Makonda: Acheni kumjadili Lissu. (Je, wakati unamwandikia waraka wa wazi, wewe ulikuwa na matatizo?)

DAB anaweweseka aamini kama chuma kimepona,huko RC Sara anasema serikali ingekuwa imefanya hilo tukio wangekuwa washamuua lissu maana hawawezi askari wao wapoteze risasi zaidi ya 30 bila kuua kweli Awamu hii ya 5 tutashuhudia vihoja vingi sana! yaani kiongozi anatoka hadharani na kutema mashudu namna hiyo,inaonekana sirikali inaua sana watu kwa risasi ndio maana amesema huwa hawakosei wakifanya hayo mambo,anaongea kulingana na uzoefu wao,kitendo cha wasiojulikna kumkosa lissu basi sio sirikali ndio imefanya kama ingefanya sirikali ingekuwa "BESHARA" ishakwisha.
Mie huwa naumia sana kwani huwa naomba Mungu ashuke ili hawa wauwaji hawape kichapo chao hapa hapa duniani sote tukishuhudia ila inashindikana matokeo yake wanaendelea kukejeri, napenda ili liwe funzo hata kwa wanaowaza kuthubutu kuwaumiza watanzania innocent

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani Makonda, the prime suspect, bado ana ujasiri wa kuongelea swala la Lissu. This is very amazing.
 
Huyu katumia lugha ya kebehi ( satirical language)! Kwa wale wataalam wa fasihi, hili lipo wazi mno! Isitoshe, yeye alimwandikia zaidi ya nyaraka nne mtu ambaye hajapona na hakumbuki chochote! Kweli? Inawezekanaje leo amuone Lissu katika angle hiyo ilihali kabla alimuona mzima? Basi ni sawa amejisahihisha, lakini bado kuna mashaka katika andiko lake ambayo mgonjwa anatakiwa kumakinika na siyo abweteke kwa kuwa mwenye hoja kamjudge kuwa bado anaumwa! Na yawezekana mtazamo wake huu ni mkakati no.2 baadaya ule wa kwanza kugoma!
Anasahau kuwa hakuna mwananchi hata mmoja aliyemtuma kumsemea bali akiri kuwa kajituma mwenyewe kwani wananchi walio wengi bado wanamuombea Lissu apone kabisa ili arudi kuwatetea na kuwafundisha!
 
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vingine vya siasa nchini, kuacha kumjadili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kwa kuwa amekiri bado hajapona.

Makonda amesema Lissu ameeleza wazi kuwa daktari wake bado hajamthibitishia kama amepona, hivyo Watanzania wanapaswa kumwacha aendelee na matibabu yake.
“Siridhishwi na mjadala unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini kuhusu Lissu," Makonda alisema alipozungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana.

Makonda alisema kuwa, kama Lissu hajapona, hawezi kurudi nchini kuwashukuru Watanzania na chama chake kilichomchangia fedha za matibabu.

"Nawasihi wanasiasa, vyama vya siasa, hasa chama changu CCM na Watanzania wazalendo, kuacha kumjadili na kumlaumu Lissu kwa sababu yoyote ile kwa sababu ameshathibitisha kuwa bado hajapona vizuri," Makonda alisema.

"Kama mgonjwa hajapona, ni wazi kuwa hawezi kukumbuka chochote, hawezi kurudi nchini kuwashukuru Watanzania na wananchi wake waliokuwa wakimwombea na kumtolea mchango.

"Lakini pia ni wazi kuwa hakumbuki chochote kama alichangiwa na akapatiwa matibabu mjini Dodoma. Hawezi kukumbuka hata maombi aliyofanyiwa na viongozi wa dini."

Alidai kuwa wanasiasa na watu wanaomjadili na kumlaumu Lissu, hawapaswi kufanya hivyo kwa kuwa hana anachokumbuka kuhusu kilichomkuta na badala yake waendelee kumwombea arudi katika hali yake ya kawaida.

Makonda alidai Lissu hawezi kufahamu madhara yanayoipata nchi kwa kile anachokizungumza anapokuwa mataifa mengine kwa kuwa bado hajapona vizuri.

Alidai kuwa Watanzania ambao wataendelea kubishana na mbunge huyo juu ya kile anachozungumza, wataonekana wao ndiyo wenye matatizo.

Makonda aliwataka wanasiasa na wadau wa maendeleo kujikita kujadili masuala ya maendeleo na kuhoji ahadi zilizotolewa na serikali kuhakikisha taifa linapiga hatua kubwa za kukuza uchumi wake.

Alisema kuna miradi mikubwa inayoendelea nchini ikiwamo ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na mradi mkubwa wa kufua umeme (Stiegler's Gorge) ambayo inatakiwa kufuatiliwa kwa karibu na wananchi.

"Wanasiasa na jamii wahoji utekelezaji wa miradi kama hii ya maendeleo badala ya kuendelea kupigia kelele suala Lissu ambaye bado yupo nje ya nchi kwa matibabu,” Makonda alisema.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, Lissu (51), amekuwa nje ya mipaka ya Tanzania akipatiwa matibabu kutokana na kushambuliwa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari lake nyumbani kwake Area D jijini Dodoma Septemba 7, 2017.

Baada ya shambulio hilo, mtaalamu huyo wa sheria alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alikopatiwa matibabu ya awali kisha kuhamishiwa Hospitali ya Nairobi, Kenya na baadaye Ubelgiji.

Hivi karibuni, mbunge huyo alianza ziara kwenye baadhi ya nchi za Ulaya na Amerika na kueleza mambo kadhaa kuhusu tukio la kushambuliwa kwake na yanayoendelea katika siasa za Tanzania.

Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu huyo wa Chadema, ameshaweka wazi kuwa, Februari 20, mwaka huu, anatakiwa kuwa Ubelgiji kwaajili ya upasuaji wa 23 mwilini mwake.

Makonda: Acheni kumjadili Lissu

Je, mheshimiwa Paul Makonda, wakati unaandika WARAKA KWA LISSU, wewe ulikuwa na matatizo?
Makonda anazungumzia mijdala inayoendelea nchini kama nani?
 
Hivi huyu mkuu alishakubali au kukanusha kama alikuwa Dodoma September 7, 2017? Mwenye kufahamu tafadhari.
 
Pengine

Back
Top Bottom