Makonda alichaguliwa na nani kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Taifa Stars ?

Mambo ya mwendawazimu, nduli na dikteta wa Ikulu. Acha tu tubugizwe goli za uhakika.

Nimeona kwenye Gazeti la Mwananchi Ndugu Makonda akitambulishwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Taifa Stars , huku katibu wa Kamati hiyo akitajwa kwa jina la Herisi Said , hivi hii kamati ya hamasa ina majukumu gani na iliteuliwa na nani kwa utaratibu upi ? inakuwaje watu wasio na mchango wowote kwenye soka wakapewa jukumu la uhamasishaji ?

Makonda mtu mwenye bifu kila mahali anawezaje kuwa mhamasishaji wa soka , mchezo ambao hajawahi kuucheza tangu azaliwe ? atamhamasisha nani ? Hakika mikosi ya Taifa stars inaletwa na mengi sana ! mtu aliyeshindwa kukomboa makontena yake ya biashara bandarini atahamasisha nini kwenye soka , mchezo unaohitaji pesa , umoja na mshikamano ?
 
Back
Top Bottom