Makinda: Wabunge msiwe kama watu wa Kariakoo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda: Wabunge msiwe kama watu wa Kariakoo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Jun 14, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Makinda: Wabunge msiwe kama watu wa Kariakoo
  Je ni sahihi kwa Spika wa Bunge kutumia mfano wa Wajasiriamalim wa Kariakoo kama watu wasiokuwa na Ustaarabu na mipango katika kujadili mambo kama walivyokuwa wabunge hapo jana katika kuchangia Mpango wa Maendeleo 2011/12 - 2015/2016.

  Katika hali isiyokuwa ya kawaida hapo jana Jioni wabunge walitawaliwa na miongozo ya mara kwa mara hali ambayo iliamsha hisia na mkanganyiko wa mabo wakati mwingine huku MIC nyingi mjengoni zikiwa ON na sauti za lugha za vijembe zikisikika LIVE.

  Hatua hii ya Spika inafuatia utaratibu mzuri alioutumia asubuhi hii Mh. mbowe ya Kuuliza muungozo baada ya kipindi cha Maswali na majibu kukamilika

  Mh Mbowe aliomba kupewa Muongozo kufuatia Majibu ya Naibu Waziri ambayo alisema alidanganya katika ufafanuzi wake kuhusu mkataba wa Uwanja wa Ndege wa KIA

  Spika: Kamuomba Mh. Mbowe alete maelezo yake kwa maandishi ili kuomba ufafanuzi zaidi

  Na ndipo Mama akakumbushia sekeseke la jana kuwa utaratibu wa kuomba muongozo wa Spika unatakiwa kufanyika kama alivyofanya leo MH.MBOWE

  Hivyo amewaomba Wabunge wasijidharau na kuwa kama watu wa Kariakoo

  anasema hakuwa hata na hamu ya kuangalia kupitia luninga hapo jana kwa jinsi wabunge walivyobehave jioni

  Source: Maswali na Majibu Bungeni asubuhi hii kupitia STAR TV​
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  She needs Communication Skills; Kwa mtu kama yeye sio busara kutoa statement zinazoweza kuwa portrayed kama kashfa au looking down on people,

  Tena mimi ningependa wawe kama watu wa Kariakoo kwa kupata mishahara midogo na kutiwa posho, ili wawe kama watanzania wenzao
   
 3. e

  emalau JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,177
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 180
  hii tabia ya kudharau watu wa kariakoo haijaanza leo, hata Makamba aliwahi kutoa statement kama hiyo, nawashangaa watu wa kariakoo uchaguzi ukija CCM inapata kura nyingi kariakoo !
   
 4. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi kariakoo kuna wapiga kura wachache sana, ehe?

  By the way, kama watu wa kariakoo sio wastaarabu basi nina msahihisha mh speaker "Jamani wabunge wanzangu wa ccm, msiwe kama watu wa kariakoo ..."

  lol
   
 5. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Walikwisha watumia October 2010, hawana kazi nao tena kwa sasa.
   
 6. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndio shukrani zao kwa wapiga kura, tunawapa nafasi watuongeze then wanatudharau, hii ni sawa na kumtukana mwajiri wako.
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  bibi kiroboto anasomeka “hana heshima kwa jamii ya watanzania” atambue anaichoma nyumba anayoishi huku akiwa ndani yake. moto usipomuua utamjeruhi, kama kweli ni msomi ayaelewe na maneno haya.
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mjadala haukwenda vizuri jana jioni baada ya idadi kubwa ya wabunge kutoka nje ya mjadala na kuanza kukandia vyama vingine vya siasa wakiongozwa na Hon. Dr. Augustino Mrema
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,297
  Trophy Points: 280
  Reference ya kariakoo sijaipenda, tunaomba Spika aliombe radhi bunge kwa kauli hii.
   
 10. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Amesahau kuwa hao anaowadharau ni tunda la uongozi wa CCM kwa miaka 50 sasa. Nao kwa jinsi wsivyoelewa, watawapa kura 2015. Ni juzi tu kwenye uchaguzi walidanganywa wameendelea sana chini ya CCM wakaichagua.
   
 11. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wewe na Makinda mmeanza sasa kuchokoza watu wa kariakoo. Shauri yenu
   
 12. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Huyu Anne Makinda kwanza akafungue barabara yetu inayounganisha Kijitonyama na Sinza badala ya kututukana sisi walalahoi wa Kariakoo.

  Hana busara kabisa na hasitahili kuwa kiongozi, ndiyo maana amefikia hatua ya kutufunga barabara yetu ili tuendelee kutaabika. Kama hututaki basi atuuwe wote tuwaachie nchi nyinyi wastaarabu waheshimiwa wabunge!
   
 13. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Du! kejeli kweli hii..si bora angewaambia anaomba ukimya kuliko hiyo kauli..
   
 14. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kaishaomba radhi lakini msemo huo si wa leo tu. msemo huo umekua ni sehemu ya msamiati wa lugha yetu mahala pengi hapa Tz. Sokoni popote pale kila mtu anasimamia maelezo yake kwa taratibu anazozikubali yeye mwenyewe - ndio kukolea kwa ufanisi wa shughuli ziendeleazo hapo. Bunge sio sokoni. wabunge jana walikuwa kama wako sokoni wakinadisha bidhaa na hiyo si mahala pake.
   
 15. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Kaomba radhi kijanja, kakwepa kwamba hakuwasema watu wa Kariakoo bali utaratibu wa kuongea bila mpangilio uliopo kariakoo.
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Ameomba radhi??
   
 17. k

  kiyeyeu Member

  #17
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  alishawah kuzomewa pale kariakoo na nilishuhudia, ilikuwa jumapili asubuh akiwa ktk v8 nyeusi,
   
 18. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Namsamehe bure baada ya kuona CV yake. Akichoka atawaachia wenye uwezo
   
 19. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 880
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80

  Oh hoh!

  Unamaanisha wanawafanya kama dawa ya penzi?
   
 20. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #20
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wanawake wakiwezeshwa wanaweza, lakini huyu sijui vipi kila siku anaharibu.
   
Loading...