Makinda: Waandishi wa habari wanapotosha suala la Posho

Hii serikali ya magamba inabidi iondolewe nadarakani mapema sana.Jk na wenzake wanabidi wapewe azabu kali sana wakitoka madarakani ili iwe fundisho .

Turudi kwenye hoja ya huyu mama.Huyu mama ana matatizo sana,kwa minajili hii amewaharibiwa wanawake sana katika swala la uongozi.Hastahili hata kuwa mwenyekiti wa kitongoji.Alaaniwe kwa ufedhuli anaowafanyia watanzania kwa kuwafanya majuha.
 
I hate this contempt of the people. HIvi kweli anafikiria kuna mtu anayefikiria wabunge wanalipwa posho kwa siku 365 au mmoja wa watu wake ndio wamemuambia "unajua wananchi wanafikiria mnalipwa kwa siku 365"? Ni sawasawa na wale ambo walikuja kutuelewesha kuwa ule "mswada wa sheria ya mapitio ya Katiba siyo Katiba yenyewe kwani wapo watu wanafikiria ndio katiba yenyewe"? Unajua kuna mtu anaweza kulewa akawa chakari; lakini kuna wengine wanalewa wanakuwa bwii! hawa wamelewa bwii!

Ugimbi wa madaraka!
 
Yaani huyu ni ziro full!!!Kwa hiyo anaona ni sawa wao kulipwa posho wakiwa Bungeni?
Kwa hiyo kila ofisi ya serikali wafanyakazi wakikutana kwenye vikao kujadili issue mbalimbali nao walipwe? Mfano,vikao vya walimu,madaktari,nk?

Hana SABABU za msingi kabisa!!!
 
Unajua kuna mtu anaweza kulewa akawa chakari; lakini kuna wengine wanalewa wanakuwa bwii! hawa wamelewa bwii!

Ugimbi wa madaraka!

Mpaka wanaanza kutenda mambo ya aibu na ajabu mbele ya umma. Sawa na mlevi anaelewa na kuanza kuropoka yeye ni tajiri sana huku akitukana wahudumu na wateja waliomzunguka hapo klabuni.
 
Spika wa Bunge Mh.Anna Makinda leo alikutana na waandishi wa habari baada ya kuahirisha Bunge kutolea ufafanuzi suala la posho na tamko la serikali bungeni kuhusu mgomo wa madaktari.

Katika mkutano huo, Spika kadai kwamba watanzania wengi wanadhani wabunge hulipwa posho za kila siku kwa siku zote 365 za mwaka, jambo ambalo si kweli. Posho hizo hutolewa pale tu wanapokua na mikutano ya bungeni Dodoma.

Spika pia kafafanua kwa nini Serikali haijatoa tamko lolote kuhusu mgomo wa Madaktari bungeni. Kwa maelezo yake, Spika anaeleza kwamba tamko hilo ni lazima liandaliwe kwa maandishi, wabunge wote wagawiwe na kulipitia kabla ya kusomwa rasmi. Mchakato wa kuliandaa bado unaendea wizara ya afya na baada ya wabunge kugawiwa tamko hilo litajadiliwa.

Source: Taarifa ya habari TBC saa 2 usiku.

Hivi tuna kiongozi hapo?

Yaani kama mganga anapiga ramli, kanatisha sana...
 
Gazeti la mwananchi lina mlengo wa chadema ndio maana hata likiharibu mambo linatetewa sana na wafuasi wa chama hicho hapa JF
 
Yaani huyu ni ziro full!!!Kwa hiyo anaona ni sawa wao kulipwa posho wakiwa Bungeni?
Kwa hiyo kila ofisi ya serikali wafanyakazi wakikutana kwenye vikao kujadili issue mbalimbali nao walipwe? Mfano,vikao vya walimu,madaktari,nk?

Hana SABABU za msingi kabisa!!!

Lakini angalau katuondolea shaka na mtazamo wa wengine ambao tulidhani wanalipwa posho mwaka mzima. presha imeshuka kidogo
 
Wananchi wanafahamu kwamba posho ya kukaa inalipwa wabunge wanapokuwa wanahudhuria vikao vya bunge, hakuna mwananchi anayesema kwamba wanalipwa posho ya sh.330,000 kwa siku katika siku zote za mwaka.
Hapa ametengeneza habari mpya na kuwatupia waandishi wa habari kwa lengo la kukwepa hoja ya msingi na kuleta kitu kipya tena cha hovyo.

Alichopaswa kuwaambia wananchi ni kwa uhalali gani wabunge wameamua kujipandishia posho kwa 186% bila kuzingatia hali za wananchi, huduma za jamii zinadorora pamoja na wananchi wengi kupinga ongezeko hilo.

Kwanini anaibeba serikali kwa mbereko ya chuma hata ktk dharura ambapo wananchi wanapoteza maisha kwa uzembe na ubabe wa serikali?

Hapa ndipo nataka kuanza kumchukia huyu bibi kiboroto.
 
Hana SABABU za msingi kabisa!!!

Kabisa. Hoja yake kuu ilikua ni kupanda kwa gharama za maisha hapa Dodoma (hususani gharama za malazi). Mfano,yeye Makinda na wabunge wengine ambao ni viongozi waandamizi wa serikali wanaishi katika nyumba za bure! Hizo gharama za malazi wanazijua kweli? Pia kuna wabunge ambao wanadoea nyumba za wazazi wao,Lusinde,kina Kawawa wanaishi kwenye nyumba za wazazi wao! Gharama za malazi wanazijua kweli?!

Yaani kauli za huyu mama zimepelekea gharama za maisha hapa Dodoma kupanda kikweli kweli sasa. Nyanya hazikamatiki,kisado kilichokua kinauzwa tsh. 2500 hadi 3000 sasa ni tsh. 6000 hadi 7000! Nyanya moja sasa ni tsh. 200! Tsh. 10000 soko la majengo haina thamani kabisa;soko ambalo walala hoi na walala hai wanapigana vikumbo,huku walala hoi wakiuma na kuzidi kulala hoi!
 
Spika wa Bunge Mh.Anna Makinda leo alikutana na waandishi wa habari baada ya kuahirisha Bunge kutolea ufafanuzi suala la posho na tamko la serikali bungeni kuhusu mgomo wa madaktari.

Katika mkutano huo, Spika kadai kwamba watanzania wengi wanadhani wabunge hulipwa posho za kila siku kwa siku zote 365 za mwaka, jambo ambalo si kweli. Posho hizo hutolewa pale tu wanapokua na mikutano ya bungeni Dodoma.

Spika pia kafafanua kwa nini Serikali haijatoa tamko lolote kuhusu mgomo wa Madaktari bungeni. Kwa maelezo yake, Spika anaeleza kwamba tamko hilo ni lazima liandaliwe kwa maandishi, wabunge wote wagawiwe na kulipitia kabla ya kusomwa rasmi. Mchakato wa kuliandaa bado unaendea wizara ya afya na baada ya wabunge kugawiwa tamko hilo litajadiliwa.

Source: Taarifa ya habari TBC saa 2 usiku.

Hivi tuna kiongozi hapo?

....Ili uweze kumuelewa huyu spika wetu.
anza mazoezi hapa halafu ndo baadae ujitahidi kumuelewa. ...English iko gumu bana.... - Global Publishers
 
huko Ikulu sielewi wanakanusha nini wakati Rais ni kweli ametia saini kubariki posho hizo na wabunge wamekwishawekewa kwenye accounts zao!
utakuwa wewe ndio lile gazeti la mwananchi unatetea hoja yako punguza udaku
 
Spika wa Bunge Mh.Anna Makinda leo alikutana na waandishi wa habari baada ya kuahirisha Bunge kutolea ufafanuzi suala la posho na tamko la serikali bungeni kuhusu mgomo wa madaktari.

Katika mkutano huo, Spika kadai kwamba watanzania wengi wanadhani wabunge hulipwa posho za kila siku kwa siku zote 365 za mwaka, jambo ambalo si kweli. Posho hizo hutolewa pale tu wanapokua na mikutano ya bungeni Dodoma.

Spika pia kafafanua kwa nini Serikali haijatoa tamko lolote kuhusu mgomo wa Madaktari bungeni. Kwa maelezo yake, Spika anaeleza kwamba tamko hilo ni lazima liandaliwe kwa maandishi, wabunge wote wagawiwe na kulipitia kabla ya kusomwa rasmi. Mchakato wa kuliandaa bado unaendea wizara ya afya na baada ya wabunge kugawiwa tamko hilo litajadiliwa.

Source: Taarifa ya habari TBC saa 2 usiku.

Hivi tuna kiongozi hapo?
Hapo spika anapotosha mada. Swala ni kupinga posho za kukaa kitako, hapa kila mtu anaelewa maana ya posho hizo kuwa mtu analipwa kwa kuhudhuria vikao na sio siku zote ktk mwaka. Hata hivyo kwa maana hiyo hiyo ya posho bado zinapingwa vikali kwa sababu ugumu wa maisha ktk mji wa dodoma si kwa wabunge pekee bali kwa kila mtu aliyepo hapo kuanzia wabunge, wauguzi, waalimu, wanafunzi, wakulima mpaka hata polisi. kwa hiyo hamna mantiki ya kuongeza posho kwa wabunge ukaacha watu wengine.
 
Wabunge wakiwa Dodoma wanalipwa Per diem! Hii ndiyo stahili halali ya kufanya kazi yao waliyoajiriwa nje ya vituo vyao vya kazi. Hii posho ya kukaa (Sitting allowance) ni kwa ajili ya kazi gani nyingine zaidi ya waliyotumwa na kulipwa per diem? Mimi ni mtumishi wa serikali hiyo hiyo, nikitumwa kufanya kazi nje ya kituo changu cha kazi nalipwa per diem na nauli ya kwenda na kurudi huko kwenye kazi. Hata kama nitakalia viti 20 kwa kazi niliyotumwa, silipwi posho ya kukalia viti hivyo. Iweje Wabunge walipwe kwa kukaa wakati ndiyo kazi yao waliyotumwa? Au wanataka wafanye kazi waliyotumwa wakiwa wamesimama? Nadhani sasa wabunge waamue moja, ama walipwe per diem au posho ya kukaa. Haiwezekani walipwe mara mbili kwa kazi moja.
 
Sijawahi kuona mwanamke mwenye roho mbaya na ngumu kama huyu Spika Makinda..kazi kuvaa manywele ya bandia tu
 
Back
Top Bottom