EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema Serikali ya CCM imeshindwa kazi hivyo haifai kuwa madarakani wala kuongezewa wabunge kwa kuwa itazidi kuwadidimiza wananchi.
Alisema haiwezekani rais wa awamu ya nne apelekwe London kupimwa na kununuliwa suti halafu aweze kuwasimamia wananchi wenye matatizo mengi.
Eti Msemaji wa Ikulu anakanusha ukweli..., hii ni aibu kwa taifa, alidai Mbowe na kuongeza:
Nchi inauzwa watu wanapewa suti hii ni mbaya, amekuwa akienda Marekani na akirudi anasema amekwenda huko kuwaona wakubwa watusaide neti..., wametuletea vyandarua hivyo tuvitumie kwa umakini , alibeza Mbowe.
Alisema hii ni aibu kubwa kwa nchi ya Tanzania kuomba mgawo wa neti, wakati rasilimali zilizopo nchini zinaweza kutatua tatizo hilo la malaria.
Source: Mwananchi