Makonda aanza mipasho na kejeli dhidi ya Ukawa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameanza kutoa kauli za mipasho dhidi ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anaandika Regina Mkonde.

Akizungumza na Umoja wa Vijana Waendesha Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Viwanja vya Leaders Club jijini humo leo, Makonda amesema wapinzani wataishia kuchongwa, na kwamba, mamlaka ya jiji hilo yapo mikononi mwake.

Kauli yake inafanana na iliyotolewa na Said Meck Sadick, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati akikabidhi ofisi hiyo siku chache zilizopita.

Makonda ametoa kauli hiyo siku tatu baada ya Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kutangazia umma kwamba licha ya uanachama wake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), atafanya kazi bila kujali itikadi za vyama vya siasa.

“Mamlaka ya uamuzi ya utendaji kazi Mkoa wa Dar es Salaam yako mikononi mwangu. Wengine wataishia kusema wee,watapiga domo wee, lakini mwenye mamlaka ya mwisho katika uamuzi ni mimi,” alitamba Makonda.

Mimi ndiyo Rais wa Dar es Salaam.Ninayo mamlaka ya kukataa chochote wanachopanga hawa wapinzani; Ni lazima mipango yao yote wailete kwangu na nitaamua kwa maslahi ya wananchi na si vinginevyo; Makonda alizidi kutamba kwa kejeli.

Kauli hiyo ya Makonda ni muendelezo wa mikogo yake dhidi ya UKAWA ambao tayari wameonesha dhamira ya kuachana na migogoro ya kisiasa ili kuhudumia wananchi.

“Msiwe kama baadhi ya viongozi wa waendesha bodaboda wanaofuata wanasiasa na kuwatajia idadi ya wanachama wanaowamiliki ili wapate hela na kutumikishwa kisiasa ili wafanye fujo halafu waanze kusema, serikali haifanyi kitu, haithamini wananchi wake na mambo mengine ya kisiasa,” Makonda aliwaambia bodaboda hao.

Aidha, ametoa maagizo kwa Simon Sirro, Kamanda Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam akimtaka ashughulikie matatizo ya waendesha bodaboda.

“Ndani ya siku 90 kabla ya kupatikana kwa Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Waendesha Bodaboda, nakuagiza Sirro ukawaambie polisi wako waache kuingilia matatizo ya waendesha bodaboda, bali polisi wawe washauri wa shughuli zinazofanywa nao,” amesema.

Makonda ametaja takwimu za ajali na vifo vilivyosababishwa na bodaboda katika Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2015. Takwimu hiyo inaonesha kutokea kwa ajali zaidi ya 1000 na vifo 100.

“Katika Wilaya ya Ilala, ajali zilizotokea ni 486, vifo 34, Temeke 542, vifo 31 na Kinondoni ajali 170 na vifo 36,” amesema.
Daud Laurian, Katibu wa Kamati iliyomaliza muda wake, wakati akisoma risala, amemtaka Makonda kushughulikia baadhi ya wajumbe wa Saccos ya umoja huo (DABOSA) kwa kosa la kufanya ubadhilifu wa fedha zao kiasi cha Sh 50 milioni.

“Tunakuomba Mkuu wa Mkoa Paul Makonda, uwatumbue baadhi ya viongozi wa Saccos yetu ambao wamefuja fedha zetu shilingi milioni 50 kwa manufaa yao binafsi,” amesema Laurian.

Chanzo: MwanaHalisi Online
 
hakukuwa na umuhimu wa kutaja hayo mambo.
Nchi hii ni ya watu wote, Hayo majigambo hayawezi kutupatia pesa za kureplace MCC.

Tunataka umoja wa kitaifa, Kejeli na Dharau kwa watu waliochaguliwa kwa nguvu ya UMMA sio sawa.
Hizo siasa taifa iliziacha kuanza Oct 2015. Hizi kauli ndio zinatufanya vijana tuonekane Hatuna uwezo wa kazi kubwa.

Vijana wana nafasi kubwa ya kufanya maajabu katika taifa lao kuliko Hata Wazee

Salim Ahmed salim Balozi akiwa na Miaka 22,
JK Nyerere 36 alikuwa waziri baadae 38 rais
Alexander the great alitawala dunia nzima kutoka Ugiriki hadi india kila mahala akiwa na miaka 23
Mfalme Yosia Alikuwa Mfalme akiwa na Miaka 8, lkn busara zake ziliokoa taifa la Yuda.
 
PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameanza kutoa kauli za mipasho dhidi ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anaandika Regina Mkonde.

Akizungumza na Umoja wa Vijana Waendesha Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Viwanja vya Leaders Club jijini humo leo, Makonda amesema wapinzani wataishia kuchongwa, na kwamba, mamlaka ya jiji hilo yapo mikononi mwake.

Kauli yake inafanana na iliyotolewa na Said Meck Sadick, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati akikabidhi ofisi hiyo siku chache zilizopita.

Makonda ametoa kauli hiyo siku tatu baada ya Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kutangazia umma kwamba licha ya uanachama wake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), atafanya kazi bila kujali itikadi za vyama vya siasa.

“Mamlaka ya uamuzi ya utendaji kazi Mkoa wa Dar es Salaam yako mikononi mwangu. Wengine wataishia kusema wee,watapiga domo wee, lakini mwenye mamlaka ya mwisho katika uamuzi ni mimi,” alitamba Makonda.

Mimi ndiyo Rais wa Dar es Salaam.Ninayo mamlaka ya kukataa chochote wanachopanga hawa wapinzani; Ni lazima mipango yao yote wailete kwangu na nitaamua kwa maslahi ya wananchi na si vinginevyo; Makonda alizidi kutamba kwa kejeli.

Kauli hiyo ya Makonda ni muendelezo wa mikogo yake dhidi ya UKAWA ambao tayari wameonesha dhamira ya kuachana na migogoro ya kisiasa ili kuhudumia wananchi.

“Msiwe kama baadhi ya viongozi wa waendesha bodaboda wanaofuata wanasiasa na kuwatajia idadi ya wanachama wanaowamiliki ili wapate hela na kutumikishwa kisiasa ili wafanye fujo halafu waanze kusema, serikali haifanyi kitu, haithamini wananchi wake na mambo mengine ya kisiasa,” Makonda aliwaambia bodaboda hao.

Aidha, ametoa maagizo kwa Simon Sirro, Kamanda Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam akimtaka ashughulikie matatizo ya waendesha bodaboda.

“Ndani ya siku 90 kabla ya kupatikana kwa Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Waendesha Bodaboda, nakuagiza Sirro ukawaambie polisi wako waache kuingilia matatizo ya waendesha bodaboda, bali polisi wawe washauri wa shughuli zinazofanywa nao,” amesema.

Makonda ametaja takwimu za ajali na vifo vilivyosababishwa na bodaboda katika Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2015. Takwimu hiyo inaonesha kutokea kwa ajali zaidi ya 1000 na vifo 100.

“Katika Wilaya ya Ilala, ajali zilizotokea ni 486, vifo 34, Temeke 542, vifo 31 na Kinondoni ajali 170 na vifo 36,” amesema.
Daud Laurian, Katibu wa Kamati iliyomaliza muda wake, wakati akisoma risala, amemtaka Makonda kushughulikia baadhi ya wajumbe wa Saccos ya umoja huo (DABOSA) kwa kosa la kufanya ubadhilifu wa fedha zao kiasi cha Sh 50 milioni.

“Tunakuomba Mkuu wa Mkoa Paul Makonda, uwatumbue baadhi ya viongozi wa Saccos yetu ambao wamefuja fedha zetu shilingi milioni 50 kwa manufaa yao binafsi,” amesema Laurian.

Chanzo: MwanaHalisi Online
daah sasa tumekuwa na marais wangapi? akili za viroba bhana hv hata hao viongozi wanaowateua wanatumia criteria zp ? au kuwa mwana nyinyiem yahitaji ujazwe kamasi kichwani
 
Majigambo haya yalikuwa appropriate kwenye serikali ya awamu ya nne sio sasa.ajifunze kutoka kwa boss wake na asome alama za nyakati.He is going back to his old bad days.Aangalie JPM asije akajuta kumteua.
PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameanza kutoa kauli za mipasho dhidi ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anaandika Regina Mkonde.

Akizungumza na Umoja wa Vijana Waendesha Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Viwanja vya Leaders Club jijini humo leo, Makonda amesema wapinzani wataishia kuchongwa, na kwamba, mamlaka ya jiji hilo yapo mikononi mwake.

Kauli yake inafanana na iliyotolewa na Said Meck Sadick, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati akikabidhi ofisi hiyo siku chache zilizopita.

Makonda ametoa kauli hiyo siku tatu baada ya Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kutangazia umma kwamba licha ya uanachama wake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), atafanya kazi bila kujali itikadi za vyama vya siasa.

“Mamlaka ya uamuzi ya utendaji kazi Mkoa wa Dar es Salaam yako mikononi mwangu. Wengine wataishia kusema wee,watapiga domo wee, lakini mwenye mamlaka ya mwisho katika uamuzi ni mimi,” alitamba Makonda.

Mimi ndiyo Rais wa Dar es Salaam.Ninayo mamlaka ya kukataa chochote wanachopanga hawa wapinzani; Ni lazima mipango yao yote wailete kwangu na nitaamua kwa maslahi ya wananchi na si vinginevyo; Makonda alizidi kutamba kwa kejeli.

Kauli hiyo ya Makonda ni muendelezo wa mikogo yake dhidi ya UKAWA ambao tayari wameonesha dhamira ya kuachana na migogoro ya kisiasa ili kuhudumia wananchi.

“Msiwe kama baadhi ya viongozi wa waendesha bodaboda wanaofuata wanasiasa na kuwatajia idadi ya wanachama wanaowamiliki ili wapate hela na kutumikishwa kisiasa ili wafanye fujo halafu waanze kusema, serikali haifanyi kitu, haithamini wananchi wake na mambo mengine ya kisiasa,” Makonda aliwaambia bodaboda hao.

Aidha, ametoa maagizo kwa Simon Sirro, Kamanda Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam akimtaka ashughulikie matatizo ya waendesha bodaboda.

“Ndani ya siku 90 kabla ya kupatikana kwa Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Waendesha Bodaboda, nakuagiza Sirro ukawaambie polisi wako waache kuingilia matatizo ya waendesha bodaboda, bali polisi wawe washauri wa shughuli zinazofanywa nao,” amesema.

Makonda ametaja takwimu za ajali na vifo vilivyosababishwa na bodaboda katika Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2015. Takwimu hiyo inaonesha kutokea kwa ajali zaidi ya 1000 na vifo 100.

“Katika Wilaya ya Ilala, ajali zilizotokea ni 486, vifo 34, Temeke 542, vifo 31 na Kinondoni ajali 170 na vifo 36,” amesema.
Daud Laurian, Katibu wa Kamati iliyomaliza muda wake, wakati akisoma risala, amemtaka Makonda kushughulikia baadhi ya wajumbe wa Saccos ya umoja huo (DABOSA) kwa kosa la kufanya ubadhilifu wa fedha zao kiasi cha Sh 50 milioni.

“Tunakuomba Mkuu wa Mkoa Paul Makonda, uwatumbue baadhi ya viongozi wa Saccos yetu ambao wamefuja fedha zetu shilingi milioni 50 kwa manufaa yao binafsi,” amesema Laurian.

Chanzo: MwanaHalisi Online
 
Huyu ni muotaji the dreamer hujui alisemalo wala alitendalo
Amesema hivi
1. Yeye ndiye mamlaka ya mwisho njiani
2. Polisi wawe washauri wa bodabida
3. Bodaboda wachape kazi wasiwe ngazi ya wanasiasa kwa kupewa vijihela
4. Amemwagiza kananda Siro kuwataka askari wake wasiwabugudhi bodaboda

Sasa ipime kauli yako kwa hoja
 
Alichosema kipo kwenye Thread usidanganye watu
 
Ingekuwa vema akapewa nafasi TOT Taarabu asaidiane na Hadija Kopa kuimba hiyo mipasho itamlipa zaidi ya siasa maana anamfanya aliyemteua huko kwenye nafasi ya siasa adharaulike
 
Amesema hivi
1. Yeye ndiye mamlaka ya mwisho njiani
2. Polisi wawe washauri wa bodabida
3. Bodaboda wachape kazi wasiwe ngazi ya wanasiasa kwa kupewa vijihela
4. Amemwagiza kananda Siro kuwataka askari wake wasiwabugudhi bodaboda

Sasa ipime kauli yako kwa hoja
Kuna hoja ya nguvu na wala sio nguvu ya hoja
 
Back
Top Bottom