Makombora yatua nyumbani kwa Pinda - Askari Wafuta Picha

Wazo la Tume ya Kijeshi naliafiki kabisa na wala TUSILETE WATU JIKONI KWETU kutoka nje ya nchi kwa jina la wachunguzi. Wachunguzi wa kutoka nje wachunguze Dowans lakini MASWALA YETU YA KIJESHI WASIGUSE HATA KIDOGOOO!!!
 
GHILIBA ZA SERIKALI KUTAFUTA VISINGIZIO KUTANGAZA HALI YA HATARI
KUUA MOTO WA KUDAI TATIBA NCHINI HAIKUBALIKI


Hii dhana inayojitokeza hivi sasa kwamba kuna mtu mmoja Tanzania nzina (kwa jina la Dr Mbura) kuona kitu cha ajabu angani mda mfupi kablaa mabomu kuanza kulipuka Gongolamboto na sasa kudeshesha wazo kwamba huenda tulishambuliwa kutoka nje ya nchi yote niwazo la hatari sana na yakemewe sana na wapenzi wa demokrasia nchini.

Ni wazi kwamba pindi mawazo ya ajabu ajabu na kauli za KINAJIMU HIZI zote ni katika KUTAFUTIA SERIKALI KISINGIZIO CHA SERIKALI YA KIKWETE KUTANGAZA HALI YA HATARI ili kuua moto wa kudai KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI zote kupitia bungeni.

Wa-Tanzania tuamke na tuangalie sana hizi ghiliba wakati wananchi wenzetu wanapotezeshwa uhai hivi!! Tukumbuke haya yote yanatokea wiki moja tu tangu Lowassa kupewa uwenyekiti wa kamati hiyo bungeni, tukiwa katikati ya moto wa kudai katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na hatua dhidi ya mafisadi.

Hakuna aliyetarajia huyu bwana kupewa kiti nyeti kiasi hicho kwa taifa letu mbali na shutuma lukuki shingoni mwake!!
 
Habari ipo kwenye gazeti la MWananchi na nisingependa kuirudia yote ila nachotaka kusaidia hao waandishi ni kwamba:-
KUNA NAMNA YA KURUDISHA PICHA ZILIZOFUTWA ZOTE........ Wala wasiogope hao Askari akili kichwani hakuna,,, wanadhani ukifuta kitu ndio kinaondoka? Kama waandishi wako interested nitawapa means za kuweza kurecover hizo pictures unless hiyo Memory Card ya Camera imeingizwa kwenye Sulphuric Acid
 
Of course they are interested!!!! Ndo maana wakazipiga hizo picha... Mkubwa ikiwezekana hebu wasiliana nao uwasaidie. We need to see those pics.
 
Kwa nini wamefuta hizo picha? Ina maana hawataki ionekane kwamba na wakubwa nao wa wameathirika? Kwa hiyo wanataka walala hoi ndo waonekane wameathirika. Kama vipi waandishi wasusie kufanya kazi na jeshi la polisi.
 
What is a medical doctor doing in the ministry of defense anyways? Halafu tunasema hatuna madaktari, afukuzwe aende hospitali ya mnazi mmoja unguja, tunahitaji waganga huku ati?

Off course we need doctors, but they have right to lead any ministry like any other Tanzanian, however, the problem here is accountability and not being a doc.
 
Wakuu mimi sijasoma hilo gazeti, nini kimetokea? Yani bomu limetua kwa pinda? Then what happened?
 
kwa hali hii, mean kwa mabomu ya Mbagala na Gongo la mboto Tanzania haina tofauti na mabomu yale yaliyotokea japan 1945, na kwa mwendo huu tutegemee makubwa zaid ya vifo. Kwa wajawazito ni hatari zaidi, tutegemee watoto waaina yake na dhaifu, walemavu na wenye utindio wa ubongo. Binafsi naamin licha ya kubomoa makazi ya watu, kuuwa, kujeruhi, naamin sumu iliyotoka Itakuwa na madhara makubwa kwa wananchi na wakazi wa maeneo hayo na tutegemee madhara makubwa zaidi ya hayo!
 
hili jeshi lina matatizo ina maana hao wakubwa ni soo wao kukumbwa na majanga kama haya ila raia wa kawaida wanachukulia poa?
 
Inawezekana hawajadhulika kwa sababu mabomu sijuhi makombora yanaruka juu na mrushaji si lazima aumie. Kwa hiyo kwa kuwa wao walikuwa kwenye point of departure wamepona majirani wa mbali ndo yamewaangukia

Ndugu wanaJF kua kitu kinanishangaza, hivi katika milipuko ya mabomu Gongo la Mboto hakuna wanajeshi aliojeruhiwa na kufa? Mbona hatuambiwi?
 
Laana ya udanganyifu bungeni, halafu anajiona mshua. Ongea yake tu hisia za kisharobaro
 
Hitler wa Ujerumani alikuwa na bunkers za zege ambazo zilikuwa bomb proof. Jee mbinu hiyo haiwezi kutumika kuhifadhi mabomu ya jeshi letu - na hasa kama wanadhani ni lazima yabaki mijini?
 
Ndugu zangu wana wa jamiiForums, baada ya tukio la mlipuko wa mabomu Gongolamboto kutokea nilitarajia kuwa tutakuwa tumepoteza maisha ya askari wetu wengi saana. Lakini cha ajabu saana hadi hii leo tuna ambiwa kuwa hakuna askari au mwanafamilia wa askari yeyote wa pale yalipolipuka mabomu alikufa. Kwangu mimi taarifa kama hii inanifanya nijiulize maswali mengi saana ambayo yote yanaishia kwenye swali kuu KWA NINI HAWAKUFA??? Je ni MIUJIZA GANI ILITOKEA??? Maswali kama hayo najiuliza baada ya kuangalia scenarios kama hizi zifuatazo:
1) Kambi ya Gongolamboto ndio lilipo Ghala kuu la JWTZ, hivyo ni kambi kubwa na yenye maeneo mengi nyeti yanayohitaji ulinzi muda mwingi kama sio wakati wote. Kwa tuliopitia JKT tunajua kuwa angalau kila lindo huwa halikosi askari kama wawili hivi. Hivyo ukiwa na malindo kama kumi tu, utakuwa na askari 20 walioko zamu. Ina maana pamoja na kuwa haikuwa siku ya kazi lakini kulikuwa na askari kama 20 hivi wakiwa malindoni hadi hapo milipuko inatokea. Malindo hayo ni pamoja na hayo maghala yaliyolipuka. Je hawa askari wote walipona kweli????

2) Kambini pale tunaambiwa kuna mahanga au mabweni mawili ya askari wasiooa au kuolewa, ambao kwa uchache tuseme ni kama 20 wanaume na 20 wanawake. Kwa muda kama ule wa jioni wengi wao tunategemea walikuwa ndani ya mahanga au walikuwa mesini wakipata chakula cha jioni, hawa nao hakuna hata mmoja aliyepigwa na bomu???? Tunaambiwa haya mahanga yamepigwa na kuharibiwa kabisa kiasi kuwa hata kijiko hakipatikani.

3) Kambini pia kuna nyumba za askari waliooa au kuolewa na wenye familia zao kama watoto na wazazi wao watu wazima. Pamoja na kuwa tunaambiwa kuwa askari wote wamepata mafunzo ya nini cha kufanya hatari kama ile inapotokea, yawezekana ni ukweli, na sina ubishi juu ya hilo. Ila napata wasiwasi kidogo napojiuliza je na hao watoto wao na hao wazazi wao nao je wamepitia hayo mafunzo kweli??? Kama bomu limepiga na kuharibu kabisa nyumba kama mbili za hao askari ambazo kila moja ilikuwa na kama familia nne hivi kweli hakuna aliyeuawa???

Kama mabomu yaliweza kuharibu kabisa vifaa kama magari yote yaliyokuwapo karibu, na pia yakaweza kuwaua raia waliokuwa jirani na kambi pamoja na wengine waliokuwa mbali iweje kweli yashindwe kuua hata askari mmoja???? Hapa ndio panapopelekea baadhi yetu kujiuliza saana na kusema KWANINI??? NI AJALI KWELI AU KUNA WATU WALIJUA KABLA NA WAKAJIHAMI???? Ndio maana tulihitaji saana mjadala ufanywe ndani ya bunge kwanza juu ya hili suala
 
Back
Top Bottom