Makinikia ya kutongozea demu.

eddy brown

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
413
310
*Sasa hivi ukitaka kupiga sound demu unatumia maneno haya yanayokwenda na wakati*


vita ya kutazama uzuri wako haijawahi kuziacha hisia zangu salama . nipe makinikia ya moyo wako. Naahidi kulipa mirahaba yako na kodi zote za mapenzi. Sitakudanganya kiwango cha madini kilichoko kwenye mchanga wa madini ya mapenzi kama acacia. Please usizuie contena la mchanga wa madini ya penzi langu kwenye bandari ya moyo wako, usiniundie kamati za marafiki zako kufanya uchunguzi wa makanikia ya upendo wangu
usinitangaze kuwa naiba utajiri wa mgodi wa moyo wako hadharini mbele ya vyombo vya habari, nitakufata hata kwa private jet kama raisi wa Barick nitakuomba tukae kwenye meza ya mazungumzo ili uniruhusu kuchimba sukari ya moyo wako. Usiwahusishe viongozi wastaafu ma X wako katika katika ombi langu sababu wengine watakuwa walikusainisha mikataba mibovu ikakuumiza na wengine wamepumzika baada ya kazi kubwa ya kulijenga taifa la moyo wako....
 
Nikiwa form three kuna kijana aliniandikia barua ya mapenzi, nikawa ninapiga story na shost kumbe na yeye aliandikiwa barua na mtu yule yule tulicheka sana kubwa zaidi alikopi maneno yale yale..
Kumbe nawe uwa unatongozwa duuu vijana wanamoyo


Swissme
 
Nikiwa form three kuna kijana aliniandikia barua ya mapenzi, nikawa ninapiga story na shost kumbe na yeye aliandikiwa barua na mtu yule yule tulicheka sana kubwa zaidi alikopi maneno yale yale..
Mlimkubalia?
 
Kumbe nawe uwa unatongozwa duuu vijana wanamoyo


Swissme

Mtafute binadamu asiye na moyo tumuweke kwenye Guinness book of records

Maana naamini kuwa uzuri wa mwanamke ni kauli zake sasa najaribu kufikiria kauli zako ni mbaya sana yaweza kuwa unafanana nazo


Swissme

Uzuri uko kwenye macho ya mtazamaji

Asubuhi njema na huyo aliyepotea njia bye.



Swissme

Kama ulivyopotea wewe
Dah mmenichekesha sana
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom