Makombora yatua nyumbani kwa Pinda - Askari Wafuta Picha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makombora yatua nyumbani kwa Pinda - Askari Wafuta Picha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, Feb 18, 2011.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Ndugu wanaJF kua kitu kinanishangaza, hivi katika milipuko ya mabomu Gongo la Mboto hakuna wanajeshi aliojeruhiwa na kufa? Mbona hatuambiwi?
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Eti wao wanajua kuyakwepa!!!!
   
 3. Katibukata

  Katibukata Senior Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wanajeshi = watanzania = watu
  Upo hapo?
   
 4. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Ni siri za jeshi hizo. usipende kuzichimbua
   
 5. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  mara zote hesabu znazohusisha askari hukokotoa kati ya raia na askari.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hawajataja kwa kuchambua..Lakini kwa akili ya kawaida tu utajua kuwa wanajeshi wengi sana wamekufa eneo la kambi.
  After all nyumba 70% zinazozunguka kambi ni za wajeshi, so you can just measure the magnitude of destruction to their families.
   
 7. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika taarifa zote zinazotolewa na vyombo vya habari kutokana na uvumbuzi wao ama kutoka kwenye vyombo husika kama jeshini na serikalini (Hotuba ya Mkwere) zote zinabeba ujumbe kwamba HAKUNA HATA MWANAJESHI MMOJA ALIYEPOTEZA MAISHA kutokana na milipuko ya Mabomu ya Gongo la Mboto.

  Huu ni Uongo wa Makusudi kabisa, naweza nisivisontee mkono vyombo vya habari moja kwa moja kutokana na ugumu ambao vitakuwa vinapambana nao katika jitihada zao za kupata habari kuhusiana na Uzembe wa Jeshi na Serikali.

  Mkwere lazima amepata taarifa zalizo sahihi na hivyo amekubaliana na Jeshi kuficha ukweli.

  Kwa haraka haraka tu, Je inawezekana watu ambao kwa uzembe kabisa Mabomu, yaliyo kwenye makazi yao yanaripuka bila mpangalio maalumu WAKAWA NA UELEWA WA KUEPUSHA MAISHA YAO NA HATARI INAYOBEBWA NA MILIPUKO YA MABOMU kwa umakini wa asilimia mia moja? Eti wanajeshi wakike, bweni lao limeharibiwa kabisa kabisa, na kila kitu kilichokuwa katika bweni lao kimeharibika kabisa kabisa lakini wao woooote wako salama salimini!!!!!

  Katika kambi ya Jeshi ya Gongo la Mboto, kuna familia za wanajeshi zinaishi pale, zooote ziko salama salimini!!!!! kweli Mkwere, Mwinyi na Nahodha inawezekana kweli?

  Bahati nzuri, njia ya Muongo ni fupi, Katika Hotuba ya Mkwere ametoa maelezo haya "Baraza la Usalama limetoa pole nyingi kwa mkuu wa Majeshi, Maofisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa MAAFA MAKUBWA YALIYOWAKUTA NA HASARA WALIYOIPATA KWA MILIPUKO...".

  Taarifa aliyotaka kuilazimisha Mkwere ni kwamba kilichotokea Jeshini Gongo la Mboto ni uharibifu wa MALI Pekee, katika hili angekuwa consistent kama angetoa pole kwa Hasara waliyoipata, lakini dhamira ya walioandaa hotuba hii na Mkwere mwenyewe imewasuta na kuwalazimisha kukiri kwamba wanajeshi wamekufa pia, NDIO MAANA AMETOA POLE KWA MAAFA MAKUBWA YALIYOWAKUTA, Maafa haina tofauti na msiba, Maafa ni Msiba mkubwa sana, ni neno linalotumika pale haraiki ya watu wanapopoteza maisha, kama ilivyotokea kwa wanajeshi na raia Gongo la Mboto Jeshini.

  Waliopoteza ni ndugu zetu, ni kaka zetu, ni dada zetu, baba, mama, shangazi, wajomba, wakwe, ni rafiki na maswahiba zetu hata mkificha misiba yao tutapata taarifa tu, mjue mnachokifanya ni kusogeza msiba mbele.

  Jakaya utuambie Ndugu zetu wanajeshi na familia zao wamekufa wangapi. Tunataka tulie sasa tumalize, tunamachozi sasa, tuache watanganyika tulie mkwere
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WANANCHI HATUKO SALAMA TENA NA MALI ZETU, KIIO KILA LEO NA MAYATIMA
  KUONGEZEKA HIVYO SERIKALI NZIMA IJIUZULU HATA KABLA YA MAANDAMANO
  YA KUTETEA 'UHAI WA WENZETU' KUANZA KOTE NCHINI


  Mheshimiwa Kikwete kama amiri jeshi mkuu ajiuzulu pamoja na serikali yake.

  Jukumu la msingi halijazingatiwa; wananchi hatuko salama!! Tusianze kuzungusha kiswahili hapa ni uhai umepotea kwa uzembe!!! Hawa mayatima wanahitaji sauti zetu!!

  Hatutaki tena tume kwa hata kule Mbagala chombo kama hicho hakikutusaidia zaidi ya kuwapa wanasiasa na makampuni ya kibiashara kujinadi kwenye kioo cha televisheni mgongoni mwa msiba na damu kwa wengine.

  Jukumu la kwanza la kuhitajika uwepo wa serikali katikati yetu NI KUHAKIKISHA USALAMA KILA MMOJA WETU NA MALI ZETU. Kwa mtaji hizi picha nilizoona, serikali nzima ya CCM ijiuzulu mara moja

  Mauaji Arusha walitupuuza kana kwamba kuliuaua nzi tu. Kule kwenye mashamba ya mpunga wala hawakujishughulisha kitu kuwajibika mtu. Sasa kama kweli kuna JAMBO AMBALO KIUKWELI KABISA KINATUHITAJI KUANDAMANA MPAKA KUELEWEKE NI KATIKA KUTETEA UHAI WA WENZETU.

  Kama tutaona vifo hivi kama vile ni ya 'akina wale' na kwamba sisi wengine hatuhusiki basi hapo ndipo kiama chetu kinapoanzia. Kwa vifo hivi vyote 17 taifa tumepata yatima wangapiii?????????????
   
 9. C

  Codecola Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kufikia hitimisho haraka namna hii wengine tunapata wasiwasi, the motive behind andiko lako. Mimi nikuulize kama umeweza kuandika haya yote kwani usipate ushahidi hata wa mwanajeshi mmoja aliyekufa? Hawa wanajeshi wana ndugu, misiba yao lazima itawaguza na ndugu zao. Sasa unataka tuamini kuwa kunamwanajeshi amekufa ndugu zao na waliohudhuria msiba wake wote wafungwe mdomo na serikali wasiseme? Kwanini mbagala waseme kuwa wanajeshi wamekufa na gongolamboto waamue kuwa kimya? Wewe unataka tuamini kuwa wanajeshi wanaweza kukubali vifo vya wenzao viweze kutumika kwa maslahi ya mtu au kikundi cha watu? Pengine unaweza kuwafanya watu wengine kukuamini lakini sio mimi.
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,777
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  ..haijalishi kama wanajeshi wamekufa ama la.

  ..kuna raia wa kawaida ambao wamepoteza maisha, viungo,na mali.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Kuna wanajeshi zaidi ya 4 wamepoteza maisha. Ngoja niendelee na intelijensia yangu nitakuja na majina kabisa. Kuna malalamiko ya ufanyaji kazi katika mazingira magumu hasa kwa sakari wa vyeo vya chini. Kifupi ni uzembe tu ndicho kilichopelekea maafa hayo.
   
 12. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hii serikali bwana ni kichekesho kabisa,
  nilikuwa naongea na Mwananjeshi mmoja ananiembia kuwa hayo mabomu mengiu yalikuwa ni ya mwaka 1971,1972..etc
  inasemekana walikuwa wakipewa pesa kila mwaka kununua mapya na vifaa vingine jamaa wanaweka kibindoni na kuthaminisha hayo yaliyo expire.
  Ni uwazi usiopingika kuwa wanajeshi woye walijua kuwa hayo mabomu yangeweza kulipuka mda wowote
  hivyo si ajabu wote wakawa wameshakimbia nyumba zao kabla ya mlipuko
  wasingeweza kutoa taarifa kwa wannchi kwani waliogopa kujulikana kuwa walijua litatokea na kwa nini walishindwa kuyazuia mapema?
  Hivyo hilo lilijulikana, na kama hawajafa ..inawezekana kabisa ikawa hivyo
  Hata jamaa yangu kanieleza kuwa hakuna mwanjeshi hata mmoja aliyekufa( unless kama ameniingiza mjini kwa hilo):usa2:
   
 13. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hii serikali bwana ni kichekesho kabisa,
  nilikuwa naongea na Mwananjeshi mmoja ananiembia kuwa hayo mabomu mengiu yalikuwa ni ya mwaka 1971,1972..etc
  inasemekana walikuwa wakipewa pesa kila mwaka kununua mapya na vifaa vingine jamaa wanaweka kibindoni na kuthaminisha hayo yaliyo expire.
  Ni uwazi usiopingika kuwa wanajeshi woye walijua kuwa hayo mabomu yangeweza kulipuka mda wowote
  hivyo si ajabu wote wakawa wameshakimbia nyumba zao kabla ya mlipuko
  wasingeweza kutoa taarifa kwa wannchi kwani waliogopa kujulikana kuwa walijua litatokea na kwa nini walishindwa kuyazuia mapema?
  Hivyo hilo lilijulikana, na kama hawajafa ..inawezekana kabisa ikawa hivyo
  Hata jamaa yangu kanieleza kuwa hakuna mwanjeshi hata mmoja aliyekufa( unless kama ameniingiza mjini kwa hilo):usa2:
   
 14. C

  Codecola Member

  #14
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hii post inatulazimisha tuamini wanajeshi wamekufa pia, hata bila ya kutoa ushahidi usio na mashaka, si dhani hii ndio njia tunayotaka kwenda nayo, hakuna sababu ya kuulea uzembe huu wa kufikiria eti ni mwanajamii mwenzetu.
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mtumishi wa mungu Masa na wengine: Inawezekana kabisa kuwa hakuna mwanajeshi hata mmoja aliyekufa na hiyo inawezekana tu kama yafuatayo ni sahihi.

  1. Wanajeshi kama watunza silaha na watu waliokuwa karibu kabisa na mlipuko siku ya tukio hawakuwa wanalinda maghala hayo

  2. Wanajeshi walikuwa na perfect information juu ya ulipukaji wa mabomu hayo, yaani siku, saa na mahala patakapolipuka mabomu hayo

  3. Kwa kuwa wanajeshi wao wamefundishwa mbinu za kujilinda na mabomu vitani haswa pale yanapolengwa kwao basi ni dhahiri kuwa wanajeshi walichukua tahadhari ya kujilinda na mabomu hayo hata kabla hayajalipuka vinginevyo yangewakuta kama wenzao wa Mbagala ambao hawakuwa na taarifa rasmi ya ujio wa milipuko

  4. Wanajeshi walipoona yanakaribia kulipuka wakaamua kuingia kwenye mahandaki yao yaliyozagaa kambini na kuyaacha mabomu yalipuke mpaka yatakapotulia ndipo wakatoka na kutangaza wameyadhibiti.

  Kama hayo yote hapo juu ndivyo ilivyokuwa basi ni dhahiri mlipuko huu ulikuwa ni wa makusudi na wenye lengo la kuwadhuru wananchi wasio na hatia ili kutimiza malengo fulani, kwa definition ya kuua raia wasio na hatia kwa malengo ya kisiasa, huu unastahili kuitwa ni UGAIDI japo si wakujitoa muhanga. Vinginevyo ni lazima out of control milipuko ianze na kudhuru from the source kabla ya kule yatakapotua mabomu hayo kama ni perimeter ya 10 kilometer au below.
   
 16. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Jamanii kuna habari za kiintelijensia zinasema jeshi lilishakuwa tayari kwa milipuko dalili zilishaanza kuonekana tangu saa 5 asubuhi....waliwapigia simu wastaafu wa vyeo juu...woote wanaokaa ukonga na gmboto kuwa waondoke.....kuna mstaafu mmj ambae ame pooza anaishi ukonga aliondoka saa 9,,.....,wanajeshi walishajiandaaa wakawa on high alert hajafa hata mmj....walijua...fanyeni utafiti
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WANANCHI HATUKO SALAMA TENA WALA MALI ZETU, KIIO KILA LEO NA MAYATIMA KUONGEZEKA: KWA HILI SERIKALI NZIMA IJIUZULU HATA KABLA YA MAANDAMANO
  YA KUTETEA 'UHAI WA WENZETU' KUANZA KOTE NCHINI


  Mheshimiwa Kikwete kama amiri jeshi mkuu ajiuzulu pamoja na serikali yake.

  Yalianza na vifo vya raia kule (1) Pemba, baadaye (2) Unguja, Kisha (3) Mbagala, nako Arusha Mjini, (4) mauaji ya wakulima kule Mashamba ya mpunga kule Mabuki Mbeya na sasa (5) Gongolamboto.

  Ajabu ni kwamba licha ya wananchi wengi kuuaua na mali zao kuteketea, hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kuwajibika wala kuwajibishwa serikalini. Kote ni kiburi na jeuri tu mbe ya kupotea uhai wa mtu na watoto kubaki miyatima!!!

  Jukumu la msingi halijazingatiwa; kuna watu wanasinzia kwenye majukumu nyeti na sasa kutugharimu kiasi hini, wananchi hatuko salama!! Tusianze kuzungusha kiswahili hapa ni uhai umepotea kwa uzembe!!! Hawa mayatima wanahitaji sauti zetu!!

  Hatutaki tena tume kwani hata kule Mbagala chombo kama hicho hakikutusaidia zaidi ya kuwapa wanasiasa na makampuni ya kibiashara kujinadi kwenye kioo cha televisheni mgongoni mwa msiba na damu kwa wengine.

  Jukumu la kwanza la kuhitajika uwepo wa serikali katikati yetu NI KUHAKIKISHA USALAMA KILA MMOJA WETU NA MALI ZETU. Kwa mtaji hizi picha nilizoona, serikali nzima ya CCM ijiuzulu mara moja

  Mauaji Arusha walitupuuza kana kwamba kuliuaua nzi tu. Kule kwenye mashamba ya mpunga wala hawakujishughulisha kitu kuwajibika mtu. Sasa kama kweli kuna JAMBO AMBALO KIUKWELI KABISA KINATUHITAJI KUANDAMANA MPAKA KUELEWEKE NI KATIKA KUTETEA UHAI WA WENZETU.

  Kama tutaona vifo hivi kama vile ni ya 'akina wale' na kwamba sisi wengine hatuhusiki basi hapo ndipo kiama chetu kinapoanzia. Kwa vifo hivi vyote 17 taifa tumepata yatima wangapiii?????????????


  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  Debris and arms were hurled across the Tanzanian of city of Dar es Salaam on Wednesday night after an accident triggered a series of explosions at Gongola Mboto military base.
  [​IMG]Tanzania's Red Cross says about 200 children who lost their parents during the confusion of the blasts are being cared for at the city's stadium.

  [​IMG]


  [​IMG]
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kw matukio mbalimbali nchini bila hata mtu mmoja kuwajibika katika historia ya nchi yetu, ukiachilia mbali tu hadithi tunazosimuliwa Mzee Mwinyi huko nyuma, ni kashfa kubwa KUDHIHIRISHA JINSI TUSIVYO NA THAMANI kwa watawala.

  Wao wakiugua tu mafua au chunusi mara utasikia kapelekwa Afrika Kusini, Ulaya, India mara sijui wapi huko. Tujue ukimya wetu ni USALITI MKUBWA WATOTO YATIMA KAMA HOA KWENYE PICHA JUU, NI USALITI KWA WAFU WETU na kamwe hawatatusamehe tukiendelea hivyo na usaliti huu.

  Hivi vijitoto yatima vingekua vinajua ni kitu gani kinaendelea hivi sasa wala wasingetusalimia huko mahospitalini walikolazwa na kilema cha maisha huyu mwili wa mzazi ukisubiri kwenda kuzikwa.

  Tunataka kuona watu wakiwajibika haraka hapa, na wala si jambo la utani mtu kupoteza uhai. Kwingineko huko duniani, kifo cha mtu mmoja tu chaweza kupotezesha watu wengi sana kazi zao lakini sisi hapa ni kana kwamba kafa inzi tu na watu kuendelea tu kupindisha kiswahili.
   
 19. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Wandugu kuna taarifa za kiintelijesi zinazosema kwamba kambi ilijuwa
  Kuwa mabomu yangelipuka wakati wowote tangu mwaka jana.waliomba serikali fedha za kuangamiza
  Mabomu hayo na serikali ikadai haina fedha.kwa hilo jeshi lilijiandaa kwa lolote.
  Na mabomu ya namna hiyo yapo kila kambi hivyo tutegemee mengine yatakuja kama
  Jitihada za makusudi za kuyangamiza.jk anajua na ameamua kuficha ukweli
   
 20. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama Watagoma kujiuzulu, Basi Tuwashitaki kwa Kesi ya Kuua Watanzania Wenzetu.
   
Loading...