Makinikia ya Tani 7 za dhahabu kwa mwezi

Mzee wa Usafi

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
644
292
Baada ya vumbi la Kamati Teule ya Mheshimiwa Rais kuanza kutulia ningeomba kudadavua namba za Kamati hiyo kwa makini zaidi ili tujiridhishe zaidi.

Ukichukuwa kwa namba za wastani, wastani wa dhahabu kwa kila kontena ni kilo 28.
kuna makontena 277 yaliyozuiwa sehemu mbalimbali.
Baada ya kadhia hii kujitokeza uongozi wa Acacia ulitoa kipeperushi kuonesha mchanganuo mzima wa jinsi makinikia na dhahabu ya "tofali" inavyo patikana. katika kipeperushi hicho, Acacia wameeleza makinikia yana wastani wa asilimia 50 ya dhahabu inayo zalishwa kutoka kwenye migodi yake ya Bulyanhulu na Buzwagi. Hivyo asilimia 50 nyingine ni "vitofali".
Acacia pia wametueleza hayo makontena 277 ni uzalishaji wa mwezi mmoja tu. Hivyo kufuatana na hesabu za Kamati teule dhahabu ya migodi hiyo miwili kwa mwaka inatakiwa kuwa ifuatavyo

28kg x 277 x12(miezi) x 2=186,144kg
kilo 186,144 ni sawa na gramu 186,144,000
Na kwa kuwa kipimo cha dhahabu kinafuata matakwa ya Wamarekani ambacho ni Troy Ounce (wakia) basi tubadirishe uzalishaji wa mwaka mzima katika kipimo hicho
186,144,000/31.1034
Hii ni sawa na wakia 5,984,683.35 Oz

Hiki ni kiasi kikubwa mno kuzalishwa na Migodi miwili na sijawahi ona mgodi Dunia wa kuweza kuzalisha kwa mwaka hata robo ya hiyo dhahabu.
Mgodi mkubwa sana Dunia kupita yote ni Grasberg mine upo nchini Indonesia unawezo wa kuzalisha gramu 58,474,392 za dhahabu. Huu mgodi una wafanyakazi zaidi ya 19,000

Kitu kingine ambacho bado natafuta kukifahamu ni pale Kamati ilipo sema kuna madini ya chuma ambayo hajaripotiwa.

Duniani kote chuma huchibwa na kuchenjuliwa kutoka kwenye Oxide minerals kama hematite, goethite, magnetite na mengine. Hakuna mgodi wowote Duniani unao chenjua chuma ya kutoka kwenye Sulphides...Sasa kwanini kamati ili amua kuweka na chuma na yenyewe inaweza chimbwa kwa faida...mimi sijui!!!!

Suala la madini gani yaechenjuliwe au la linatokana na mashapo ya mgodi husika, na Financial model yake kama madini hajafanyiwa modelling ina maana hayawezi chenjuliwa kwa faida....Sasa kwanini kamati ilingiza REE rare earth elements ambazo kikawaida zina kuwa gangue minerals?

Jioni Njema
 
Kuna watu watakuja pata aibu kubwa sana....ni swala la muda tu.
Hata mm naliona hilo ukizingatia kwamba ma Professor waliokuwa kwenye kamati ya madini wana nadharia nyingi ukilinganisha na hali halisi.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
~~>>Ndio maana Lisu alisema ule utafiti wao ni Uchafu......... Ila Sizonje kwakuwa ana akili ndogo aliwaamini na kuamua kumtumbua Muhongo kwa "data" za kutengeneza

Sent using Nokia toch......
 
Back
Top Bottom