aliapa kamwe hatoomba radhi hata iweje! Na kwamba sababu ni upande wa pili ambao ni upande wake yeye mvamizi haukusikilizwa! Ndipo nikajiuliza yeye upande wake alikuwa na kipi cha kujitetea? Tena ushahidi wa videos ukiwepo? Kwangu ninaamini Makonda aliongozwa na kiburi! Kwenye ile video clip ambapo TEF walimuita Ruge na Makonda, ambapo Makonda aliweka wazi kabisa kuwa hakutaka Ruge awepo! Alimwambia karibu wa TEF kuwa “hataki kumuona Ruge”, yani hata siyo kusema “hataki kukutana naye”, bali hataki kumuona! Nilishangazwa sana na maneno yale yaliyojaa chuki ya kutisha na kuogofya! Na hilo ni baada ya “kupatanishwa” na rais kule Tanga! Kumbe bado aliondoka na bifu kali kabisa!

Makonda kwenye hiyo press conference baada ya kupatanishwa kule Tanga, alisema kamwe hawezi kuomba msamaha! Na kwamba upande wake haukusikilizwa!

Sasa kwanini Makonda hakupewa hiyo nafasi ya kusema huo upande wake? Sijui kwanini watu hawakuuliza ili tuweze kusikia utetezi wake wa kuvamia studio za clouds usiku? Na kisa ikisemekana kuwa ni kipindi ambacho alitaka kirushwe hewani,ambapo kulikuwepo na tuhuma kuhusu Gwajima kuzaa mtoto wa nje! Kipindi hicho ni wakati ule ambapo rais Maghufuli mwenyewe alisema “I wish I could be IGP, baada ya polisi kuwatizama, pamoja na mengine, wanakwaya wa kanisa la Gwajima wakiimba nje ya kituo cha polisi. Je rais hafahamu kuwa hapo ni sawa na kuzungumza kwa codes?

Wale wakuu wa mafioso ndiyo huzungumza kwa codes! Wanasema jambo kwa kuchukizwa, na anayetajwa ole wake! Hata Trump wa Marekani anashutumiwa kwa jambo hili! Mwanasheria wake na fixer wake ambaye amehukumiwa jela kwa kuidanganya Congress ili kumkinga Trump na kashfa ya kutembea na porn star! ushahidi wa Michael Cohen kwenye Congress alisema hilo! Ni sawa na ile kauli ya rais kuhusu Lissu kuwa msaliti wakati tuko vitani! Kilichofuatia tunafahamu!

Sasa Makonda utetezi wake ni upi huo? Utetezi unaompa kiburi hadi anashindwa kuomba msamaha kwa kosa lilo dhahiri kabisa?! Nina amini kuna siku inakuja haya maswali yatahitaji majibu!

Sishangazwi na yeye kukosa la kusema kwenye msiba wa Ruge. Anasubiri aambiwe na Mungu! Huyo Mungu wake asiye na masamaha? Mwenye kiburi kile wanaita cha uzima?

Makonda upande wako wa pili uliosababisha ukakataa kumuomba msamaha Ruge na clouds ni upi huo?

JF ianzishe tuzo kwa bandiko bora
 
Ila Ruge kilikuwa kichwa. Ametoa maelezo hadi bashite anebaki kupepesa pepesa macho maana maelezo ni very professional

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi niliona hilo! 👍🏽Ila kuna saa alitoa macho kwa hasira, dharau, kebehi na kiburi. Where as Ruge alikuwa calm, cool and collect under pressure!
 
Maskini mtoto wa marehemu aliomba radhi kwa niaba ya baba yake. Lakini Makoda anamtumia Mungu kulinda kiburi chake na ubadhirifu wake!
 
Wanajamvi, Hii nchi yetu mambo yake ni kama tamthiliya!

Baada ya kufuatilia kuhusu maisha ya Ruge kutokana na tetesi kuhusiana na kifo chake, pamoja na wale wanaosemekana kuwa “maadui zake”, baada ya Makonda kudai “ana subiri Mungu amwambie cha kusema” kuhusu msiba wa Ruge, niliona nipitie nyuma kuhusu haswa msingi wa ugomvi wao!

Baada ya lile tukio la Makonda kuvamia studios za clouds usiku akiwa na walinzi wa ikulu wakiwa na silaha, jambo lile lilikuwa la kushtusha sana! Kwani nchi zilizopinduliwa, ndiyo huwa vyombo vya habari vinavamiwa na kutangaza “a new order”

Baada ya vutanikivute baina yao, kwakweli Makonda alionyesha kiburi Cha hatari sana. Nilimuelewa Ruge aliposema yeye kama Ruge hana shida na Makonda. Lakini kwasababu yeye ni mkurugenzi wa taasisi hiyo kubwa ya habari nchini, basi alikuwa anawajibika kwa watu wengi na kamwe haikuwa issue ambayo ni personal! Ila Makonda alichukulia personal kwa kila hali!

Kwanza alikataa mapendekezo ya kuomba radhi! Ambapo aliapa kamwe kuwa hatoomba radhi hata iweje! Na akasema “narudia tena kwa capital letters, SITOOMBA MSAMAHA”. Na kwamba sababu ni upande wa pili ambao ni upande wake yeye mvamizi haukusikilizwa! Ndipo nikajiuliza yeye upande wake alikuwa na kipi cha kujitetea? Tena ushahidi wa videos ukiwepo? Kwangu ninaamini Makonda aliongozwa na kiburi! Kwenye ile video clip ambapo TEF walimuita Ruge na Makonda, ambapo Makonda aliweka wazi kabisa kuwa hakutaka Ruge awepo! Alimwambia katibu wa TEF kuwa “hataki kumuona Ruge”, yani hata siyo kusema “hataki kukutana naye”, bali hataki kumuona! Nilishangazwa sana na maneno yale yaliyojaa chuki ya kutisha na kuogofya! Na hilo ni baada ya “kupatanishwa” na rais kule Tanga! Kumbe bado aliondoka na bifu kali kabisa!

Makonda kwenye hiyo press conference baada ya kupatanishwa kule Tanga, alisema kamwe hawezi kuomba msamaha! Na kwamba upande wake haukusikilizwa!

Sasa kwanini Makonda hakupewa hiyo nafasi ya kusema huo upande wake? Sijui kwanini watu hawakuuliza ili tuweze kusikia utetezi wake wa kuvamia studio za clouds usiku? Na kisa ikisemekana kuwa ni kipindi ambacho alitaka kirushwe hewani,ambapo kulikuwepo na tuhuma kuhusu Gwajima kuzaa mtoto wa nje! Kipindi hicho ni wakati ule ambapo rais Maghufuli mwenyewe alisema “I wish I could be IGP, baada ya polisi kuwatizama, pamoja na wengine, wanakwaya wa kanisa la Gwajima wakiimba nje ya kituo cha polisi. Je rais hafahamu kuwa hapo ni sawa na kuzungumza kwa codes?

Wale wakuu wa mafioso ndiyo huzungumza kwa codes! Wanasema jambo kwa kuchukizwa, na anayetajwa ole wake! Hata Trump wa Marekani anashutumiwa kwa jambo hili! Mwanasheria wake na fixer wake ambaye amehukumiwa jela kwa kuidanganya Congress ili kumkinga Trump na kashfa ya kutembea na mwigizaji maarufu wa filamu za ngono Stormy Daniels! ushahidi wa aliyekuwa mwanasheria wake ndugu Michael Cohen kwenye Congress alisema hilo! Kwamba alizungumzia “in codes” Ni sawa na ile kauli ya rais kuhusu Lissu kuwa msaliti wakati tuko vitani! Kilichofuatia tunafahamu!

Sasa Makonda utetezi wake ni upi huo? Utetezi unaompa kiburi hadi anashindwa kuomba msamaha kwa kosa lilo dhahiri kabisa?! Nina amini kuna siku inakuja haya maswali yatahitaji majibu!

Sishangazwi na yeye kukosa la kusema kwenye msiba wa Ruge. Anasubiri aambiwe na Mungu! Huyo Mungu wake asiye na masamaha? Mwenye kiburi kile wanaita cha uzima? Mtoto wa Ruge aliweza kuwa omba radhi wote baba yake aliowakosea kwa niaba yake. Lakini Makonda yeye anaomba Mungu amaambie cha kusema. Mungu kamwe halindi viburi. Mungu ni misamaha!

Makonda upande wako wa pili uliosababisha ukakataa kumuomba radhi Ruge na clouds ni upi huo?

Makinda is a sniir criminology yaani ni profesa mbobezi wa criminal hapa nchini

Lizaboni
 
J. K. Nyerere aliwahi kuomba radhi kwa aliyotenda ktk awamu yake bila kuombwa au kulazimishwa
Nyerere alikua anasababu nyingi za kutokuomba msamaha kuliko Makonda.
 
Back
Top Bottom