Kwa miaka ya hivi karibuni hususani siku za sherehe za kitaifa tumeshuhudia makomandoo wakionyesha mambo mbalimbali ambayo hayana tofauti sana na miaka ya nyuma yalikuwa yakionyeshwa na vikundi vya maigizo vya sarakasi na karate na wanafunzi wa shule za msingi, sekondari au vikundi vya sanaa vya mtaani.
Je, kwanini miaka hii maonyesho au maigizo hayo yanafanywa na jeshi hususani kitengo cha makomandoo? Je, inaleta picha gani komandoo kufanya maonyesho ambayo hata watoto wa shule za msingi au nursery schools wanafanya? Je, mtoto wa shule ya msingi ambaye anaweza kufanya maonyesho kama hayo atajisikiaje au atalionaje jeshi letu hususani makomandoo kufanya maonyesho ambayo yeye anaweza?
Je, maonyesho kama hayo yanapofanywa na makomaandoo wetu yanatoa taswira gani kwa mataifa mengine wanapoona?