Makinda: Waandishi wa habari wanapotosha suala la Posho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda: Waandishi wa habari wanapotosha suala la Posho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MachoMakavu, Jan 31, 2012.

 1. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Spika wa Bunge Mh.Anna Makinda leo alikutana na waandishi wa habari baada ya kuahirisha Bunge kutolea ufafanuzi suala la posho na tamko la serikali bungeni kuhusu mgomo wa madaktari.

  Katika mkutano huo, Spika kadai kwamba watanzania wengi wanadhani wabunge hulipwa posho za kila siku kwa siku zote 365 za mwaka, jambo ambalo si kweli. Posho hizo hutolewa pale tu wanapokua na mikutano ya bungeni Dodoma.

  Spika pia kafafanua kwa nini Serikali haijatoa tamko lolote kuhusu mgomo wa Madaktari bungeni. Kwa maelezo yake, Spika anaeleza kwamba tamko hilo ni lazima liandaliwe kwa maandishi, wabunge wote wagawiwe na kulipitia kabla ya kusomwa rasmi. Mchakato wa kuliandaa bado unaendea wizara ya afya na baada ya wabunge kugawiwa tamko hilo litajadiliwa.

  Source: Taarifa ya habari TBC saa 2 usiku.

  Hivi tuna kiongozi hapo?
   
 2. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu mama ana watoto?? Mume wake nani vile?
   
 3. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,798
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mimi hata sijui hii ni laana au nini??

  Yani sasahivi kila jambo ambalo serikali italifanya au kuamua linatuacho hoi Wananchi.

  Viongozi wanapojifunga vibwebwe na kutolea ufafanuzi katika hizo sintofaham, Wananchi ndio tunazidi kubaki midomo wazi na kuchanganyikiwa zaidi. Wakati mwingine naona bora wakae kimya japo nayo haisaidii....

  Nimejitahidi kuelewa hii serikali pamoja na shutuma kibao zinazo ibuliwa, nimekua navuta subra nikiaamini kuna viongozi makini na watakuja na ufafanuzi ulionyooka lakini kila wanapoibuka ndio nazidi kuchoka kabisa. Hapo hajazungumza Raisi wao, yeye ndio huwa anavuruga mambo kabisa. Hebu nyie wazee wenye busara mliotengwa na hii serikali hovyo jitokezeni muiongoze nchi hii inaangamia kwa kweli. Wapi Salim Ahmed Salim? Wapi walioba? Mzee Malicela uko wapi baba? Jamani mambo huku ni vuruvuru JK nchi imemshinda jamani...

  Lowasa uko makini lakini ukimya wako unatutia shaka (huenda kweli ni fisadi)
  Sita umepoteza muelekeo(hasira zako za kukosa uspika zimekupoteza, ungetulia ungejijengea heshima sana) otherwise ungeweza kusaidia.

  Dah...niko Hoiii....!
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  yani nikikutana mahali popote na huyu mama ntamkata mtama mpaka apae juu ya bati.
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kwa maana nyingine ni kwamba wananchi tunapaswa kuridhika wabunge walipe hz posho kwani ni ndgo tu kutokana na siku wanazokuwa na vikao vya bunge.
   
 6. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hivi hawa viongozi wetu wanajua emergence, au hawajui kama mgomo wa madaktari ni emergence kwa taifa? Wamekaa wanakula kuku wakati watu wanakufa wanasema tamko linaandikwa!! Hahahaha! Perhaps para moja then wanaenda kula mpaka kesho.
   
 7. a

  abdalah Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Matamko mangapi ya sirikali hutolewa bila vikao vya bunge
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  huyu mama ni cchp kweli kweli..yaani anafikiri watz ni vilaza kiasihuki..hivi ni mbunge wa wapi huyu?
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Pia nimeikuta hii katika ukurasa wa Rais JK katika mtandao wa Facebook:

  Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku.

  Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao:

  Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakun...a mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.

  Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:

  Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili.

  Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu.
  Dar es Salaam.
  31 Januari, 2012
   
 10. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Huyu mama anakatisha tamaa kabisa,hata kwa hizo siku chache that is too much ,halafu sababu sio ya msingi sana,kama ni kupanda kwa maisha dodoma ati anavyodai yeye.

  Huyu mama ni tatizo la kitaifa,serikali ndo usiseme kushney hakuna kitu.Kitu urgent kama mgomo wa madaktari huezi kusema ati una andaa makaratasi ya kutoa taarifa,kuandaa makaratasi huko kutachukua muda sana.Serikali haijui ku act,haiwezi kuwekewa matumaini na wananchi,Serikali inapishana katika kusema,Raisi hivi,waziri mkuu vile.This is really the hopeless government.Naona Miaka 4 iliyobaki tutateseka sana.
   
 11. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hakuna mtu aliyesema wanakutana siku 365 achekupotosha na kupiga chenga hoja ya msingi. Hoja ya msingi hapa ni malipo ya TZS.330,000(200,000+80,000+50,000) kwa siku Moja kwa mbunge ambaye ameingia Bungeni.Iwe ameongea au amelala.Hii siyo sawa kabisa.Ubunge siyo professional ni WITO unajitoa kuwatumikia wananchi waliokuchagua sasa wao wamegeuza ajira.....
  "Shame on you na hili la posho litawatafuna na kuwagawa mpaka mtashangaa"
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mizee ya ccm nadhani pia imelogwa, wanamuogopa kweli jk nadhani sababu ni yakumwakwembeana ndo inawatisha hawa wazee. Ccm woote vilaza isipokuwa kingwangala na makamba tuu.
   
 13. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Hata wanapokuwa bungeni wanalipwa posho kwa lipi? Kusinzia? Kuna mbunge anaenda dom hata mdomo hafungui na aanalampa posho lol!
   
 14. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kumbe ile j,pili pinda alienda kama pinda na si serikali!!?
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa waandishi wa habari kweli wanajua maadili ya kazi yao? Kuandika habari za uongo ni kosa na ni upotoshaji umma
   
 16. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Heeheeeheeee para moja wanalamba POSHO hadi kesho yake kuendelea na para inayofuata!
   
 17. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  huko Ikulu sielewi wanakanusha nini waka Rais ni kweli ametia saini kubariki posho hizo na wabunge wamekwishawekewa kwenye accounts zao!
   
 18. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  huko Ikulu sielewi wanakanusha nini wakati Rais ni kweli ametia saini kubariki posho hizo na wabunge wamekwishawekewa kwenye accounts zao!
   
 19. don-oba

  don-oba JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 1,384
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hana mume, ana mdomo ivo ataishi na mume?
   
 20. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ndiyo maana yake mkuu anamaanisha kabum kenyewe ni kamda mfupi tukachunie tu.
   
Loading...