Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,863
- 5,694
Hatimaye Leo Kamishina mkuu Wa Mamlaka ya kudhibiti madawa ya kulevya nchini amekosoa mtindo aliokuwa akitumia bwana Makonda kutaja watuhumiwa hadharani kuwa haufuati sheria.
Akihojiwa na redio sauti ya ujerumani jioni hii alipo ulizwa swali ni Kwa nini hawakutangaza Majina ya watuhumiwa Wa madawa ya kulevya Kama hapo awali Bwana Rogers Sianga kamishina mkuu alisema hivi.
Kwanza ktk kupambana na madawa ya kulevya ni lazima uzingatie sheria, Kwa kusema hivyo ana maana kuwa Makonda alikuwa anavunja sheria kutangaza watuhumiwa.
Pili akasema hawawezi kumkamata mtu bila kuwa na ushahidi wowote Kwa kuwa wapo wanaotoa taarifa zisizo sahihi na za chuki jambo linalo weza kuleta uonevu Kwa RAIA wema. Lazima wafanye kwanza uchunguzi kabla ya kumkamata au kumhoji mtuhumiwa.
Tunakuunga mkono kamishina Kwa kutumia weledi ktk kupambana na madawa ya kulevya na tupo tayari kukupa ushirikiano kikamilifu ili mradi pawe na uzingatiaji wa sheria ili haki ionekane ikitendeka bila kuonea watu.