Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,053
- 4,499
Mchanga aka makinikia aka magwangala ni makombo yatokanayo na shughuli ya uvunaji (extraction) ya tofali za dhahabu. Na kawaida ya makombo tajiri huwa aidha anayatupa jalalani na masikini au scavengers wengine wanaweza kupatamo ridhiki.
Na hiki ndicho tulichoaminishiwa tangu awali. Kuwa hayana thamani ya maana. Yalikuwa hayalipiwi hata hiyo royality fee hadi kipindi cha awamu ya nne, baada ya kuona yanasafirishwa sana nchi za nje, kampuni ilibanwa kuyalipia pia royalty hiyo ya 4% of gross value kama inayolipwa kwa tofali za dhahabu wanayosafirsha.
Kampuni imetudanganya hiyo gross value ya makinikia hayo. Kampuni inapinga hiyo scientific analysis ya watalaamu wetu. Hili sina tatizo nalo maana jibu lake litapatikana kwa njia za kisayansi (scientific methodology). Hili tuwaachie wanasayansi wenyewe. Sisi halituhusu kwa sasa.
Kampuni imedanganya uzito wa mchanga uliomo kwenye hayo makontena. Hili halihitaji ubobezi wa kisayansi. Yaani u declare kwamba ni tani 20 wakati ni tani 23. Yaani tani 3 nzima ukosee kuzipima! Na kwa nini usikosee ukasema ni tani 17 ili hizo tani tatu zile kwako? Yaani hiyo mizani yako ina macho ya kukosea tu kwa manufaa tu ya upande wako? Siku za mwizi ni arobaini. Kuna uwezekano mkubwa kuwa containers hizo zilikuwa na mchanga wa tani 20 wakati zinafungwa mbele ya mawakala wetu wa TMAA.
Baadaye zilifunguliwa na kutumbukiziwa miche ya dhahabu ya tani tatu au mbili ndani ya kila container na kufungwa tena kwa nakili hizo hizo. Kulikuwa na tempering ya hizo containers kama watu wanavyo temper na mita za TANESCO.
Walifanya hivyo wakijua scanner zetu pale bandarini ni za low quality zisizo na uwezo wa mionzi yake ku penetrate huo mchanga kuona kilichofunikwa ndani ya mchanga. Bahati nzuri kwetu na mbaya kwao, baada ya kitendo hicho walisahau kupunguza mchanga wa kiasi kinacholingana uzito na kile walichokichomekea ili uztito ubaki ule ule wa tani 20. Au walijua pale bandarini kwetu aidha tuna mazezeta au wana watu wao hapo bandarini wanaowalipa mlungula. Tofauti ni kubwa sana. Tani tatu nzima za dhahabu kila container! Ingekuwa angalao kilo 100 tungesema ni normal standard deviation ya mizani, kitu ambacho ni nadra kutokea. Hawakuridhika hiyo angalao kilo 100 ambayo tungeweza kuwasamehe au kumezea.
Wametudanganya. Inabidi tupate haraka scanner ya uwezo wa kuona kinachoweza kuwa kimechomekewa kwenye hayo makontainer yaliyozidi uzito. Makontena hayo yaliyopitiliza uzito kamwe yasiruhusiwe kuondoka nchini. Kwanza yametuharibia barabara zetu, na sijui kwanini maofisa wetu wa mizani barabarani waliyaruhusu kupita (rushwa, uzembe kila mahali). La sivyo tukishindwa kupata scanner sahihi haraka, basi mchanga huo umwagwe na kuchambuliwa wote manually ili tujilidhishe na hicho kilichomo cha tani tatu kila container.
Kama wameweza kutudanganya kwenye haya makombo ambayo kwa muungwana alipaswa kutuachia bure ili nasi angalau tunukie dhahabu badala ya kupelekea nduguze ulaya, watashindwaje kuwa walikuwa wanatudanganya kwenye gross value ya tofali za dhahabu wanazochuma. Ni lazima sasa baada ya uchunguzi wa makombo tukachunguze chakula chenyewe. Nadhani huko tutazimia kabisa na wengine wanaweza hata poteza maisha kwa blood pressure na adrenaline hyper secretion!!!
Tukisha thibitisha kuwepo kwa cheating wa kiwango cho chote kisichovumilika, tutakuwa na halali ya kuvunja mkataba nao. Mkataba wa pande mbili hata kama ni strict kiasi gani, kama upande mmoja unakuwa danganyifu, ni halali kuuvunja. Hata kwenye ndoa ambazo pande mbili zimeapa hadi kifo kiwatenganishe, upande mmoja ukishuhudiwa unafanya udanganyifu wa mchepuko, ndoa hiyo lazima invunjikae. Hawa wanandoa wenzetu ACACIA wamekuwa wanafanya michepuko na tumeishuhudia red handed. Ndoa yetu hii sasa basi, lazima ivunjike. Tuwewashika red handed wakifanya mchepuko, arbitration court yo yote duniani itatuelewa na wala hatutakiwi kuwa na wasi wasi maana tayari tuna ushahidi wa kutosha. Tuendelee kutafuta ushahidi zaidi ili tukawagandamize kabisa mwanayu.
Hata kama mkataba ungekuwa mzuri kiasi gani, hususani kugawana nusu kwa nusu hiyo thamani ghafi (gross value), kama mwenzako kwa sababu yuko jikoni, zikipatikana kilo 100, anaficha kilo 40 na kukuambia kuwa mwezi huu tumepata kilo 60. Hivyo wewe unapata kilo 30 kumbe mwenzako kachukua kilo 70. Si mwaminifu. Ukija kugundua lazima mtavunja mkataba huo na kugawana mbao. Wala hakuna mahakama yo yote itakayosema kwamba sisi ni haki yetu kudanganywa. Na sidhani katika mkataba huo kuna kipengele kinachowapa haki ACASIA kutudanganya wapendavyo. Waliouona huo mkataba watujuze kama kuna kipengele cha hivyo. Wengi wetu hatujauona huo mkataba ila tumeambiwa tu kwamba ni mbovu sana.
Hicho ndicho kinachoelekea ACACIA walikuwa wanatufanyia. Tusubiri zile kamati zingine zitapata nini zaidi kuhusu sakata hili. Tutoe constructive ideas zitakazotuwezesha kushinda hiyo kesi ya kuvunja mkataba na hawa jamaa kwenye hizo mahakama za mataifa. Tusijenge ideas za kutukatisha tamaa kwamba haiwezekani kushinda kesi hii kwenye mahakama hizo.
Kwamba mkataba huu ni wa milele, lije jua ije mwezi hatuwezi kuuvunja bila ya kuadhibiwa vikali na nchi za ulaya na marekani (kuwekewa economic embargo kama Zimbambwe walivyo fanywa). Yaani madini yetu lazima yaendelee kuchukuliwa bure tutake tusitake.