Makofi mengi kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Bungeni yanaashiria nini?

stephen4440

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
901
1,000
Leo alipotajwa Mhe. Kassim Majaliwa Kassim Bungeni, alipigiwa makofi mengi sana tofauti na wenzake.

Kwa mtazamo wangu kwa wiki hizi kadhaa Waziri huyu mkuu amekosha nyoyo za watanzania wengi na ameonekana kukubalika sana.

Huenda KMK akawa ndiye Rais ajaye wa JMT.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,633
2,000
Majaliwa ni jembe. Kuna katuni moja nakumbuka ya Kipanya anasema tunataka rais ambaye atakuwa na haiba katikati ya Magufuli na Kikwete.

Nadhani rais huyo ni Majaliwa. Jamaa ni nusu uMagufuli nusu uJk.
Kama ni jembe si mlipeleke shambani kwenu likalime? Hana sifa ya kuitwa Rais, kama ilivyokuwa kwa magufuli.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,390
2,000
Majaliwa ni jembe. Kuna katuni moja nakumbuka ya Kipanya anasema tunataka rais ambaye atakuwa na haiba katikati ya Magufuli na Kikwete.

Nadhani rais huyo ni Majaliwa. Jamaa ni nusu uMagufuli nusu uJk.
Alifanya kosa kubwa sana kulidanganya taifa

Ila all in all anaweza kuwa rais bora maana hana makandokando ya ufisadi.
 

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,819
2,000
Namkubali sana Majaliwa hasa baada ya kifo cha Magufuli! Ameonyesha msimamo na sio mnafki!
Baada ya kifo niliona amekimbilia kufanya ziara kwenye bwawa la umeme alijuwa tayari kuna mafisadi wanataka kulikwamisha!
Sio yule aliyesema “awamu iliyopita ilikuwa ya ajabu sana”!
Wasiwasi wangu wataanza kumchafua!
Pia Ummy mwalimu anafaa sana!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom