Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,649
- 119,257
Wanabodi,
Kwenye hii kadhia ya makinikia ya dhahabu, kuna swali kuhusu mchango wa Vyombo vya Habari katika kuwahabarisha na kuwaelimisha Watanzania kuhusu kadhia hii, jee vifukue makaburi ya kutafuta chanzo kilichotufikisha hapa, au kuendelea kujikita kwenye kushangaa tuu matokeo ya kuwa tunaibiwa baada ya rais Magufuli kuzuia kusafirishwa kwa mchanga wa makinikia ya dhahabu as if ndio tumeanza kuibiwa leo, badala ya kujikita kubaini chanzo, kilichopelekea sisi kuibiwa, jee tumefikaje hapa?.
Kama ni kuibiwa hatujaanza kuibiwa leo na hiki kilichoibuliwa na Tume ya Magufuli sio kipya na sio chanzo bali ni matokeo tuu, kwa nini leo tunajadili matokeo, badala ya kujadili chanzo? . Tume ya Bomani iliishabaini tunaibiwa, kuna ripoti ya kitaalamu ya Alex Stewart Asseyers nao walibaini na serikali ikaelezwa na kufanywa siri!. Kwa nini vyombo vya habari vya Tanzania, havitaki kuwajulisha Watanzania chanzo kilichopelekea sisi kuibiwa na kufikishwa hapa tulipofikia, na badala yake watu wanajadili matokeo.
Hoja hizi zimeibuliwa kwa kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa na Star TV live Jumamosi asubuhi.
Washiriki ni mwandishi Kennedy Nation, na mhadhiri wa SAUT Mlakiri Kopoka, chini ya usimamizi wa nguli Dotto Emmanuel Bolendu.
Endelea kufuatilia with hoja ya msingi in your mind, jee yaliyopita sii ndwele, tusifukue makaburi ya chanzo cha kuibiwa huku na waliotufikisha hapa, bali tujadili tuu matokeo tuu baada ya kugundua tunaibiwa, tufanye nini tusiendelee kuibiwa?.
Paskali.