Makonda aanza mipasho na kejeli dhidi ya Ukawa

kiongozi mzuri anaanza kujiongoza mwenyewe kama ameshindwa kudhiti mdomo wake,dahhh hatuna kiongozi hpo(bomu)
 
Huyu jamaa akitaka kuingia kwenye siasa za kuchapa mdomo atajiaribia career yake ,ajifunze kwa Mwigulu ,kabla ya kuwa naibu waziri fedha alikua anatumika vibaya mpaka kuishia kuita watu magaidi ,ameusoma mchezo sasa hivi katulia kimya anasoma ramani
 
WOTE WAFANYE KAZ KUWATUMIKIA WANANCHI bila kuingiliana bali washauriane. tunachotaka maendeleo. mjanja atakayecheza rafu tunaye Dar ndio penyewe.
 
Njaa haina baunsa mjomba .

hakukuwa na umuhimu wa kutaja hayo mambo.
Nchi hii ni ya watu wote, Hayo majigambo hayawezi kutupatia pesa za kureplace MCC.

Tunataka umoja wa kitaifa, Kejeli na Dharau kwa watu waliochaguliwa kwa nguvu ya UMMA sio sawa.
Hizo siasa taifa iliziacha kuanza Oct 2015. Hizi kauli ndio zinatufanya vijana tuonekane Hatuna uwezo wa kazi kubwa.

Vijana wana nafasi kubwa ya kufanya maajabu katika taifa lao kuliko Hata Wazee

Salim Ahmed salim Balozi akiwa na Miaka 22,
JK Nyerere 36 alikuwa waziri baadae 38 rais
Alexander the great alitawala dunia nzima kutoka Ugiriki hadi india kila mahala akiwa na miaka 23
Mfalme Yosia Alikuwa Mfalme akiwa na Miaka 8, lkn busara zake ziliokoa taifa la Yuda.
 
Viongozi wetu kama wanataka mambo yaende vizuri habari ya mipasho ya kivyama waache hadi kipindi cha uchaguzi. Kinachohitajika sasa ni kuwa wamoja ili kufanikisha HAPA KAZI TU!
 
Mwigulu kamrudia Mungu na yupo makini zaidi. Hafanyi mambo ya kipuuzi nimekuwa nafuatilia utendaji wake wa karibuni.Design ya Makonda ni Nape!

Huyu jamaa akitaka kuingia kwenye siasa za kuchapa mdomo atajiaribia carrier yake ,ajifunze kwa Mwigulu ,kabla ya kuwa naibu waziri fedha alikua anatumika vibaya mpaka kuishia kuita watu magaidi ,ameusoma mchezo sasa hivi katulia kimya anasoma ramani
 
Ila kwa sasa mwache aseme najua Mayor sio mtu wa mipasho yeye focus yake ni kuonyesha njia kuinuka kiuchumi Kama mayor yuko kisheria mwache makonda aseme yote yanayomtatiza maana naye binadamu siyo malaika
 
Huyu ni muotaji the dreamer hujui alisemalo wala alitendalo
Hapo ndipo ninapoishangaa serikali ya CCM, kama unaona madiwani na mameya hawana kazi kwanini msifanye mabadiliko kupunguza gharama? Warioba alisema nafasi za mkuu wa wilaya na mkoa ni mzigo tu na kweli leo wanatuonyesha. Mh Rais kunawakati anatuzuga tu kama anania kweli ya kubana matumizi ondoa nafasi za wakuu wa mikoa, punguza majimbo ya ubunge, acha kuongeza wilaya na mikoa kila kukicha.
 
Hivi hii mikoa mipya inatoka wapi sq zetu mraba zinaongezeka ama ndo zile zile za toka kitambo !!
 
Dar es Salaam na mikoa mingine inapata shida ya kutawaliwa na watu immature kama Makonda kutokana na JIPU LA KATIBA. Jipu mama linalokabili nchi hii ni la kukosa katiba ya wananchi. Ingekuweko basi wananchi wangechagua viongozi wao wa kisiasa wa ngazi zote, ikiwa ni pamoja na mkoa. Kwa njia ya uchaguzi, Makonda hangeweza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. He is an imposition on us, and he is acting like the fool that he has always been.
 
Back
Top Bottom