MAKINDA: Swala la Lema sitalirudisha bungeni (Amehofia nini?) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAKINDA: Swala la Lema sitalirudisha bungeni (Amehofia nini?)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kipre tchetche, Feb 17, 2011.

 1. K

  Kipre tchetche JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa maneno haya ya spiker Ana makinda anataka
  kuwaambia nini watanzania na watu wa Arusha?
  Je hii sio mwanzo wa kushindwa kuliendesha bunge?
  Je atahimili au yeye ndie atakuwa chanzo cha uvunjifu wa Amani? Nawasilisha :source magazeti ya Leo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Katika hili Spika Makinda umelikoroga
  [​IMG]

  Shehe Semtawa

  [​IMG] KUCHAGULIWA kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, kulizua mabishano kutoka kwa wadau mbalimbali kuwa asingeweza kuongoza Bunge hilo, kwa kile kilichoelezwa kuwa jazba alizonazo zingeshindwa kuamua mambo ya msingi.
  Spika huyu amerithishwa nafasi hiyo kutoka kwa aliyemtangulia, Samuel Sitta, ambaye alionekana kukubalika miongoni mwa jamii kutokana na uendeshaji wake wa Bunge lililopita.
  Kabla hata ya kufikia nusu ya mwaka tangu kuanza kwake kazi, spika huyu amekuwa akionyesha dosari mbalimbali katika kusimamia vikao vya Bunge, kitu ambacho kinawapa nafasi waliokuwa wakimpinga kupata nguvu ya kudhihirisha maneno yao ya awali.
  Makinda, anatumia vibaya kiti chake kwa kudhani kuwa yeye ni mwelewa wa kila kitu kuliko wengine, wakati sivyo, kwani wapo wengi wenye uwezo wa kufanya kazi ile.
  Atambue kuwa huu si wakati wa kuburuzana, kwani kila mmoja katika nchi hii ana haki ya kujieleza ili mradi hakuna kitendo chochote kinachoashiria uvunjifu wa amani katika yale yatakayoelezwa.
  Tukio la spika Makinda la hivi karibuni kuyaita magazeti kuwa ni sawa na barua hivyo hawezi kufanya kazi kwa kuyaamini, si la busara.
  Hatua ya Spika huyo kutamka maneno hayo ilifanyika baada ya mwandishi wa gazeti moja la kila siku kutoa maoni yake gazetini kuhusu staili ya uongozi wa spika huyo katika chombo hicho.
  Kwa hili nadhani Spika Makinda hakutenda haki kwa waandishi wa habari pia inasikitisha kwa mtu mweledi kama yeye kushindwa kutofautisha barua na gazeti.
  Kwa kumsaidia kidogo, barua ni taarifa inayoandikwa na mtu mmoja bila kupitiwa na zaidi ya mtu mmoja kwenda kwa mwingine, hiki ni kitendo cha mawasiliano kati ya mtu na mtu na si vinginevyo.
  Wakati gazeti ni chombo ambacho kinaongozwa na kundi la watu ambao wana taaluma ya uandishi wa habari ambayo ina miiko yake kikazi.
  Ni wajibu wa spika kuelewa kuwa kwenye vyombo vya habari hakuna kukurupuka bali kila kinachoandikwa huwa kinapembuliwa kwa lengo la kuielimisha jamii kinachotokea.
  Nashindwa kuamini kuwa spika kweli hajui maana halisi ya gazeti ambalo huwa linakuwa na safu kama maoni ya mhariri, makala za mahojiano, uchambuzi wa nyanja mbalimbali, habari za michezo na burudani, mashairi na hata barua za wasomaji na mambo kadha wa kadha.
  Kama kweli havielewi hivi basi nadhani umefika wakati yeye kutambua kuwa kuna vitu hivyo ambavyo vinatumia katika nyakati mbalimbali katika magazeti.
  Ni wakati pia kwake kuitambua vizuri tasnia hii ya habari kuwa ni pana, kinyume na anavyoifikiri pamoja na wengine, wakiwemo baadhi ya wanasiasa.
  Hata hivyo, anaweza kutusaidia katika kusoma kwake kama aliwahi kufundishwa na walimu aliyokutana nao kuwa gazeti ni barua, atuambie.
  Uandishi wa habari ni fani iliyotukuta na yenye kuaminika miongoni mwa jamii kutokana na kuibua mambo mbalimbali ikiwamo ufisadi kinyume inavyotazamwa na kuchafuliwa na watu wachache wasiopenda kufuata maadili ya kazi zao na haki za wengine.
  Katika hali ya kawaida, spika hapaswi kudharau magazeti, kwani hata kufika kwake hapo kwa njia moja au nyingine kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari mbalimbali yakiwamo magazeti anayoyaita barua.
  Leo itakuwa ajabu kwa spika kutoa lugha za kebehi kuwa hawezi kufanya kazi kupitia magazeti ambayo anayaona kuwa sawa na barua.
  Kwa hili ukiwa kama mwanadamu kubali umepotoka na huna budi kuomba radhi.
  Kwa mtazamo wangu, sitaki nikuone kuwa wewe ni bora kiongozi, bali nataka uwe kiongozi bora, hivyo ni vema kuacha kuwadharau wale ambao hawajaonyesha dharau katika kazi zako ambazo kwa kiasi kikubwa zinahitaji msaada wa wana habari.
  Ukiwa kiongozi wa wananchi unapaswa kuwa mvumilivu pale unapo kosolewa kwani kama ungekaa nyumbani kwako hakuna ambaye angejaribu kukuelekeza jinsi ya kufanya kazi kwa kufuata kanuni.
  Si vizuri kuingia kwenye mgogoro na wanahabari hadi kufikia hatua ambayo huko nyuma iliwahi kutokea kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Omar Mapuri.
  Kwa kuwa Bunge hili ni fupi, bado unao muda wa kutoa tamko kuhusiana na kauli yako ile ambayo kwa kiasi kikubwa haikubaliki kwa tasnia ya habari.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Ni dhahiri Makinda amegundua ya kuwa jazba zake zitampeleka kubaya.............................Lema alichomba ni mwongozo lakini yeye Anne akaamua kumlazimisha Lema amtuhumu Pinda kuwa kasema uongo wakati sivyo..........................Lema alichoomba ni mwongozo tu wa nini kifanyike wakati Mheshimiwa Mbunge amegundua ya kuwa PM amelidanganya Bunge........................................

  Spika angelikuwa mwangalifu angempa Lema mwongozo siyo kumlazimisha kumtuhumu PM wakati hata hansard zinathibitisha ya kuwa hakufanya hivyo............................Jitihada za Mnyika kumnusuru Spika hazikuzaa matunda kwa sababu Anne Makinda alifikiri kwa wakati ule hili suala lingempa umaarufu wa bei ya chei baada ya kukutana na washauri wake wa karibu amegundua ni yeye na PM sasa wako kikaangoni..........................................kwa sababu ni ukweli usiopingika ya kuwa Pinda alisema uongo Bungeni alipodai Chadema ndiyo chanzo cha vurugu Arusha wakati hakuna ushahidi wowote ule alioutoa Bungeni kuthibitisha tuhuma yake hiyo....................

  Kulingana na kanuni za Bunge huo ni uongo...................................

  Anachofanya Anne hivi sasa ..........ni damage control................................lakini hilio bado litamlazimu Pinda aliombe radhi Bunge kwa kusema uongo kwa maana ya kutoa tuhuma dhidi ya Chadema huku hakutoa ushahidi wowote ule......................
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  Kwanza amuombe radhi Kamanda Mheshimiwa Godbless Lema kwa kumuita mtovu wa adabu. Aombe radhi laivu au asome ushahidi wa Lema au Lema aweke mambo hadharani juu ya kile alichoandika kwenye ushahidi wake.

  Huyu mama siyo kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
   
 5. Double X

  Double X Senior Member

  #5
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uyu mwanamke kwakweli bunge limeshamshinda hata ukimuona amekaa pale mbele ni mtu wa kutojiamini kabisa.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kama fomu ya uspika alichukuliwa na mafisadi wakampelekea njombe aijaze unategemea nini???lazima alipe fadhila hana lolote huyo mama.....amewekwa kulinda mafisadi na yeye fisadi mkubwa ametutia aibu wana iringa
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,133
  Trophy Points: 280
  Aombe radhi au hiyo ushahidi usomwe bungeni.
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  toka mwanzo mi nilisema hakuna spika hapa...watu wakabisha kiko wapi sasa
   
 9. L

  LAT JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Lema atoe ushahidi wake kwa wananchi ili na wananchi waweze kutoa uchambuzi na hukumu yao dhidi ya pinda
   
 10. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Maskini Mzee Sitta umetuachia kiti cha uspika wakati bado tunakuhitaji... leo bunge limegeuka kijiwe cha mafisadi kiasi kwamba Makinda ananadi kamati muhimu za bunge kwa Makamba na Lowasa.
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  PM yuko sahihi kabisa na hakusema uwongo, nyie CHADEMA mliisha pewa agizo la kuacha maandamo, kwa utovu wenu wa nidhamu, kujitafutia umaarufu kwa gharama za maisha ya watu na kujifanya wajuzi kama sio wajuvi, ndiko kuliko sababisha mauaji na vurugu za Arusha.
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Feb 17, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Kwanza ieleweke vema, na nadhani wengi hawafahamu, Mh Lema hakumtuhumu Pinda. Baada ya maelezo ya Pinda aliomba mwongozo wa spika kutaka kujua kiongozi anayeongea uongo hi hatua gani anazochukuliwa. Hakumtaja pinda bali kiongozi.
  Maoni yangu: Mh Lema hakupaswa kujibu kama alivyoagizwa na Spika Makinda, kwasababu aliomba muongozo na si kumtuhumu mtu.

  Makinda: Kwa kutaka kuonyesha kuwa anajua zaidi na pengine kuwafurahisha wale waliomfikisha hapo, akakurupuka kutoka kusikojulina na kumuagiza Mh Lema alete maelezo. Hii ipo kwenye Hansard za bunge. Kibaya zaidi hakusema apeleke ofisini kwake bali apeleke bungeni.

  Majibu: Nimesoma majibu ya Mh Lema (Raia mwema), kwakweli ni afadhali Makinda ameepusha aibu kwake binafsi na kwa waziri mkuu. Majibu yale yameandaaliwa na Vichwa vilivyotukuka vya Chadema. Kama Makinda haelewi basi zifanywe jitihada zaidi za kuanzisha tuition baada ya vikao vya bunge.

  Mwelekeo: Huyu mama amedhamiria kuwakwamisha Chadema kwa kulinda maslahi binafsi ya kundi fulani. Amekataa hoja binafsi, na jana Mnyika ameomba suala la umeme lijadiliwe, Makinda akalirudisha katika kamati ya January kwani huo ndio ulikuwa mpango wao. Hoja nzito zipelekwe kwenye kamati. Sasa sijui watu watajadili vipi Richmond/Dowans ikiwa mwenyekiti wa kamati ya nishati ni January, na kamati ya Ulinzi na mambo ya nje (inayowahusu wawekezaji ) ni Lowasa.
  Chadema jipangangeni maana bunge limezibwa kila mahali na Mafisadi. Hili kundi la mafisadi linayumbisha nchi sio siri. Lina nguvu sana na sasa naelewa kwanini Mh Pinda aliwahi kusema ni watu hatari sana.
   
 13. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Crap!
   
 14. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Mkuu hapo umenena. This is what i was looking for. Umbumbumbu wa spika huo...
   
 15. A

  Akiri JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145


  nahisi malaria yamekupanda kichwani, au mwendawasimu fulani, au unatoa maoni yako ukiwa hujavaa nguo hata moja
   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #16
  Feb 17, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Usichokijua ni kuwa maandamano si zawadi, ni haki ya msingi na ya kikatiba ya mwananchi. Katiba ya nchi yetu inaeleza. Lakini hata kule kuliko na udikteta kama Misri bado watu walisimamia haki hiyo. Leo Baharain wanakolipwa mishahara bila kufanya kazi wanaandamana, Libya Gaddafi ana hali ngumu n.k.
  Hakuna sababu ya kuwazuia watu kuandamana kwa amani, na aliyeanzisha vurugu ni polisi, hata Waziri wa mambo ya ndani Membe amekiri mbeye ya jumuiya ya wanadiplomasia kuwa haki ya kuandamana ni ya msingi na polisi walitumia nguvu nyingi bila sababu.
  Kuthibitisha kuwa Waziri mkuu Pinda alisema uongo, Mh Lema ametoa hoja zake na amezuiwa kuzisema bungeni. Lakini hoja zake zimepatikana na zipo magazetini. Nenda kasome gazeti la Raia Mwema mtandaoni utajua nini kilitokea. Kukudokezea tu, PM alisema raia waliouawa ni 3, ukweli ni kuwa ni 2 na mmoja Njuguna ni wakenya si wa Tanzania. Endelea kusoma kule Raia mwema.
   
 17. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na Romana Mallya  17th February 2011

  [​IMG]
  Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (Chadema)  Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema uamuzi kuhusu suala la Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (Chadema), hautarudishwa bungeni na badala yake anakusudia kulimaliza mwenyewe.
  Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na NIPASHE kuhusu uamuzi wake baada ya Lema kuwasilisha vielelezo vyake vya kutetea hoja yake kama alivyotakiwa na Spika.
  Alisema taratibu zinazoendelea ni za ndani na hataziweka hadharani kuanzia sasa kwa kuwa ana uwezo wa kulimaliza mwenyewe.
  "Jana (juzi) Lema aliwasilisha vielelezo kimaandishi kama Bunge lilivyomtaka, kuhusu hatua gani atachukuliwa, hizi ni taratibu za ndani siwezi kuziweka hadharani," alisema.
  Lema alitakiwa kutoa ushahidi wa alichokisema baada ya kuomba mwongozo wa Spika akitaka kujua hatua ambazo mbunge anazoweza kuchukuliwa iwapo atagundua kiongozi mkubwa wa serikali kama Waziri Mkuu, amelidanganya Bunge.
  Akitoa ufafanuzi wa mauaji yaliyofanywa na polisi Arusha Janauri 5, mwaka huu, katika kipindi cha maswali na majibu siku hiyo ya Alhamisi iliyopita, Pinda alisema Chadema ndiyo chanzo cha vurugu hizo kwani walikataa ushauri waliopewa na polisi.
  Pinda alikuwa akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, (Chadema) kutaka kusikia kauli ya serikali juu ya mauaji hayo, kama serikali ilikuwa tayari kuunda Tume kuyachunguza na kuwawajisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema.
  Katika maelezo yake, Pinda pamoja na kueleza kusikitishwa na mauaji hayo huku akisema hayakuwa na sababu, aliwalaumu viongozi wa Chadema kwamba walikuwa kiini cha kutokea kwake kutokana na kukaidi ushari wa polisi wa kutumia ruti (barabara) waliyoelekezwa.
  Pia alisema chama hicho kiliwahamasisha wananchi kwenda kuvamia kituo kikuu cha polisi cha Arusha ili kuwakomboa viongozi wa chama hicho waliokuwa wakishikiliwa hapo kwa kushiriki maandamano.
  Baada ya majibu ya Pinda ndipo Lema aliposimama na kuomba mwongozo wa Spika, lakini Spika hakuridhika na maneno yaliyotolewa na Lema hivyo akampa siku tano awe amewasilisha ushahidi wa kile alichosema.
  Lema aliomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni namba 64 ya Bunge kutaka kufahamu iwapo Waziri Mkuu atakuwa ametoa maneno ya uongo bungeni, Mbunge anapaswa kuchukua hatua gani kuhusu suala hilo.
  Spika Makinda akitumia kanuni namba 63 na vipengele vyake vyote vinane, alimtaka Lema kuwasilisha uthibitisho kwamba Waziri Mkuu alikuwa ametoa maelezo ya uongo bungeni alipokuwa akielezea kiini cha mauaji hayo na alimtaka awasilishe vielelezo hivyo ndani ya siku tano.
  Makinda alisema mbunge akishindwa kuthibitisha kauli aliyoitoa bungeni anaweza kukabiliwa na adhabu ya kusimamishwa kushiriki vikao vitano.
  Kadhalika, alisema iwapo wabunge wataona adhabu hiyo ni ndogo wanaweza kupendekeza adhabu kubwa zaidi kuchukuliwa dhidi yake.  CHANZO: NIPASHE
   
 18. LD

  LD JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Usitake ionakane wanawake hawawezi Mheshimiwa!!
   
 19. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Ambacho hatakipeleka bungeni ni ule ushahidi aliyomtaka Mheshimiwa Lema aupeleke tarehe 14. Kama hawezi kuupeleka bungeni basi ajibu hoja ya Mhe. Lema iliyotaka mwongozo wa Spika, kama waziri mkuu akilidanganya bunge na umma anachukuliwa hatua gani, na baada ya hapo asubiri aone Lema ama wabunge wengine watataka nini baada ya majibu yake, siyo kuligeuza bunge kama bedroom yake na kusema hovyohovyo kwasababu tu yeye ni spika.
  Haka kamama ni kadikteta fulani hivi.
   
 20. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwa ukurupukaji wake,makinda hana ubavu wa kuongoza bunge hili!!
   
Loading...